We nae ni Waziri wa Ajabu sana. Kodi haziwezi kuleta maendeleo kama mtaendelea kufanya
overspendings zisizo na kichwa wala miguu, mfano mdogo tu Mnatumia takriban
nusu trilioni(Kwa mujibu wa gazeti la mwananchi) kununua magari mapya kwa mwaka, hivi kwa nchi masikini kama Tanzania hizi ni akili au matope?
Mmetengeneza departements nyingi nyingi ambazo hazina umuhimu na zina uwezo wa kuwa merged kuwa departments moja.
Safari za nje kibao, Mnashindwa nini kutumia serikali mtandao mkafanya hivyovikao online ili kusave pesa za umma?
Serikali kwa kauli ya Mh Rais anakili kuna wizi(Japo wewe unakanusha) sasa unategemea hizo kodi zitafanya nini cha maana kama kuna upigaji?
Wewe kama kweli ni waziri msomi (Which I highly doubt) fanya yafuatayo.
1)
Implement Zero Based Budgeting.
Kila idara ya serikali itengeneze bajeti yake from scratch acheni ku edit templates za previous years. Hii itasaidia kuondoa unnecesary expenditures
2)
Cut Non-Essential Travel and Allowances.
Mambo mengine ni ya kujiongeza tu, badala ya kupeleka wasanii wanaoigiza ujinga ujinga nje, kwa nini hizo pesa msitumie kusomesha radiologist na kada nyingine za afya ambazo zina uhitaji wa hali ya juu (Value for Money)
3)
Acheni upigaji na wapigaji wachukuliwe hatua, Miaka karibu miwili mfululizo CAG anaripoti madudu kibao lakini hakuna kinachoshughulikiwa(Kwanza ningekuwa CAG ningeshajiuzulu maana hizo ni dharau). Hivi hamuoni aibu unaiba pesa za umma ukanunue magari sijui ukajenge majumba ya kifahari I swear yatawatokea puani MUNGU HADHIHAKIWI.
4)
Mnakusanya kodi kwa maguvu badala ya akili.
Unasema walipa kodi Tanzania ni chini ya asilimia 20 tu, umeshafanya tafiti ukajua kwanini asilimia 80 hawalipi kodi???? Mbona majibu yapo wazi?
5
) Kama kweli mna uzalendo mawaziri wote (Ambao kimsingi ni wabunge) Mishahara yenu ya mawaziri ikatwe nusu na pia msilipwe kama wabunge.
Ile sheria ya kuwalipa wake wa vigogo wastaafu ni sheria ya kipuuzi ifutwe haraka sana (President Ruto amefuta huu ujinga). Sheria ziko wazi serikali haiwezi kufanya malipo mara mbili mbili kwa mtu mmoja huyo huyo mke wa mstaafu lakini yeye mwenyewe bado yupo bungeni au serikalini.
6)
Magari ya kifahari sijui VXR sijui V8 mwisho kwa mawaziri na majaji basi.
Watumishi wengine sijui wakuu wa mikoa, sijui ma dc sijui RAS , DAS wote hao wapewe Totoya Vanguard au kama mnataka durability basi Land cruiser hardtop zinawafaa. Hii itasaidi kupunguza spendings zisizo na kichwa wala miguu. Imagine nchi masikini kama Tz RAS anatembelea gari ya 300M+ (Ila nyie mna dhambi nyie Mungu awasaidie sana mbadilike)
Yes tunajua nchi yetu haiwezi kujiendesha yenyewe kwa kutegemea bajeti ya ndani. Hii ni kweli kabisa sasa punguzeni matumizi yasio ya lazima, kamateni wabadhirifu, wekeni kodi rafiki kulingana na kipato cha mtu bila kumkandamiza, Haiwezekani niagize kifaa cha 30,000 Alibaba halafu kikifika mnataka nilipe kodi ya 30,000 yaani thamani ya kifaa ni sawa na kodi 🤣🤣🤣.
Kwa kifupi wewe baba uchumi wa nchi upo hovyo gharama ya maisha inapanda kila siku sijui mnataka yaje ya zimbabwe?