Koffi Olomide ahukumiwa miezi 18 jela kwa kosa la kumshambulia Dansa wake

Koffi Olomide ahukumiwa miezi 18 jela kwa kosa la kumshambulia Dansa wake

Mwanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) Koffi Olomide leo amehukumiwa kifungo cha jela miezi 18 kwa kosa la kumshambulia moja wa madansa wake jijini Nairobi juzi.

Mahakama moja mjini Kinshasa imetoa hukumu hiyo leo muda mfupi baada ya mwanamuziki huyo kukamatwa wakati akiwa nyumbani wake.

Alipangiwa kutumbuiza mashabiki wake Bomas of Kenya Jumamosi lakini tamasha hiyo ikaahirishwa.

Olomide alikamatwa Ijumaa usiku na maofisa wa polisi wa Kenya na siku iliyofuata asubuhi akaingizwa kwenye ndege na kurejeshwa Kinshasa.

Katika hatua nyingine, waandalizi wa tamasha ambalo Olomide alipangiwa kutumbuiza nchini Zambia pia walitangaza kufuta hafla hiyo kutokana na yaliyotokea Nairobi.

Mwanamuziki huyo, akiandika kwenye ukurasa wake wa Facebook Jumapili, aliomba radhi mashabiki wake na hasa “wanawake na watoto”.

“Najutia sana yaliyotokea… kilikuwa ni kipindi kifupi cha wenda wazimu,” aliambia kituo cha televisheni cha taifa cha RTNC.

Baadaye, aliomba msamaha kutoka kwa raia wote wa DRC ambao huenda alihisi kwamba tabia yake iliwavunjia heshima.

Waziri wa masuala ya vijana na jinsia Kenya, Sicily Kariuki katika taarifa kwa vyombo vya habari baada ya video iliyoonyesha tukio hilo kusambaa, alipendekeza Olomide azuiwe daima kutembelea Kenya.
 
Siku ile nilisema anandamwa na msimu wa yule mzee alie fiya jukwani kwani walikuwa madui wakubwa sana, acha afundishwe adabu alidhani pesa yake itamsaidia kumbe heshima ni bora kuliko pesa
 
Iwe fundisho kwa wengine wanaowashambulia wake zao, iwe faragha au hadharani.
 
Bado sijaamini hizi habari, labda waandishi wa hili gazeti ndio wale wale. Inakuwaje akamatwe jana leo tu afungwe?
Kinachocheleweshaga kesi nyingi ni ukosefu wa ushahidi ambao kwa kesi hii ushahidi uko wazi...
 
Jamaa ana mkosi kajichafulia balaa ufaransa anatafutwa kenya katimuliwa kwao kimenuka aisee uzee wa kikongo mbaya inaelekea jamaa mwanamke kwake sio kitu muhimu akome aisee mbwembwe zote za ekotite akazifanyie kolokoloni
 
Huko Naona hawacheleweshi, kesi mahakamani na hukumu hapo hapo?.
 
MASIKINI KAKA KOFFI OLOMIDE ANAKWENDA JELA ..............

Kofi.jpg
 
Na huyu Cindy wake anaempa wazimu atakuwa anatafunwa na wengine, haahaa mwanaume unaingilia ugomvi wa wanawake kisa umfurahishe mupenzi acha aonje maisha ya miezi 18 bila demu pembeni yake.
 
Hakuna hata kesi mahakamani?

Ni kutoa amri tu...kamata funga huyo?

Only in Africa!
Mkuu acha tu afungwe amejisahau sana.Huwezi kufanya kitu kama hicho tena in public....no way ngoja anyoooke
 
Back
Top Bottom