Ni kufanya maonyesho kwenye sherehe za kitaifa?
Hawa komandoo wanaifanyia nini Tanzania kwa wakati huu ambao nchi ina amani (haina vita)?
Kila uchao benki zinavamiwa. Polisi wanapata taarifa kwamba majambazi wanasilaha. Wanapotezea. Komandoo hawawezi kutumika kwenye mazingira haya?
Wizi wa uporaji magari na fedha za wafanyabiashara unafanyika kila kona. Komandoo hawawezi kutumika hata kuwakimbiza, kama Polisi wanaogopa?
Wanyamapori kama vile Tembo wanauawa sana. Serikali inapeleka "mgambo" kwa jina la askari wa kulinda wanyama pori. Kwanini komandoo wasitumike?
Ajali za baharini zinatokea. Wanaanchiwa wavuvi kusaidia uokozi. Kwanini komandoo wasitumike, wakati wao wamepata mafunzo ya juu kabisa ya usalama na uokoaji?
Au kazi yao ni kutumika kwenye vikosi vya umoja wa mataifa tu?