Komandoo wa Tanzania wana kazi gani?

Komandoo wa Tanzania wana kazi gani?

Wizi wa EPA na Ufisadi ni wa kisayansi zaidi si wa kutumia mabavu wala nguvu.Polisi, TAKUKURU na mahakama vinatosha sana kukiwa na dhamira ya dhati ya mkuu wa nchi

Tatizo tulilonalo ni kuzoeleka kwa rushwa ambayo imezaa ufisadi kiasi kuwa kila mfanyakazi anatamani kupata nafasi .Ukiona mtu anapiga kelele ya mafisadi hajapata mwanya

Makomandoo hawatumiwi kwenye kazi nyepesi za kiintelijensia?
 
3.Kusaidia mamlaka zingine za kiraia na kushirikiana na vyombo vingine vya usalama ktk majanga mbalimbali kama ajali,mafuriko,migomo,na kutuliza ghasia kubwa.

Acha wanyama wetu waendelee kuuliwa porini!! Ila 'wananchi wakigoma ni virungu tu'. Asante kwa taarifa.
 
Ukamandoo jeshini ni kipaji ambacho ni wachache sana huweza mafunzo yake yanyohusu matumizi ya mwili na silaha. Kwa mfano makomandoo wa marekani wanaojulikana kama SEAL ni wachache sana ukilinganisha na jeshi lote la Marekani. Watu hawa si wa kupigana vita ya kawaida tu, bali hutumika katika operationsmaalum zinazohitaji vipaji vya hali ya juu sana kuhus matumizi ya mwili na silaha; kwa mfano operation inayotakiwa imalizike kwa muda mfupi kwa ushindi.

Operesheni hizo huwa siyo lazima ziwe za kivita: Marekani wameatumia SEALs katika kuwakamata wauza madawa ya kulevya, kwa mfano kumakamata Manuel Noriega. Kwa hiyo matumizi ya makomandoo ni unlimited, siyo vita conventional tu, bali vita yoyote inayolihusu taifa. Kwa wenzetu Marekani kuna makomandoo wa aina mbili; wale wanaohusu matukio ya nje ya nchi, ambao ndio SEALs na wale wanaohusu matukio ndani ya nchi ambao hujulikana kama SWAT.

Kosa la mtoa mada ni kudhani kuwa makomandoo wanaweza kwenda kulinda au kupambana, hapana wao ni kwa ajili ya ya kukamilisha operation iliyokwisha pangwa. Kuzuia wizi wa benki haiwezi kuwa kazi ya makomandoo kwa vile wizi huo hutokea ghafla bila kuwepo kwa taarifa zozote za kuweka mkakati wa mapambano; usidhani kuwa makomandooo wana miili ya chuma, hapana, sifa yao kubwa ni kuwa wana ubongo unaofikiria haraka sana wakati wa operesheni, na miili yao inaweza ku-react haraka sana tena kwa nguvu sana wakati huo.

Nadhani kosa linakuwa ni kwa upande wa watu wetu wa usalama wa taifa kushindwa kujua mipango ya ujambazi kabla haujatokea. CIA ndiyo hutoa taarifa zinazosaidia SEALS kupanga mpango wa mashambulizi. Kwetu sisi USALAMA wa taifa wanafanya kazi ya kung'oa watu meno kwa bisibisi lakini hawajui taarifa za uwezekano wa kutokea kwa ujambazi.
 
Ni kufanya maonyesho kwenye sherehe za kitaifa?

Hawa komandoo wanaifanyia nini Tanzania kwa wakati huu ambao nchi ina amani (haina vita)?

Kila uchao benki zinavamiwa. Polisi wanapata taarifa kwamba majambazi wanasilaha. Wanapotezea. Komandoo hawawezi kutumika kwenye mazingira haya?

Wizi wa uporaji magari na fedha za wafanyabiashara unafanyika kila kona. Komandoo hawawezi kutumika hata kuwakimbiza, kama Polisi wanaogopa?

Wanyamapori kama vile Tembo wanauawa sana. Serikali nonsense!
 
[h=3]Fikiria tu kwa harakaharaka mtu mwenye uwezo wa kuvunja tofali la kuanzia nchi sita kwenda juu labda kwa kutumia kichwa, mikono au miguu...unadhani anastahili majukumu ya aina gani?.[/h]
 
Matukio mengi ya mauaji ya utata ujambazi wa kutisha ni sehemu ya kutestiwa ukomandoo wao.ktk kipindi hiki cha amani huwa wanafanya kazi za siri sana.
 
