Na hayo matamshi wanayo wengi, pale Makole maabara kuna namba ya simu mlangoni wengi hawajui Ile namba ni ya Nani, ukifika maabara unaweza usimkute mtu pale ndani nasemea wakati wa usiku kumbe labda yupo anawajibika huko ndani au ametoka unakaa kumsubiri haji Kwa vile kuna namba mlango unaamua kupiga [emoji15] kosa umempigia boss naye anamtafuta. Hapo sasa umelianzisha cha kwanza atakuuliza Kwa nini usimuulize mlinzi hapo getini, unataka kuniharibia kazi, sasa kuna huyu mama ananongwa kila akikuona lazima akumbushie namwambia hivi ipo siku nitamrekodi halafu namuonyesho huyo boss wake na hanioni tena Makole, Bora angekuwa ndani lakini katokea maeneo ya getini, hospital zipo nyingi.