Kodi ya VAT ifumuliwe. It's a complex sales tax iliyojaa ujanja mwingi na upigaji. Itozwe kwenye source pekee as a sales tax na kusiwe na tax returns

Kodi ya VAT ifumuliwe. It's a complex sales tax iliyojaa ujanja mwingi na upigaji. Itozwe kwenye source pekee as a sales tax na kusiwe na tax returns

Mfanya biashara hawezI kuwa mlaji, yeye ni mtengeneza faida tu, na tayari kwemye mifumo ya kodi kuna kodi kadhaa analipa ikiwemo mapato,
Mfanya biashara anayeuza mbolea kwa mfano, anakuwaje mlaji wakati mbolea anatumia mkulima namtumbo huko?

Baada ya kusoma msingi mkuu wa wenzetu wakati wanaanzisha hii kitu nimegundua kuna shida kwenye mifumo yetu. Mfumo wa theory uko sawa, ila kwenye utekelezaji ndo kuna shida. Hii inaweza kutokana na mifumo yetu ya utekelezaji au watendaji wetu husika.

Hii inatokana na ukweli kuwa:
Kwa vitendo, mfumo wa VAT umezingatia mtengenezaji wa bidhaa, muuzaji wa jumla, muuzaji wa rejareja na mlaji wa mwisho. ILA kwenye utekelezaji ndo kuna KUKENGEUKA.

Twende na mtiririko huu:
Mfano:
Kama VAT ni 10% ni nini kinatakiwa na wapi tunakwama.

Soda iliyotengenezwa kiwandani:
1: Mtengenezaji atanunua materials ambazo zina 10% VAT. Materials ni shilingi 50, 10% ni shilingi 5. Atalipa shilingi 55.
A: shilingi 50 bei ya materials
B: shilingi 5 VAT(10%)

Atatengeneza kinywaji, atapiga gharama za uzalishaji pamoja na faida yake, atapiga 10% VAT. Kisha atalipa VAT serikalini kwa kutoa kiasi alicholipa kwenye materials.

Mfano:
Gharama na faida ni shilingi 60
Atapiga VAT10% atapata shilingi 6
Atauza kwa shilingi 66
Atalipa 10VAT kwa shilingi 6-5 = 1
Ina maana amelipa VAT ya thamani iliyoongezeka baada ya ile ya materials.

Ambayo ni sawa kabisa atakuwa amelipa shilingi 6 kwa jumla tangu materials mpaka kuuza.

2: Muuzaji wa jumla atapokea soda, atajumlisha gharama zake pamoja na faida atapiga VAT 10%. Atawakirisha VAT yake serikalini kwa kutoa ile iliyokwisha lipwa na mtengenezaji.

Mfano:
Gharama ya soda na faida ni shilingi 80. Atapiga 10%VAT, ambayo ni 8
Atalipa shilingi 8-6 = 2
Ambayo 6 ilishalipwa na mzaliahaji. Yeye anawajibika na shilingi 2 zilizoongezeka.

3: Muuzaji rejareja atapiga hesabu ya gharama na faida, atapiga VAT10%. Atawasilisha tofauti ya VAT yake na ile iliyolipwa na muuzaji wa jumla.

Mfano:
Gharama na faida ni shilingi 100.
Itapigwa 10%VAT, ambayo ni shilingi 10
Hapa, muuzaji atatakiwa kurejesha shilingi
10-8=2
Atarejesha serikalini shilingi 2

4: Mtumiaji wa mwisho, atanunua soda kwa gharama halisi na faida kwa muuzaji rejareja. Ataongezewa VAT10% zima yaani shilingi 10. Kwa nini?

Kwa nini huyu mnunuzi wa rejareja asilipe 10%VAT kwa kutoa anayotakiwa kurejesha serikalini muuzaji wa rejareja kama hapo juu namba 3?

Yaani kwa nini halipi shilingi 2 VAT badala yake ni shilingi 10?

Kwa sababu hapo ndo unakuwa umelipa gharama ya kiasi kilichoongezeka/value added toka kwa muuzaji wa jumla mpaka kwa muuzaji rejareja?

Hili ni swali kwa watendaji, je wanashindwa kufuata mnyororo na kuishia kurundika hii kodi kwa mlaji bila kujali?

