Mziki wa ukweli tunaupima kwa kitu gani mkuu?
Watu wengi huwa wanaamini mziki bora ni mziki kuwa na Bass ya kufa mtu.
Mziki ni ZAIDI YA HAPO.
Kuna vitu kama hivi hapa (nataja vichache)[emoji116]
- Soundstage
- Imaging
- Speakers kuwa na uwezo wa ku-dissappear.
Swali langu ni kwamba, Hizi system zetu tunazoongelea hapa zinatupa hayo mambo?
1. Tukisikiliza mziki, huwa tuna feel a realistic soundstage mbele yetu?
2. Je tunaweza kupoint-out vyombo vya mziki vikiimba? Mfano, unaweza kupoint out kinanda kipo wapi, gitaa lipo wapi etc? (IMAGING)
3. Unaposikiliza mziki, huwa Unamsikia Mwimbaji kutokea Katikati ya stage? Na waimbaji wengine unawasikia around her/him? Huwa tunapata huu UHALISIA ambao ndio upo in real life?
Au huwa tunasikia wanaimba kutokea kwenye Speakers?
4. Ukisikiliza mziki, hutakiwi kuzisikia speakers. Speakers SHOULD DISSAPPEAR COMPLETELY. Unatakiwa kusikia mziki kutokea mahali unapotakiwa kusikika (refering point no 2 on Imaging) lakini hutakiwi kuzisikia speakers zikitoa sauti.
Je, Hizi miziki zetu za budget(za jamii ya kina kodtec) huwa zinatupa hizi experience?