Kodi ya majengo kupitia luku baadhi ya watu wanaumia Kwa kuibiwa

Kodi ya majengo kupitia luku baadhi ya watu wanaumia Kwa kuibiwa

Nadhani Kuna kikundi lipo kwenye mfumo kimetengeza mrija wa kuwaibia watu wanachofanya ni kutwist system Kwa kubambikiza deni randomly Kwa baadhi ya wateja,nchi hii wizi umeota mizizi,Wanachofurahia Hawa wezi ni kuwa wengi tunaobiwa ni wapifa kelele zisizokuwa na impact yoyote(rejea ripoti ya CAG),yaani tumekuwa nyuki wa mashineni ila wanachopaswa kujua Kuna siku tutaamuka na hakuna atakayeweza kuzuiwa hasira zetu.
 
Tanesco imesema kuwa kwa sasa makadirio yamepanda
Kwa wenye ghorofa ni 60,000 kwa Mwaka
Hivyo kila mwezi wanakata 5000

Wengine ni 12,000
 
Kuna tangazo wametoa jana
 

Attachments

  • FB_IMG_1683214954185.jpg
    FB_IMG_1683214954185.jpg
    57 KB · Views: 17
Nyumba yangu Ina luku nne na wanakata zote, nilipokwenda kulalamika TRA wakaniambia ngoja watizame kama kuna wapangaji ili wanilipue na15% ya kodi ninayo lipwa.
Sikurudi tena🙄
🤣🤣🤣
 
Kuna tangazo wametoa jana
Hii ni kama ku discourage kujenga maghorofa.
Mimi naona wenye maghorofa ndio wangepewa unafuu zaidi ili ku encourage ujenzi wa maghorofa zaidi maana wanasevu maeneo kwa kuitumia vilivyo ardhi tuloyonayo.
Hata kama kusingekuwa na upendeleo huo, haiingii akilini eti mwenye sakafu mbili analipa 10,000 kwa mwezi wakati mwenye sakafu moja (nyumba ya kawaida)anakipa 1,000 tu kwa mwezi.
Nadhani kuna haja ya kuviangalia upya hivi viwango ili kuweka usawa miongoni mwa wananchi.
Viwango hivi vilivyowekwa vinatengeneza matabaka miongoni mwa wananchi, kitu ambacho ni hatari kwa mstakabali wa umoja wetu.
Au nasema uwongo ndugu zangu?
 
Ukiwa na Deni linakatwa mara moja. Hutaweza kununua umeme mpaka ulipe deni lote. Hata kama unadaiwa laki moja, itabidi ulipe deni lote kwanza ndio upate umeme

Binafsi leo nimekatwa laki moja kama deni.
Naomba kufahamishwa kulingana na hiki walichokata kama deni kwa kila mwezi watakuwa wanakata kiasi gani ili niweze kujipanga.
Natanguliza shukrani.
 
Hata ukienda Tanesco hakuna kitu kitabadilika. Kuna mmoja alipata hiyo changamoto mwaka jana, alihangaika Tanesco Ila mwisho akaamua kukubali matokeo.
Mimi mbona nilipeleka barua na nilifanyiwa marekebisho.
 
Wahusika Leo wamerekebisha mfumo,ukiwa unadaiwa kiwango chako Cha deni kiaoneshwa,hoja yangu ya pili nadhani imeaanza kujibiwa,haiwezekani kukisia deni unaponunua umeme,LAKINI ishu ya wizi Bado IPO inaexist,Kuna mteja ameingiza umeme march 2023 Leo kaja kununua umeme anambiwa anaedaiwa 18000 hii sio fair,labda wamemterm kama anaghorofa
 
Wahusika Leo wamerekebisha mfumo,ukiwa unadaiwa kiwango chako Cha deni kiaoneshwa,hoja yangu ya pili nadhani imeaanza kujibiwa,haiwezekani kukisia deni unaponunua umeme,LAKINI ishu ya wizi Bado IPO inaexist,Kuna mteja ameingiza umeme march 2023 Leo kaja kununua umeme anambiwa anaedaiwa 18000 hii sio fair,labda wamemterm kama anaghorofa
Naomba nisaidie namna ya kufahamu/ kuona kiasi kinachodaiwa.
Moja ya nyumba yangu niliunganisha huduma ya umeme mwezi Februari. Mara ya mwisho nilinunua umeme mwezi Machi, lakini jana nilivyonunua umeme nilikatwa Tshs. 12,000/=.
Kifupi nilishindwa kuelewa makato hayo ni kwa ajili ya nini. Aheri wangekata elfu 3 kwa maana ya kodi ya miezi mitatu ya Machi, Aprili na Mei.
Napata wasiwasi isije kuwa kampuni yenye zabuni ya kusimamia "software" ya Tanesco inashiriki katika wizi wa mtandao au vinginevyo.
 
Tanesco imesema kuwa kwa sasa makadirio yamepanda
Kwa wenye ghorofa ni 60,000 kwa Mwaka
Hivyo kila mwezi wanakata 5000

Wengine ni 12,000
Naona mambo ya sensa
Kazi yake ishaanza kuonekana

Ova
 
Back
Top Bottom