Kama mifumo yetu haiwezi kunasa hizi factors zote hapo katikati basi irekebishwe kuwezeshwa au tubadili mfumo kwenda sales tax payment.
 
Alichokieleza mleta hoja:
1: VAT-mzalishaji
2: VAT-muuzaji wa jumla/wholesaler
3: VAT- muuzaji mdogo/retailer

1 na 2 zina return ni kweli, ila zinaathiri bei ya bidhaa sokoni kuwa kubwa. Mnunuzi ananunua bidhaa yenye 60% VAT au zaidi baada ya hizi VAT kuongezwa na zenyewe kwenda kujinyumbulisha/kuzaa.

Mfano: namba moja pia baada ya kujiongeza, itaongeza 18% ya namba mbili, namba tatu itachukua 1&2 pia pamoja na gharama nyinginezo/value added.

Kama kodi inalipwa na mnunuzi wa mwisho, kwa nini muuzaji wa mwisho/retailer ndo asiweke VAT baada ya mnyororo wote wa thamani kuongezeka?

Hii inatokana na kwamba mzalishaji wa mwanzo hatajua bidhaa aliyoizalisha hapo kwake ndo imeanza kuitwa bidhaa na yeye hawezi kujua itaongezeka thamani gani huki mbele. Inakuwa ni too theoretical kulipa VAT kwani bidhaa haijaongezeka thamani yake halisi/bado iko kwake.

Kama utekelezaji huo hauwezekani, basi itafutwe namna njema isiyo na athari kubwa kwa mnunuzi wa mwisho.

Ukweli ni kwamba kila mtanzania kuanzia akiwa tumboni mwa mama yake analipa kodi ya serikali bila yeye kujua kodi hiyo iko kwenye mfumo wa indirect taxation.

Mfumo huu ni very friendly na hakuna mtu wa kuukwepa hata kama ni mtoto mchanga. Kodi hii iko kwenye kila bidhaa au huduma anayonunua. Mama mjamzito hugawana chakula na mtoto wake aliye tumboni ambacho kalipia kodi.

Tatizo letu ni huu mfumo wa VAT wa kukusanya hiyo indirect taxes za bidhaa na huduma ambazo kila mtanzania hununua. Yaani mfumo uko complex uliojaa ujanja mwingi unaotoa mianya mingi kwa pesa hizo nyingi kuishia kwenye matumbo ya wajanja.

Mfumo wenyewe uko hivi: Chukua mfano kiwanda kinachozalisha bidhaa fulani hususani sementi. Baada ya uzalishaji kiwanda kinapanga kuuza hiyo sementi TZS 10,000 kila mfuko kikiwa kimezingatia gharama na faida ya uzalishaji huo na ushindani wa soko uliopo. Serikali haingilii bei hiyo ya mwenye kiwanda (which is very good).

Badala yake inamwambia serikali inamwambia huyo mwenye kiwanda aongeze TZS 2,000 kwenye kila mfuko ambayo itakuwa ni kodi ya serikali atakapoiuza (sales tax). Hadi hatua hiyo bado ni very good.

Tatizo na ujanja unaanzia baada ya hatua hiyo. Serikali inamwambia huyo mwenye kiwanda kwamba hiyo TZS 2,000 kwa kila mfuko serikali itamrudishia mwenye kiwanda baada ya serikali (TRA) kupata (VAT) tax returns kutoka muuzaji wa mwisho wa rejareja (retail) aka mmachinga huko Sumbawanga.

Mwenye kiwanda huuza bidhaa zake kwa wholesalers. Hivyo mfuko mmoja wa sementi mwenye kiwanda atamuuzia wholesaler kwa TZS 12,000. Huyu wholesaler naye atapanga bei atakayoiuza hiyo sementi huko Sumbawanga akizingatia gharama ya usafirishaji, faida yake na ushindani wa soko. Bei yake inaweza ikawa TZS 15,000 kwa kila mfuko. TRA itamwambia aongeze TZS 2,000 kama kodi ya serikali (VAT) ambayo atarudishiwa baada huyo atakayemuuzia (retailer) kurejesha tax returns. Hivyo wholesaler atamuuzia retailer mfuko mmoja wa sementi kwa TZS 17,000.

