meningitis
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 8,425
- 4,768
Jana nilimsikiliza Waziri Mwigulu pale TBC nikapata mashaka sana na kuona ameamua kudanganya kutaka kuupooza umma.
Akijaribu kufafanua amedai kuwa makato ya tozo hizi yanaenda kwenye huduma za afya haswa afya ya mama na mtoto.
Ningependa atoe ufafanuzi wa asilimia ngapi ya tozo itaenda huko?
Kwenye Bajeti ya Afya sijaona ongezeko la kipekee au special kwa mwaka huu wa fedha unaloweza kusema litatokana na makato ya simu.
Mfano mwaka wa fedha uliopita kila jimbo lilipata zahanati 3. Je, mwaka huu wa fedha zitaingezeka na kuwa sita au zitabaki vilevile?
Kwenye bajeti sioni ongezeko lolote la bajeti ya Zahanati.
Pia sijaona fedha maalum eti kwa ajili ya mama na mtoto tofauti na ongezeko ambalo ni routine.
Kwa ufupi, Afya imesingiziwa tu hakuna ushahidi wa kibajeti unaoonesha kuwa tozo hizi zitaenda kuboresha afya. Kama nia ya kweli ipo basi fedha za tozo ziende moja kwa moja kwenye vituo vya huduma za afya.
MWIGULU PAMBANA NA HALI YAKO usisingizie afya!