habari wakuu, leo nimekuja na mrejesho. niliwahi post humu mwezi uliopita kuwa nimekatwa 6,000 kama deni kodi ya majengo ilihali mimi mita yangu ina miezi miwili tu.
sasa mwezi huu (leo)nimenunua tena umeme nimekatwa 6,000 ikabidi nipige simu TANESCO majibu niliyopewa hakika yanavunja moyo.
jengo nimejenga mwaka huu, tangu likamilike halina hata miezi mitatu. lakini tanesco wameniambia hiyo 12,000 niliyokatwa kwa miezi miili nimelipia kodi ya jengo katika kipindi cha mwaka wa fedha kuanzia mwaka jana mwezi wa 7 au 8 hadi mwaka huu mwezi wa 7 au 8 mwaka wa fedha utakapoisha.
na wakati huo huo naambiwa kuanzia mwezi unaofuata nitakuwa nakatwa 1,000. sasa kama ni mwaka wa fedha na washachukua 12,000 tayari na mwaka wa fedha haujaisha mbona kama ntaliwa tena pesa au mimi ndio sijui mwaka wa fedha ni mwezi wa ngapi unaanza.
na kwanini nikatwe miezi ya nyuma ilihali sikuwa na jengo lolote.?