SoC01 Kodi ya Uzalendo: Ushauri wangu kwa Serikali jinsi ya kuthibiti na kujenga imani kwa walipaji

SoC01 Kodi ya Uzalendo: Ushauri wangu kwa Serikali jinsi ya kuthibiti na kujenga imani kwa walipaji

Stories of Change - 2021 Competition

Tomaa Mireni

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2015
Posts
2,395
Reaction score
2,391
Kutokana na makusanyo mapya ya kodi ya uzalendo kupitia miamala ya simu,serikali iandae system ya wazi kutrack hizi tozo na kuonyesha kila mchangiaji.

Itapendeza sana kama watanzania tutaona wenyewe kupitia system itakayoandaliwa iwe ni website au app. Kama walivyofanya CDM mwaka fulani kuona kiasi kinachochangiwa.

FAIDA YA HIYO SYSTEM.
  • Kwanza itamuahamasisha mlipaji.
  • Pili ni rahisi kufuatilia kiasi kilichopo na kilichotoka.
  • Tatu itajenga imani katia ya mlipaji na mpokeaji (serikali)
  • Nne kuthibiti wizi(ngumu fisadi kufikiria jinsi ya kuziiba sababu tutazihoji)

Hicho chama kilifanikiwa sana kwenye kipande hicho,na kila mtu aliona kwa uwazi ukituma tsh 100 unaona kwenye huo muundo (sio lazma kuonyesha majina)

Kama inavyofanya mitandao ya simu serikali pia inaweza kufanya hivyo hata kwa wasio kuwa na simu janja. Yani kuwe na options mbili,ya App na USSD kwa wale wenye simu zisizokuwa na muunganisho wa data(viswaswadu,vitochi).

Je hili wazo linafaa au sio la ulazima?
 
Upvote 21
Akuna ushauri za ya kupunguza ayo makato ni makubwa mno ayavumiliki....

Yatau na kuzorotesha biashara nyingine zinazoleta kodi pia...
 
Mimi naona tatizo si kuona kilichopatikana Bali ni ukubwa wa tozo zilizowekwa ukilinganisha na haili ya kiuchumi ya wanainchi kwa sasa
 
Issue sio tu kwamba Kodi hio haitafanya kinachokusudiwa na kwa ufanisi..., Issue kubwa zaidi ni kwamba watu watapunguza miamala na kutafuta kufanya njia mbadala..., hence Serikali, Wananchi na Makampuni Kukosa hata kidogo wanachokipata
 
Sio kwa Tanzania, wenzetu Kenya tu wana huduma nyingi sana za kuchanja na lipa kwa...sasa kibongo bongo bado sana. Mpaka mtu atoe pesa ndio alipie huduma.
 
Sio kwa Tanzania, wenzetu Kenya tu wana huduma nyingi sana za kuchanja na lipa kwa...sasa kibongo bongo bado sana. Mpaka mtu atoe pesa ndio alipie huduma.
Mkuu watu wameshaanza kuliko kutuma pesa kwa mtu ukatwe elfu kumi anaona bora ampe boda buku apeleke au wapeane wakikutana ana kwa ana....,
 
Sio kwa Tanzania, wenzetu Kenya tu wana huduma nyingi sana za kuchanja na lipa kwa...sasa kibongo bongo bado sana. Mpaka mtu atoe pesa ndio alipie huduma.
Kabisa,ushawahi kusikia mtu kaporwa pesa kwenye nchi za wenzetu labda alikuwa anaenda bank?
 
Issue sio tu kwamba Kodi hio haitafanya kinachokusudiwa na kwa ufanisi..., Issue kubwa zaidi ni kwamba watu watapunguza miamala na kutafuta kufanya njia mbadala..., hence Serikali, Wananchi na Makampuni Kukosa hata kidogo wanachokipata
Afu mgawanyo wa tozo sio kwa asilimia kumbe!!
 
Back
Top Bottom