Kodi zetu ndio Maendeleo ya Taifa letu

Kodi zetu ndio Maendeleo ya Taifa letu

Jipangeni Gen Z wa Kenya tumeshawakodi... Muda wowote wako na nyie ..... Tena km we?
 
Hizo kodi mnazokusanya kila mwaka na kujisifu mmevunja rekodi huwa mnapeleka wapi?

Lini majizi yaliyotajwa kwenye ripoti ya CAG mnayashughulikia?
 
Kuna tatizo kubwa sana katika uongozi wenu.. Hivi sasa mnatuaminisha kuwa kodi zetu ndio zitaleta maendeleo.. Vipi kuhusu rasilimali za nchi..?? Madini, bandari, Utalii, bidhaa za kilimo na ufugaji nk. Zinachangia kiasi Gani katika mapato ya Taifa..??

Mnaposema Kodi zetu, mmetuwekea mazingira rafiki ya biashara endelevu ili makusanyo ya Kodi nayo yawe endelevu au ndio mnatukamua mpaka tunafunga biashara..??

Vipi kuhusu ubadhirifu..?? Je Kodi inayokusanywa inaenda kwenye maeneo sahihi ya miradi ya maendeleo au Kodi hiyo inagharamia maisha yenu ya anasa na kujaza mifuko yenu isiyotosheka..??

Ifike mahali mjitafakari hali huku chini ni ngumu kwa sababu ya ulafi wenu.. Hela Haina thamani na imekuwa ngumu kupatikana.. Tikiti Moja pale Goba linauzwa 10,000/- Wewe kama waziri wa Fedha unajiskiaje kuona noti kubwa kuliko zote katika nchi yako inanunua tunda moja..??
 
hawezi kuwajibu hata msijisumbue kumuuliza
 
Mimi ni CCM damu damu, lakini sihawahi kumuelewa huyu waziri wa fedha wa sasa.

Hana ile cream ya kuwa na wadhifa mkubwa namna hiyo, si kwa kuongea kwake, kuvaa kwake na wala utendaji wake.

Naamini huyu ndio chanzo kikuu cha matatizo ya wafanya biashara na mengineyo mengi kuhusu mifumo ya kifedha serikalini.
Kwa ufupi. Dr. Mwigulu Nchemba ni bogus.

Watu kama huyu ndiyo wanasababisha machafuko.
 
Mh Waziri Mwigulu , ahsante kufika hapa ili usikie huku ''site' kuna hasira kiasi gani

1. Takwimu ulizotoa hazikuzingatia vigezo vingi. Moja, kama alivyosema mchangiaji mmoja idadi ya walipa kodi ikoje? Pili, ongezeko la Trilioni linaendana na thamani ya dollar!

2. Kodi ni sehemu tu ya mapato ya Taifa lakini si eneo pekee. Tunataka mchanganuo wa kila sekta halafu tupime kama tumeongeza pato au la. Ukumbuke pia 'population' ina umuhimu kuzingatia

3. Wananchi wanahasira za matumizi ya anasa. Kwanini RC anatembelea CVR lakini akiteuliwa lazima apewe V8. Mnapojinunulia V8 500 kwa milioni 400@ ni ghali sana kuliko kumlipa kiongozi huyo transport allowance ya milioni 10 kwa mwezi. kumbuka V8 ina dereva , service na maintanance kwa mwaka ni mabilioni yakwenda Japan. Kwanini serikali masikini inalea viongozi kuliko nchi kama Uingereza , USA, Ujerumani n.k.

4. Serikali ni kubwa. Kuna taasisi zisizo na kazi zinazoweza kuunganishwa .
Wizara ni nyingi bila sababu za msingi. Kuna uwezekano wa kuwa na serikali ndogo kubana matumizi

Wizara 'X' ina Waziri, manaibu 2, Katibu mkuu, naibu katibu mkuu na Wakurugezi wa idara! hawa wote wanafanya kazi gani?

5. Taasisi kama Bunge hatujui bajeti yake, tunajiuliza kwanini Mbunge alipwe lakini 2 kukaa katika kiti cha kazini?Kwanini apewe nyumba Dodoma halafu alipwa per diem, lita za mafuta kila wiki hata akienda kwa kimada wake!

