Komandoo wa Tanzania wana kazi gani?

Komandoo wa Tanzania wana kazi gani?

inawezekana wwmewekwa kwa matumizi ya baaadae! ili wasije tumika wakaisha!....ila tukiangalia kwa undani hakuna haja ya kusema kuna makomandoo huku wakijionyesha siku za skukuu za kitaifa huku wakishindwa kushughulika na matatizo katika jamii yetu/yao!
 
Kwanza kabla hujataka komando washirikishwe ktk majukumu hayo inabidi utambue kua Komando ni mwanajeshi na anawajibika moja kwa moja ktk shughuli za kijeshi kwanza.

MAJUKUMU YA JWTZ
Majukumu ya Jwtz yamegawanyika ktk nyakati kuu mbili,

1.Wakati wa vita
2.Wakati wa amani

Hapa tuangalie zaidi majukumu wakati wa amani.
1.Ulinzi wa mipaka ya nchi dhidi ya maadui.

2.Kujiandaa kwa majukumu ya vita(watafanya mafunzo na mazoezi)

3.Kusaidia mamlaka zingine za kiraia na kushirikiana na vyombo vingine vya usalama ktk majanga mbalimbali kama ajali,mafuriko,migomo,na kutuliza ghasia kubwa.

Nb-kumbuka ushiriki wowote wa jeshi ktk shughuli kama kudhibiti ujambazi,ujangili lazima agizo litoke kwa Amiri Jeshi mkuu.
Pia wenyewe jeshini wana kanuni yao wanaiita "USE OF MINIMUM FORCE"

Si jambo la busara kuwatumia makomando wetu waliofuzu vizuri kimafunzo kukimbizana wezi wa kuku vichochoroni.

Majukumu yao yapo,kumbuka Drc,Comoro komando wetu wametuwakisha vyema kabisa.

Mwenzio Jkt kwa mujibu imenifumbua macho najua walau kidogo kuhusu majukumu ya majeshi yetu.
 
Ile ndege iliyopakia Twiga wakiwa hai pale KIA inasemekana ilikuwa ni ndege ya jeshi la Qatar pia ile meli iliyokamatwa kule Zanzibar na meno ya tembo hivi karibuni inasemekana ilikuwa ni meli ya jeshi la China.

Inasemekana na wizi wa kwenye ma-benki hupangwa na kutekelezwa na polisi wenyewe!
 
mkuu ufahamu wangu unanituma kukujibu kuwa level hiyo ya ujambazi ni jukumu la polisi, makomandoo wanaingia kwenye issue kubwa ambazo madhara yake ni makubwa na yanahitaji nguvu kubwa na ya haraka kuyakabili, mfano ni ule uvamizi wa kigaidi kule kenya , hapo makomando wanaweza tumika , lakini ujambazi wa kawaida ni jukumu la polisi..
 
Macomandoo kwanini wasitumike hata mle benki kuu kuzuia wizi kama wa Epa?au TRA kuzuia mambo ya ufisadi.
 
Huwezi kutumia volvo vnl 680 kwendea ofisini, church,beach,sokoni etc.
 
Mleta mada, kwanza naamini unalipenda na kuliheshimu Jeshi letu la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Hili ni Jeshi la kupigiwa mfano, ukiacha zile dosari ndogo ndogo za hapa na pale; tena zinazofanywa na wachache.

Huwezi kujua kazi ya Komando au askari yeyote wa JWTZ hadi pale utakapokuwa eneo la kazi zao. Mambo mengi yanayofanywa na Watanzania hatuna budi kutambua na kuheshimu kwamba wanaofanya tuwe hivi ni wanajeshi wetu shupavu.

Wakati sisi tukipata moja baridi na moja moto, tukijirusha na miziki ya kizazi kipya, au tukistarehe na wapenzi wetu-JWTZ kwa ujumla wao wako kazini! Mara zote wamekataa kwa tahadhari na weledi wa hali ya juu wakiwa tayari kukabiliana na adui (siyo vibaka wa ndani). Unapoona ndege zinaruka na nyingine zikitua, ujue ni kwa sababu JWTZ wanatekeleza wajibu wao vizuri.