Huyo retailer naye atapanga faida yake na kuona aiuze kwa TZS 20,000. Naye TRA itamwambia aongeze TZS 2,000 kwenye bei hiyo kama VAT na atoe risiti na tax returns. Hivyo bei ya mfuko mmoja wa sementi anaiuza kwa mlaji kwa TZS 22,000.

Katika mfumo huo wa VAT huyo retailer anatakiwa kuandaa na kuwakilisha VAT returns za bidhaa aina zote alizouza kila mwezi ili kuwezesha hao wholesalers na wenye viwanda (source) warejeshewe hizo TZs 2,000 zao. Yeye harudishiwi cho chote.

Mlaji wa mwisho anakuwa ameongezewa TZS 2,000 mara tatu kwenye hiyo thamani ya bidhaa lakini serikali sana sana inaambulia TZS 2,000 tu! Hapo utaona kuna myanya ya wenye viwanda na wholesalers kurejeshewa hizo TZS 2,000 kwa maelewano tu na maafisa wa TRA.

Hapo utaona mapambano ya maafisa wa TRA na retailers kuhusu risiti na tax returns ambao huishia mara nyingi kwa retailers kutoa rushwa kwa maafisa hawa.

Hivyo ndivyo ulivyo mfumo huu wa VAT kwa bidhaa zingine zinazotoka nje ya nchi na ndani ya nchi. Inashangaza zaidi kuwa hata bidhaa zinazozalishwa na taasisi zinazomilikiwa kwa asilimia 100% na serikali nazo zinawekewa kodi ya serikali, yaani serikali inajitoza kodi?

Shirika kama la TANESCO miradi yake imejengwa kwa pesa yetu (kodi zetu). Hata kama baadhi ya pesa iliyotumika tulikopa nje bado kodi zetu zitalipa hilo deni letu. Ni shirika letu, sasa linawezaje kututoza kodi? Sisi ndiyo wenye mamlaka ya kupanga umeme tulipe kwa bei gani ili kuwezesha kulipa mishahara na other charges (OC) za shirika letu zilizopitishwa na bunge letu la bajeti. Ziada ikipatikana inaweza kugharimia mambo mengine hususani madawa na vifaa tiba.

Hitimisho: VAT is nothing but a sales tax. Itozwe mara moja tu kwenye chanzo ya hiyo bidhaa. Kama bidhaa inazalishwa hapa nchini basi huyo mwenye kiwanda pekee ndiye atozwe/ akusanye hiyo kodi na kuiwakilisha serikalini baada ya kuuza bidhaa hiyo.

Hao wholesalers na retail sellers na machinga haiwahusu maana serikali itakuwa ilishachukua kilicho stahili yake. Kama bidhaa inatoka nje ya nchi, serikali ichukue kodi yake pale pale mipakani inapoingilia.

Kwenye zingine kama zile za kilimo na mifugo kodi hii ilipwe kwenye minada mikubwa kutoka kwa wafanya biashara wakubwa wanaonunua bidhaa hizo. Mambo ya kurudishana kodi yawe mwisho.

Kazi ya watumishi wa TRA iwe kwenye maeneo haya tu na kushirikiana na polisi kunasa bidhaa zinazoingia kwa magendo kupitia panya routes. Serikali ni moja. Mambo ya kodi za serikali za mitaa na kodi za serikali kuu (TRA) hayana maana kwa mwananchi.

Zote kwake ni za serikali, wao watajua wanagawana vipi. Mambo ya direct taxations tuachane nayo au yapunguzwe kabisa. Yana maudhi sana na kuwafanya wananchi waichukie serikali yao. Imagine kama kodi ya kichwa ikarejeshwa hata kama ni buku moja tu kwa kila kichwa kwa mwaka, unadhani itakuwaje?
NIFUNGE MJADALA KWA KIFUPI TRA
WANAWAIBIA WANANNCHI KWA KUPITIA WIZI UNAOITWA VAT NA ALAANIWE MUANZILISHI WA VAT
 
NIFUNGE MJADALA KWA KIFUPI TRA
WANAWAIBIA WANANNCHI KWA KUPITIA WIZI UNAOITWA VAT NA ALAANIWE MUANZILISHI WA VAT
Walaaniwe hao waliocopy na ku paste bila kuzingatia hali ya uchumi wetu.
Vat inataka stable chain ya mzalishaji na mlaji kitu ambacho first class world wamefanikiwa
 
Back
Top Bottom