Lukonge
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 1,469
- 2,086
Mfanya biashara hawezI kuwa mlaji, yeye ni mtengeneza faida tu, na tayari kwemye mifumo ya kodi kuna kodi kadhaa analipa ikiwemo mapato,
Mfanya biashara anayeuza mbolea kwa mfano, anakuwaje mlaji wakati mbolea anatumia mkulima namtumbo huko?
Baada ya kusoma msingi mkuu wa wenzetu wakati wanaanzisha hii kitu nimegundua kuna shida kwenye mifumo yetu. Mfumo wa theory uko sawa, ila kwenye utekelezaji ndo kuna shida. Hii inaweza kutokana na mifumo yetu ya utekelezaji au watendaji wetu husika.
Hii inatokana na ukweli kuwa:
Kwa vitendo, mfumo wa VAT umezingatia mtengenezaji wa bidhaa, muuzaji wa jumla, muuzaji wa rejareja na mlaji wa mwisho. ILA kwenye utekelezaji ndo kuna KUKENGEUKA.
Twende na mtiririko huu:
Mfano:
Kama VAT ni 10% ni nini kinatakiwa na wapi tunakwama.
Soda iliyotengenezwa kiwandani:
1: Mtengenezaji atanunua materials ambazo zina 10% VAT. Materials ni shilingi 50, 10% ni shilingi 5. Atalipa shilingi 55.
A: shilingi 50 bei ya materials
B: shilingi 5 VAT(10%)
Atatengeneza kinywaji, atapiga gharama za uzalishaji pamoja na faida yake, atapiga 10% VAT. Kisha atalipa VAT serikalini kwa kutoa kiasi alicholipa kwenye materials.
Mfano:
Gharama na faida ni shilingi 60
Atapiga VAT10% atapata shilingi 6
Atauza kwa shilingi 66
Atalipa 10VAT kwa shilingi 6-5 = 1
Ina maana amelipa VAT ya thamani iliyoongezeka baada ya ile ya materials.
Ambayo ni sawa kabisa atakuwa amelipa shilingi 6 kwa jumla tangu materials mpaka kuuza.
2: Muuzaji wa jumla atapokea soda, atajumlisha gharama zake pamoja na faida atapiga VAT 10%. Atawakirisha VAT yake serikalini kwa kutoa ile iliyokwisha lipwa na mtengenezaji.
Mfano:
Gharama ya soda na faida ni shilingi 80. Atapiga 10%VAT, ambayo ni 8
Atalipa shilingi 8-6 = 2
Ambayo 6 ilishalipwa na mzaliahaji. Yeye anawajibika na shilingi 2 zilizoongezeka.
3: Muuzaji rejareja atapiga hesabu ya gharama na faida, atapiga VAT10%. Atawasilisha tofauti ya VAT yake na ile iliyolipwa na muuzaji wa jumla.
Mfano:
Gharama na faida ni shilingi 100.
Itapigwa 10%VAT, ambayo ni shilingi 10
Hapa, muuzaji atatakiwa kurejesha shilingi
10-8=2
Atarejesha serikalini shilingi 2
4: Mtumiaji wa mwisho, atanunua soda kwa gharama halisi na faida kwa muuzaji rejareja. Ataongezewa VAT10% zima yaani shilingi 10. Kwa nini?
Kwa nini huyu mnunuzi wa rejareja asilipe 10%VAT kwa kutoa anayotakiwa kurejesha serikalini muuzaji wa rejareja kama hapo juu namba 3?
Yaani kwa nini halipi shilingi 2 VAT badala yake ni shilingi 10?
Kwa sababu hapo ndo unakuwa umelipa gharama ya kiasi kilichoongezeka/value added toka kwa muuzaji wa jumla mpaka kwa muuzaji rejareja?
Hili ni swali kwa watendaji, je wanashindwa kufuata mnyororo na kuishia kurundika hii kodi kwa mlaji bila kujali?
Kama mifumo yetu haiwezi kunasa hizi factors zote hapo katikati basi irekebishwe kuwezeshwa au tubadili mfumo kwenda sales tax payment.