Kofi la mkunga kwa mama mjamzito limebeba ujumbe mzito; Wakunga wana mema mengi ya kusimulia

Kofi la mkunga kwa mama mjamzito limebeba ujumbe mzito; Wakunga wana mema mengi ya kusimulia

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Hata mimi hapo zamani nilikuwa nawasema vibaya sana wakunga!

Ikanibidi nifanye utafiti; je lawama zile kwa wakunga zinawastahili!?

Katika chunguza chunguza niliweza kufika kwenye hospitali moja kama mme wa mzazi mmoja aliyekuwa leba kusubili kujifungua!

Nilifanikiwa kuwa karibu sana na mkunga kiasi kwamba nilishuhudia mambo magumu sana wakunga wanayokutana nayo!

Hebu fikiria mkunga mmoja anategemewa kuzalisha wanawake karibu 20 au zaidi!

Ndani kundi hilo la wajawazito!

Kila mjamzito aliyeleba anastyle mbalimbali ya kuugulia uchungu wake!
  • Kuna wale wajawazito mimba zao za kwanza wasioelewa hata kupush
  • Kuna wapo wajawazito wanaopush na kujamba pamoja
  • Kuna wale wajawazito wanaopayuka na kutukana hovyohovyo wodini
  • Kuna wale wanaowatukana waume zao kwa kuwataja majina wakiwa leba,...mfano utasikia; wee Mudy ulini.......mba ukanipa mimba, sahivi uko huko unakula raha na mahawala wengine, wee muddy Malaya mkubwa!...oooh Muddy wee mwanaume hufai kabisa, ona ninavyotaabika....etc
  • Wapo wanaoingia uvunguni mwa kitanda wanapomuona mkunga kaingia!
  • Wapo wanaobana mapaja kiasi cha kuhatarisha maisha ya mtoto na ni wabishi wanapoelekezwa
  • Wapo wanasikilizia maumivu ya maji ya uchungu kiasi cha kusahau maelekezo ya mkunga!
  • Wapo wajawazito wanadiliki kutukana hadi wakunga n.k
Hebu fikiria kufanya kazi katika mazingira magumu kama hayo!

Jamii imekuwa ya lawama sana kiasi cha kukumbatia matukio yanayoonekana mtandaoni!

Mtakumbuka Askari zimamoto kule Kigoma alivyopongezwa na kupewa promotion kwa kuokoa mtoto kutoka kwenye shimo la choo!.

Askari ambaye kila siku anafanya mazoezi ya kushuka au kupanda na kamba, hivyo kuokoa ni wajibu wa kazi yake kama kazi zingine!

Hatukatai kuwapongeza, lakini nachotaka kusema hapa, ni vile jamii inamuona shujaa ni huyo askari anaeshuka na kamba kuopoa mtoto shimoni, lakini jamii ileile inamsimanga mkunga aliyeopoa kichanga kutoka tumboni!

ikumbukwe kosa moja tu la mkunga linasababisha kumkosa mama na mtoto au kupata mtoto kilema!

Sasa katika mazingira magumu ya kazi mkunga akipitiwa kidogo tu kumuweka sawa mama mjamzito inakuwa story!

Kwanini hatuwapi promotion WATU kama hawa? Kwanini hatuweki hata dodoso la siri kwa kila mjamzito anaejifungua ajaze max na jina la mkunga anaeona huduma yake ni nzuri hata tukawapongeza watu hawa?
Ebu fikiria mtu kutwa anagusa sehemu za siri tupu za kila aina!

Ebu vaeni uhusika wa ukunga japo siku moja, halafu mlipwe kwa LAWAMA muone mtajisikiaje!

Kama hatuwezi kuwapunguzia Msongamano Wakunga mahospitalini basi tuwape japo faraja na maneno ya shukrani!

ingekuwa Amri yangu! Wakunga wote ningewapa Special Allowance kila mwezi!
 
Acha kutetea Udhalimu na Upuuuzi wa huyo asiye na Utu wala haiba ya Ukunga. Kazi pekee anayoweza kupewa na DED ni kuwa Mgambo wa Halmashauri akakusanye ushuru huko Ziwa Rukwa lkn kamwe msianze kuleta Utetezi kwa huyu kilaza mwenzenu.

