Kodtec Speaker systems

jamaa analeta mambo ya wasafi festival sebuleni sio[emoji16][emoji16]
Soundstage and Imaging ni vitu VERY BASIC kwenye 2 channel audio. Na any True 2-channel-system inatakiwa ikupe hivyo vitu.

Tatizo ni kwamba hujawahi kuiexperience Hi-End audio inayoweza kukupa hivyo vitu nilivyoelezea.
Mimi nime-experience na ninayo hapa kwangu so ninazungumza kitu ninachokijua.

Tatizo letu wabongo huwa hatupendi kujifunza kitu kipya na kukubali kuwa tulichonacho kwa sasa bado hakijafika levels fulani. (Hapa sijisifii, I'm humbly trying to make my point)

Yaani mtu mwenye infinix hataki kukubali kuwa kuna vitu anavikosa compared na mtu mwenye Samsung S23.
 
We sound stage hio utaipata kwenye live band. Mziki ulioko recorded studio lazma usikie kwenye speaker.

Mziki wa live recording ndio utaimba hivyo unavyotaka wewe.
Mkuu, unachosema sio kweli.

Mziki uliokuwa recorded studio unaopigwa kwenye a TRUE 2 CHANNEL SYSTEM huwezi kuusikia directly kutoka kwenye Speakers. Kwa sababu system ya aina hiyo imetengenezwa kukupa UHALISIA wa mziki na sauti inapopaswa kusikika.

Tatizo ni kwamba Hujawahi kusikia system ya aina hiyo.

Note: Hapa nazungumzia A TRUE 2 CHANNEL SYSTEM...sizungumzii hii mi hiFi ya sony na lg ya laki saba.

Na ndiyo tafsiri halisi ya IMAGING. Speakers zinapaswa zikupe uhalisia wa stage.
Unasikia sauti kutoka sehemu halisi inapotakiwa kusikika...sio directly kutoka kwenye Speakers... na hapa ninazungumzia MZIKI ULIOKUWA RECORDED STUDIO.

Mkuu, I know what I'm talking about... siongei-ongei tu.
 
Hio system we unayo nije niskilize tru hi fi sounds?
 
Hio system we unayo nije niskilize tru hi fi sounds?
Kwa Mimi am sure kuwa kwenye requirements zote kuanzia subs, amplifaya, mixer na equalizer, mids na tweeter.
"Ukiongeza crossover, epicenter (DSP) audio music enhencer yaani dynamic sound processor, midi nne na tweeter nne . Unapata zaidi ya unachoongelea mkuu .
Ila tafuta bei ya hio epicenter (DSP) utanyoosha mikono yote juu,
Hapa nakukubalia saana Kwa point Yako broh
 
Kenya hpo kuna kila kitu cha audio

sema bei bdo sio rafiki mzee
 
true 2 channel unazipata kwenye monitor speakers,kama hizi za studio, ila jua keamba kila mziki una ladha yake,na sikio la kila mtu hutofautina
 
true 2 channel unazipata kwenye monitor speakers,kama hizi za studio, ila jua keamba kila mziki una ladha yake,na sikio la kila mtu hutofautina
Ni kweli kuna speakers specifically kwa ajili ya studio. Hizi huwa zinakuwa neutral with no color to the sound.. na ni mahususi kwa ajili ya kutengenezea mziki studio.

Ila si kweli kuwa True 2 channel music inapatikana kwenye studio monitors peke yake.

True 2 channel audio inapatikana pia kwenye speakers za kawaida za sisi wasikilizaji/watumiaji. From bookshelves to floor-standers.

Hapa ikumbukwe nazungumzia speakers za kweli za brand zinazoeleweka kwenye ulimwengu wa audio...sio hizi speakers za lg na sony na subwoofers za mchina.
 
Pamoja sana mkuu, nipe picha tu nijiridhishe
Okay here we go....

Naitambulisha kwenu The Fives from Klipsch.
A true HiFi System, designed for music.

Brand: Klipsch
Model: The Fives

INTRO:
Ni powered Speakers. Maana yake iko na in-built amp.. Na ina inputs connections almost zote

SOUND:
- It has a very BIG Sound.. They sound very BIG.

- Zile sifa za Soundstage and Imaging nilizozungumza kwenye comment iliyopita, unazipata hapa.

-Zinapopiga mziki, zina-dissappear. You just hear Music but You don't hear music directly from the speakers.
Zinakupa UHALISIA wa mziki in terms of sauti/instrument inatakiwa isikike kutoka wapi.

- Kwa upande wa Bass, zina Bass ya kutosha sana. Ila una option ya kuongeza sub kama utataka. (Honestly sijawahi kuhitaji kuongeza sub...The Bass here is more than Enough for me)

MY OPINION:
Kwa kifupi... Zina sound vizuri sana... I mean SANA.
Ni speakers zilizonipa Taste na experience mpya ya mziki ambayo sikuwahi kuipata popote hapo kabla.

Binafsi Naamini mtu akionja hii ladha, ni ngumu sana kurudi kwenye homethearters/soundbars na subwoofers.

Naambatanisha na Picha kama ulivyoomba.
 
hii system ulishwahi ituma humu ila sikumbuki ni uzi gani.
 
Uko wapi nije niskilize hio soundstage
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…