Matumizi ya taasisi kama Bunge yanatia hasira walipa kodi. Tuonyeshe Bajeti ya Bunge

6. Makusanyo ya kodi yanalenga Watumishi wa Umma zaidi na huduma kama vileo.

Kodi inayotokana na ongezeko la ''LUKU' ni ndogo sana ukilinganisha na Trilioni iliyopotea kwa mujibu wa CAG na ninyi hamchukui hatua kwasababu mpo katika '' inner circle''

7. Wafanyabiashara wa Kariakoo wanawakilisha hasira za wateja wao.
Kodi za Kariakoo halafu zinakwenda kununua V8 , sherehe za serikali , matumizi ya anasa ya viongozi na wizi unaofanywa na viongozi. Wafanyabishara wa Kariakoo wanawapa 'hint' ya hasira walizo nazo wananchi.

Mnaweza kuziba masikio ili mfike juu kama yule chura! Rais Ruto amejaribu kuwa chura kiziwi , maji shingoni.
 
Umejitahidi kujibu swali la kwanza Mkuu, japo hujawasilisha jibu la swali la pili.

Kwamba pamoja na makusanyo hayo makubwa ya Kodi, kwanini tunaendelea kukopa?
Gari namba E, ni nyingi mno, ubnormally kapu la umma linavuja pahala, sio bure, lakini wapi? Yapo maswali waziri hatoweza kuyajibu Isipokuwa ni mh. rais pekee!
 
Mimi ni CCM damu damu, lakini sihawahi kumuelewa huyu waziri wa fedha wa sasa.

Hana ile cream ya kuwa na wadhifa mkubwa namna hiyo, si kwa kuongea kwake, kuvaa kwake na wala utendaji wake.

Naamini huyu ndio chanzo kikuu cha matatizo ya wafanya biashara na mengineyo mengi kuhusu mifumo ya kifedha serikalini.
Kwa ufupi. Dr. Mwigulu Nchemba ni bogus.

Watu kama huyu ndiyo wanasababisha machafuko.
Bi mkubwa kweli umechafukwa moyoni, tumsaidie waziri wetu, kwani ni mwanadamu na mwanadamu huwa na mapungufu, tuonyeshe njia ya kwenda au afanyaje?, #tunasubiria maoni yako!
 
Bi mkubwa kweli umechafukwa moyoni, tumsaidie waziri wetu, kwani ni mwanadamu na mwanadamu huwa na mapungufu, tuonyeshe njia ya kwenda au afanyaje?, #tunasubiria maoni yako!
Tumemuonyesha sana lakini kiburi chake anajifanya haoni wala hasikii.

Ingawa 'dua ya kuku haimpati mwewe" lakini naamini huyo ana mwisho mbaya sana.

Ingawa mama Samia alimtetea sana kwa madudu yake lakini asifikiri mama Samia hamuelewi. Mama Samia ni mstahamilivu sana na amempa muda ajirekebishe, ustahamilivu una kikomo chake.

Ikiwa ni mwenye uelewa atanielewa nasema nini.
 
Dr. Mwigulu Nchemba, mama Samia kuna mahala leo kagusia kuhusu mikopo na kubembelezwa kukop. Usifikiri haelewi jinsi unafaidika na wakopeshaji, analielewa sana lakini wa zamani tunasema "anakuweka deka".
 
Gari namba E, ni nyingi mno, ubnormally kapu la umma linavuja pahala, sio bure, lakini wapi? Yapo maswali waziri hatoweza kuyajibu Isipokuwa ni mh. rais pekee!
Yeye ndiye mshauri Mkuu wa Mama kukopa, kwahiyo ni lazima atoe majibu ni kwanini Nchi inaongozwa Kwa kukopa?

Haiwezekani wakati JPM anafariki Deni la Taifa liwe 61T Leo hii miezi 39 baada ya Kifo chake Deni la Taifa liwe 92T

Yaani ni wastani wa kukopa Trillion 10 kila Mwaka 🙌

Huyu Waziri hajaweza kuvivaa viatu vyake sawasawa
 
Siyo tu dhamana , je inatumikaje?
wasanii watasafirishwa na nn viongozi watanunuliwa magari mapya na nini mkuu nchi inamatumizi makubwa kwahiyo hata wakikopa tunabaki kulipa deni ila maendeleo ziro ndio yale manyanyaso anayosema kiziwi frog
 
Thamani ya shilling imeporomoka kwa kasi sana . Una mpango wa kumshauri nini rais ili thamani ya fedha yetu isiporomoke zaidi ? Au akili yako imeishia kwenye tozo , kuwakamua watanzania tu na hauna ubunifu wa kuinusuru thamani ya fedha yetu .
hivi unatarajia atakujibu hahahaha mkuu pale tuna lizuzu letu linaongoza wizara basi tu ila mweupe sana kichwani
 
Back
Top Bottom