Hawezi kuja kujibu Kila mtu hapa ila Mimi naweza kujibu Baadhi ya sababu .
1.Mama amefungua Nchi,ishu ya kwanza kabisa ilikuwa kurejesha Imani ya wawekezaji na wafanyabiashara Kwa Serikali na mnakumbuka hatua mbalimbali zilifanyika ikiwemo ziara za Nje,kurudisha pesa za walioporwa na kuacha kutumia task force au kufungua accounts.Waliofungiwa accounts Kwa Sasa ni wale wanaodaiwa.
2.Utalii.Ishu ya Royal tour imeirejesha Tzn kwenye ramani ya Utalii,ni sekta imefanya vizuri Sana na kuweka rekodi kubwa kuwahi tokea.
3.Sekya ya Madini.Sekta ya Madini imekua sana awamu hii ya sita Kwa sababu ya uratibu mzuri,udhibiti na kuwajali wawekezaji wadogo na wakubwa.Mfano wawekezaji wadogo wamepewa Mitaji,umeme na mitambo Baadhi ya maeneo.
4.Sekta ya Ujenzi,viwanda na Uchukuzi imeimarika sana awamu ya 6.
5.Kekta ya Kilimo.Licha ya kwamba Bado inachangia kiwango ambacho sio kikubwa sana ila imechangia zaidi ya hapo awali.
Mazao kama ufuta,avocado,mazao ya nafaka na ya biashara hasa tumbaku yameleta pesa nyingi sana Nchini Kwa sababu ya sera na uwekezaji wa Serikali kwenye kilomo.Kumbuka mama ameweka pesa mara dufu kwenye Kilimo.
Kwa maoni yangu nilivyofuatilia nimebaini sekta hizo ndio maana mabenki na bima wamepata mabilioni Kwa mabilioni ya faida kushinda wakati mwingine wowote.