Masuala ya kuwapo vibaka ni kushindwa kazi kwa Polisi na wengine wa aina yao! Komando hawezi kwenda Temeke kusaka Mbwa Mwitu! Hiyo si saizi yao.

Nihitimishe kwa kusema kazi ya JWTZ utaijua pale utakapokuwa karibu na kazi zao! Mtoa mada ukiweza, omba siku moja au mbili uwe kule Kasulu au Ngara mpakani uone wanaume wanavyohangaika kulinda hii nyumba inayoitwa Tanzania na wenye nyumba wanaoitwa "Watanzania". Tena basi, wenye magari wawe na huruma. Wasiwapite barabarani. Wawape lifti! Hili ni Jeshi letu. Tunapaswa kujivunia hiki chombo!

Hongereni sana JWT
 
Macomandoo kwanini wasitumike hata mle benki kuu kuzuia wizi kama wa Epa?au TRA kuzuia mambo ya ufisadi.

Mkuu pesa za EPA aziibiwi kwa kutumia nguvu bali kiulaini tu zinachukuliwa kwa document zote kuwepo
 
Ni kufanya maonyesho kwenye sherehe za kitaifa?

Hawa komandoo wanaifanyia nini Tanzania kwa wakati huu ambao nchi ina amani (haina vita)?

Kila uchao benki zinavamiwa. Polisi wanapata taarifa kwamba majambazi wanasilaha. Wanapotezea. Komandoo hawawezi kutumika kwenye mazingira haya?

Wizi wa uporaji magari na fedha za wafanyabiashara unafanyika kila kona. Komandoo hawawezi kutumika hata kuwakimbiza, kama Polisi wanaogopa?

Wanyamapori kama vile Tembo wanauawa sana. Serikali inapeleka "mgambo" kwa jina la askari wa kulinda wanyama pori. Kwanini komandoo wasitumike?

Ajali za baharini zinatokea. Wanaanchiwa wavuvi kusaidia uokozi. Kwanini komandoo wasitumike, wakati wao wamepata mafunzo ya juu kabisa ya usalama na uokoaji?

Au kazi yao ni kutumika kwenye vikosi vya umoja wa mataifa tu?

Ahsante kwa kuleta hoja
 
Macomandoo kwanini wasitumike hata mle benki kuu kuzuia wizi kama wa Epa?au TRA kuzuia mambo ya ufisadi.

Wizi wa EPA na Ufisadi ni wa kisayansi zaidi si wa kutumia mabavu wala nguvu.Polisi, TAKUKURU na mahakama vinatosha sana kukiwa na dhamira ya dhati ya mkuu wa nchi

Tatizo tulilonalo ni kuzoeleka kwa rushwa ambayo imezaa ufisadi kiasi kuwa kila mfanyakazi anatamani kupata nafasi .Ukiona mtu anapiga kelele ya mafisadi hajapata mwanya
 
Kazi ya commando(special forces operator) ni kufanya covert military operations

Inaweza ikawa hostage rescue,sabotage,assasination au conventional warfare

Ila kwa kwa kwenye battlefield wanafaa sana kwa close quarter combat

Pia commando wana operate in small and light units

Kazi za makomando wa bongo ni highly classified information hata wanajeshi wa sector nyingine hawajui
 
Kwa mujibu wa katiba ya yetu na kimuundo wa jwtz, yote uliyoyataja siyo kazi za msingi (core functions) za jeshi kwa ujumla wake. Wakati wewe unalala nakukoroma kuna ni kwasababu kuna watu wapo kwenye covert and overt military operations nje na ndani ya tz. Bila wewe kujua wakati ukiwa unaendelea na kazi zake labda customer care au kuuza vocha au icecream. Jwtz muda wote wapo kazini kuzuia yanayotokea sudan kusini, durfur,drc etc yasitokee hapa tz.
 
Back
Top Bottom