Ni kufanya maonyesho kwenye sherehe za kitaifa?

Hawa komandoo wanaifanyia nini Tanzania kwa wakati huu ambao nchi ina amani (haina vita)?

Kila uchao benki zinavamiwa. Polisi wanapata taarifa kwamba majambazi wanasilaha. Wanapotezea. Komandoo hawawezi kutumika kwenye mazingira haya?

Wizi wa uporaji magari na fedha za wafanyabiashara unafanyika kila kona. Komandoo hawawezi kutumika hata kuwakimbiza, kama Polisi wanaogopa?

Wanyamapori kama vile Tembo wanauawa sana. Serikali inapeleka "mgambo" kwa jina la askari wa kulinda wanyama pori. Kwanini komandoo wasitumike?

Ajali za baharini zinatokea. Wanaanchiwa wavuvi kusaidia uokozi. Kwanini komandoo wasitumike, wakati wao wamepata mafunzo ya juu kabisa ya usalama na uokoaji?

Au kazi yao ni kutumika kwenye vikosi vya umoja wa mataifa tu?

Sina uhakika iwapo hata hao makomando tunao leo
 
kama makomando wakifanya hzo kaz za kuzuia uwiz wa mabenki uporaji n.k...jeshi la polisi litakua na kaz gan sasa nchini..?...
 
Sina uhakika iwapo hata hao makomando tunao leo
wapo.

Nenda 92kj morogoro utawakuta
wanafanya nini huko kambini wakati kuna mambo mengi yanaharibika?

nenda jeshini kaone shughuri zao
sawa.

kama makomando wakifanya hzo kaz za kuzuia uwiz wa mabenki uporaji n.k...jeshi la polisi litakua na kaz gan sasa nchini..?...
polisi wameshindwa. ni benki gani imevamiwa polisi wakafanikiwa kuweka mambo sawa?
 
labda hawana mafunzo ya kutosha kukabiliana na hali kama hzo.....jua kwamba mwalimu hawezi kukujibia maswali ila atakupa mbinu za kujibu maswali kwhyo labda kazi yao iwe ni kuwafundsha tu
 
Ni kufanya maonyesho kwenye sherehe za kitaifa?

Hawa komandoo wanaifanyia nini Tanzania kwa wakati huu ambao nchi ina amani (haina vita)?

Kila uchao benki zinavamiwa. Polisi wanapata taarifa kwamba majambazi wanasilaha. Wanapotezea. Komandoo hawawezi kutumika kwenye mazingira haya?

Wizi wa uporaji magari na fedha za wafanyabiashara unafanyika kila kona. Komandoo hawawezi kutumika hata kuwakimbiza, kama Polisi wanaogopa?

Wanyamapori kama vile Tembo wanauawa sana. Serikali inapeleka "mgambo" kwa jina la askari wa kulinda wanyama pori. Kwanini komandoo wasitumike?

Ajali za baharini zinatokea. Wanaanchiwa wavuvi kusaidia uokozi. Kwanini komandoo wasitumike, wakati wao wamepata mafunzo ya juu kabisa ya usalama na uokoaji?

Au kazi yao ni kutumika kwenye vikosi vya umoja wa mataifa tu?

Ndugu yangu kila kikosi cha ulinzi na usalama kina kazi zake,hao makomando ukiwapeleka katika kupambana na majambazi watauawa wote kwa sbbu hawana mbinu za kupambana na majambazi,bado itabaki kuwaachia polisi kushuhulikia wahalifu,wanajeshi kazi zao kulinda mipaka na kupambana na adui atokae nje na sio kudil na uhalifu hakuna mitaala hiyo ktk mafunzo yao,wala usalama wa taifa hawezi kufanya kazi za upelelezi za polisi,wala kulinda mipaka km wanajeshi,kwa hiyo bado itabaki kila kikosi na kazi zake ukiwapa kazi nyengine na kikosi kingine ndio yanaanza kutokezea matatizo,kwa hapo nadhani umeelewa.
 
Nimeelewa kwamba komandoo hawezi kupambana na jambazi. Yaani jambazi anamchakaza komandoo.
 
KM.jpg

km1.jpg
km2.jpg
View attachment 142162
 
mkuu hao wanasubiri siku chadema wakiandamana kudai katiba ndio wafanye kazi yao kazi zao nyengine ni kutoa watu meno bila ganzi na kutokomeza ujangili kama ulivyoona katika ile operation
 
Back
Top Bottom