Sio kila special force ni komandoo.
Special force ni watu maalumu waliobobea katika jambo flani, ambapo wao ndio huhitajika kwa ajili ya kukabiliana na tukio lolote linalohusiana na eneo ambalo wao ni wataalamu.
Kwa mfano FFU ni special force kwa polisi kazi yao ni kutuliza ghasia( Field Force Unit).
Magereza wana special force( wanaita special task force au kikosi maalumu cha kutuliza ghasia magerezani-KMKGM).
Jwtz ndio kuna Komandoo ambao ni special task force kwa ajili ya vita nchi mbali mbali (wanaenda missions pia), kwa ufupi komandoo ndio wanajeshi waliopitia mafunzo ya hali ya juu zaidi kuzidi wanajeshi wa kawaida, nao pia wamegawanyika kuna waliojikita katika ukomandoo wa majini(Navy), kuna ambao ni ni wataalamu wa angani na pia kuna wataalamu wa vita ya ardhini lakini wote ni komandoo, kiufupi wao ndio hujifunza karibia kila kitu kuhusu vita na defence.
Kwa sababu ya kuwepo kwa viwango tofauti tofauti vya elimu kuna komandoo ni askari wa kawaida(private mpaka warranty officers) pia kuna maafisa ni komandoo(Luteni usu mpaka Luteni General au hata General kabisa)
Kama hujaelewa uliza mkuu