Kodi zetu ndio Maendeleo ya Taifa letu

Kodi zetu ndio Maendeleo ya Taifa letu

Kuna wakati mlituambia kuwa tuko UCHUMI WA KATI ila naona kwenye takwimu ulizoambatanisha hapo inaonekana kuwa UCHUMI WETU UMEPANDA KWA SASA UKILINGANISHA NA NYAKATI ZILE ZA UCHUMI WA KATI. Sasa swali langu ni Je,kama taifa letu limekua KIUCHUMI tumehama kutoka UCHUMI WAKATI,NA SASA tuko kwenye UCHUMI WA DARAJA GANI?
labda daraja la mfugale
 
Dr. Mwigulu Nchemba, mama Samia kuna mahala leo kagusia kuhusu mikopo na kubembelezwa kukop. Usifikiri haelewi jinsi unafaidika na wakopeshaji, analielewa sana lakini wa zamani tunasema "anakuweka deka".
Mipasho na taarabu hazijengi hebu tujuze zaidi?
Ipo haja ya kukopa yale anayoyafanya ruto, mashirika yote mzigo kwa serekali, iyaachie kwa kuyabeba, Itafute namna nyingine hata ya ubia na makampuni yenye uzoefu mkubwa!
 
kusanyeni kodi na mkope kwa wingi mwakani mnunue Rolls Royce za kutembelea,mapumziko kila weekend muende Dubai.
 
Hiyo kodi yako ndo inaealipa wenza wa viongozi,ndo inalipa wasanii kwenda nje kucheza makida,ndo inawapa viongozi kula maisha.
 
Daktari wa uchumi,hivi mnaona mnampunguzia au kumuongezea mzigo huyu mwananchi??

Hili swali,hebu toka nenda kamuulize hata mpita njia,alafu tafakari.

Nyie viongozi ni mzigo kwa taifa.
 
Nimesoma comments wameliuza watu maswali lakin hakuna majibu

This means huyo sijui mnamwita mh ni NOTHING..
 
Mipasho na taarabu hazijengi hebu tujuze zaidi?
Ipo haja ya kukopa yale anayoyafanya ruto, mashirika yote mzigo kwa serekali, iyaachie kwa kuyabeba, Itafute namna nyingine hata ya ubia na makampuni yenye uzoefu mkubwa!
Umeandika mada nne tofauti, jifunze kuandika mada moja moja.

1) Unataka wimbo upi wa taarabu na mipasho, hatuwachi utamaduni wetu kwa bolingo.

2) Usifananishe machungwa na mapera. Ruto ana deni asilimia 70 ya bajetu yake, Tanzania ina deni asilimia 35 tu na mama Samia kishasema waziwazi, sasa ni mikakati ya uzalishaji na uchapaji kazi tujitosheleze. Kukopa si kuzuri ni kujishushia hadhi.

3) Mashirika ya serikali yote yapo mbioni kufanywa ya umma, au hufahamu Kitila Mkumbo na Mchechu wanafanya kazi gani mpaka sasa?

4) Katika Reforms za Rais mama Samia hafanyi kutafuta ubia na makampuni ya nje, hilo lilishafanywa na mwendazake, rejea Twiga Corp.

Reforms wanazoshughulikia Mkumbo na Mchechu sasa hivi ni kuwafanya wananchi wa Tanzania ndiyo wawe wabia, ndicho kinachofanyika hivi sasa. Hiyo ni kuyatowa mshirika kutoka kuwa ya Serikali kuelekea kuwa ya umma kiukweli. Siyo ya umma kinyerere.
 
Binafsi siamini kama ATCL inaendeshwa kwa faida,na mengi tu.
 
Kodi zetu ndio Maendeleo ya Taifa letu.

Mwaka 2021/22- Trillions 22.2.
Mwaka 2022/23- Trillions 24.1.
Mwaka 2023/24- Trillions 27.6

====
Pia soma:
Hivi, hizo kodi mbona zinatumika kununua magari ya anasa? Naomba, nikushauri ndugu yangu ili umashauri Mama Samia. Kwann wakuu wa, mikoa, wilaya na wakurugenzi wasingenunuliwa gari aina ya Kruger ya shs million 25 , kila mmoja, kuliko kuharibu na kupoteza pesa, za serikali na kununua magari ya, shs million 300:

Kama, tungefanya hivyo tungeweza kuweka lami kila kijiji. Lakin, mnatukatisha tamaa kabisa kwa mnachofanya. Lakin ipo siku history itawahukumu kwa uharibifu wa pesa za, serikali .
 
@Dr Mwigulu Nchemba..huu utajiri wa haraka haraka umeutoa wapi?
 
Mwigulu umeandika mada hii ili watu wachangie. Binafsi nimekuwa nikitamani kupata fursa ya kukupa ujumbe wangu.

Nalipa kodi kupitia ajira na biashara ninazofanya.. Maumivi ya kodi ni makubwa mno!. Maumivu haya yanazidi pale unapokuwa na waziri wa fedha mwenye tabia kama zako. Hivi, utaacha lini huo ulafi? Inawezekanaje waziri kama wewe kuona ni sahihi kununua gari la serikali lenye thamani kibwa mno kama unalotumia huku kuna shule hazina madawati? Hupaswi kuwa mfano bora wa uadilifu na kubana matumizi ili wizara zingine ziige?

Hivi ile misafara unayofanya ya msururu wa magari yenye thamani kubwa mav8 huwa ina umuhimu gani kwa wananchi? Misafara ya magari ndani mmebeba kibegi kidogo chenye bajeti ya serikali! Kwa namna nyingine unatuhimiza kulipa kodi ili wewe na walafi wengine wasioridhika muendelee kuonyesha ufahari na jinsi gani tabia zeni halisi zilivyo. Hivi , ukitumia gari yenye thamani ndogo ya kawaida ukubwa wa cheo chako utapungua? Seriously, gari ya afisa kama wewe ni milioni mia sita? Au nusu tririoni? Hapo ndio moyo wako unaridhika? Hiyo pesa ingeweza kununua madawati mangapi? Hata kama thamani ingekuwa milioni mia nne, au mia tano, moyo wako ndio utaridhika? Ni watoto wangapi wa walipa kodi wanasona katika mazingira magumu, hakuna choo, madawati, vitabu vya kugombania , huku wewe unaendeshwa kwenye gari ya thamani ya nusu tririoni. Huo ndio ubinadamu?

Je una uhakika unahimiza watu kulipa kodi ili zitumike kwenye maendeleo ya taifa, au zitumike kuneemesha nafsi zenu wewe na walafi wengine? Jf mtanisamehe, lakini, tabia binafsi za viongozi wetu, hasa waziri Mwiguru zinatia hasira na zinaleta mashaka makubwa hasa kuhusu mustakabali wa taifa letu.
 
Inawezekana kabisa mnafanya kazi nzuri sana ya kukusanya kodi,swala ni jinsi gani mnapambana na ufisadi ambapo hiki mnachokusanya kuna wachache wanakwapua kwa manufaa binafsi,onyesheni wananchi kuwa kuna hatua zinachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha,hili mkiliweza mtarudisha matumaini kwa wananchi kuwa kodi zao zinafanya kazi...
 
Back
Top Bottom