Hizi kada za Afya na Elimu kukosa kufanyiwa Interview na Vetting za mara kwa mara zimejikuta zimekusanya mijitu Hopeless kabisa
 
Vp mkunga akikutana na mwanamke anayetaka kujifungua lkn mkunga amegundua mmjamzito huyo alikuwa analiwa jicho....
Mkunga si atamzabua sana vibao
Ndizo changamoto wanazokutana nazo! Lakini nahisi wanawake wengi wa hivyo huwahi kuomba operation kwa visingizio mbalimbali
 
Acha kutetea Udhalimu na Upuuuzi wa huyo asiye na Utu wala haiba ya Ukunga. Kazi pekee anayoweza kupewa na DED ni kuwa Mgambo wa Halmashauri akakusanye ushuru huko Ziwa Rukwa lkn kamwe msianze kuleta Utetezi kwa huyu kilaza mwenzenu...
Lakini mema yao ni mengi kuliko mabaya yao! Mimi na wewe hatujui alifanya hivyo katika mazingira gani!
Kumbuka wakunga ni binadam siyo malaika mkuu!

Usiichukulie kada kama wahusika ni malaika!
 
Acha kutetea Udhalimu na Upuuuzi wa huyo asiye na Utu wala haiba ya Ukunga. Kazi pekee anayoweza kupewa na DED ni kuwa Mgambo wa Halmashauri akakusanye ushuru huko Ziwa Rukwa lkn kamwe msianze kuleta Utetezi kwa huyu kilaza mwenzenu...
Ni kweli Idara ya Afya ina watumishi wa ajabu sana; na ushahidi ni uone mama Dorothy anavyoteseka sasa hivi kuzisimamia hospitali. Yaani kuanzia RMOs hadi chini kwenye dispensaries; ... hamna kitu!
 
Hata Mimi hapo zamani nilikuwa nawasema vibaya sana wakunga!

Ikanibidi nifanye utafiti; je lawama zile kwa wakunga Zinawastahili!?....
Mkuu naunga mkono hoja, waziri kakurupuka.
 
Hata Mimi hapo zamani nilikuwa nawasema vibaya sana wakunga!

Ikanibidi nifanye utafiti; je lawama zile kwa wakunga Zinawastahili!?...
Umesikiliza vizuri hii habari au umekurupuka? Kwa vile mkeo kakuletea mtoto tulia ulee mwanao usituletee ngojera hapa.
 
Inawezekana mkuu ila tunglie na mazingira.
Naomba fuatilia hii habari Kwa uzuri, mzazi kamwita hakuja, kashuka kitandani na kujifungulia chini bila ya msaada wa mkunga hadi hapo mzazi anakosa gani afikie kuadhibiwa, kuzaa ni mtihani kufa au kupona
 
Naomba fuatilia hii habari Kwa uzuri, mzazi kamwita hakuja, kashuka kitandani na kujifungulia chini bila ya msaada wa mkunga hadi hapo mzazi anakosa gani afikie kuadhibiwa, kuzaa ni mtihani kufa au kupona
Pande mbili mkuu.
 
Hata Mimi hapo zamani nilikuwa nawasema vibaya sana wakunga!

Ikanibidi nifanye utafiti; je lawama zile kwa wakunga Zinawastahili!?...
Ndo shida ya kuitwa Mudi .........angeitwa Mo sidhani kama angepewa hayo matusi
 
Ukunga sio kazi ya lelemama wala kazi ya kufanya kisa tu iko na maslahi mazuri, utaumia wewe na wagonjwa wako!

Uchungu wa kujifungua hauna bingwa, sio mkunga wala mzalishwaji.

Hekima, busara, uvumilivu na UTU ndio guidelines za labour kwa mhudumu na mhudumiwaji japo mara nyingi sana sana mhudumiwaji anakua taken over na uchungu ambapo kibinaadam, anahama dunia kwa muda kiasi kwamba hizo guidelines hazina maana kwake, hata kidogo!

Mwanamke anapoingia labor ward, ni sawa na mwanajeshi anaeingia vitani, hapo ni kufa ama kupona na kazi kubwa ya mkunga ni KUSAIDIA na Kuhakikisha mama na mtoto wanapona ama angalau mmoja kati yao!

Mfano wako wa askari mwokozi sidhani kama unaendana na umuhimu wa mkunga na thamani yake.

Nawaheshimu wakunga wote wanaotambua wajibu wao na kuukubali bila chembe ya kinyongo, Muumba awabariki sana!

Tatizo kuna baadhi yao (hasa wadada wa makamo ya kati) ni wakorofi sana, nadhani Kinyaa na Nyongo hawakutemeshwa vizuri, hawajakomaa! Ama wapo kwa sababu fani hiyo inalipa!?
 
Unamaanisha Mudy huyuhuyu wa simba ndo kamtia mimba huyo mwanamke wa leba mkuu!!!![emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom