Kombe la Shirikisho Afrika: Yanga vs BDF XI [14 Feb 2014]

Kombe la Shirikisho Afrika: Yanga vs BDF XI [14 Feb 2014]

J

At lest umeongea point,lakini hiyo ya kutangaza tenda ya kuonesha mechi..mmmmh,kwani wenye tv wanasubiri tenda ya kuonesha mechik kwani umekuwa ujenzi wa barabara..?..ratiba wanaijua mapema na wanajua mechi itachezwa lini..na wanaosema yanga imegoma kuoneshwa mechi yao,yanga ilitangaza lini mgomo?
Mkuu kwenye biashara yoyote kutangangaza tenda kupo hata sisi wafugaji huwa tunatangaza kwamba jamani mimi nauza ng'ombe wangu yule Nzangamba mkubwa mkwendu mwenye hela anajitokeza ukiridhika nayo unachukua.

Wanaosema kwamba Yanga walikataa wana hoja, mimi kwa masikio yangu kupitia kituo kimoja cha redio nilimsikia Jerry Muro anasema wao kama Yanga hawako tayari mechi ionyeshwe kwa Dar es Salaam, walikuwa tayari mechi ionyeshwe mikoa mingine kwa makubaliano maalumu kama kuna TV ilijitokeza kwa maana ya kutorusha matangazo Dar es salaam hapo sijui ila alikataa hataki mechi kurushwa Dar es salaam na kwa sababu Dar es salaam ndo kuna watazamaji wengi hasa hawa wa ving'amuzi huenda wenye TV zao walishindwa masharti kwa nini walipe halafu wakatazwe kupeleka kule ambako wana wateja wengi.

Lakini twende mbele turudi nyuma ni kweli watu wanazipenda sana hizi timu (Simba na Yanga) lakini viongozi wa hizi timu wanakatisha tamaa sana huwezi kuzuia mamilioni ya watu wasione wakati wewe soko lako la viingilio limelenga watu chini elfu 60. Wangekuwa na liberated mind wangeshusha kwanza gharama za viingilio halafu haki za matangazo wangeuza kwa wenye TV na hapa mapato yangekuwa makubwa kuliko ya kutegemea mlangoni.
 
Masuke hatujawah kukosena heshima mimi na wewe ndugu yangu. inakuaje mpaka tunaanza kuingiliana kwenye mambo ambayo huwa hayachangiwi? huu ukaribu wa kutaka @bantu lady akukaribishe unaanzia wapi? ndugu yangu masuke tuonane hivi hivi lakini tusifikie hatua ya kuanza mpaka kuwakaribia watu wa karibu ya watu wengine. huyu bantu lady sikukutana naye barabarani hivyo nawaomba ndugu zangu msimkaribie hata kujifanya kumpa maneno matamu n,k tafadhari. natoa hili kama onyo kwenu ndugu. @moderators hili mliwekee maanani. bantu lady ni mke wangu wandoa kabisa. yeye yanga mimi simba.
Mkuu usipaniki sana kuwa na amani, mwenyewe amekataa kunikaribisha na hata kama angenikaribisha naanzaje kwenda Southern Sun usiku usiku na kuacha familia yangu. Familia yangu ndo kitu cha mhimu hapa duniani kuliko kitu chochote.
 
Sikukaribishi kabisa, umevunja makubaliano. Tena bora ungebaki kwa mikia wako, umekuwa upande wa wapinzani tunaocheza nao mechi.
Heee ndio maana hata sijakutakia Happy Valentine's...
Bora hujanikaribisha wala kunitakia Valentine njema maana mmeo anavyowaka talaka ingekuhusu.
 
Viongoz wa hiz timu zetu za Kulwa na Doto wanakera sana, wao wameweka mbele maslahi yao binafsi.
Ndo tuliowachagua na bahati mbaya kwa Tanzania mtu mwenye hela ndo anayeonaekana anaweza kila kitu, yeye ndo mwenye akili, yeye ndo anayejua uongozi. Angalia hata upande wa pili Zakaria anavyoamua kuchukua majukumu karibia yote.
 
Mechi za kombe la shirikisho barani Afrika kwa ngazi ya vilabu zinaanza mwishoni mwa wiki hii.

Wawakilishi wa Tanzania Bara Young Africans SC watakuwa nyumbani wakimenyana na BDF XI kutoka Botswana katika mechi ya kwanza ya mzunguko wa kwanza.

Hali ya hewa ya jiji la Dar es Salaam kwa siku ya leo ni jua, vipindi vifupi vya mawingu huku upepo ukivuma kutoka kaskazini mashariki kuelekea kusini magharibi.


Yanga SC 2 (FT) 0 BDF XI
Dk.1, 56 Amisi Tambwe

1600 PM

Waamuzi:
Thierry Nkurunzinza (Bur)
Ramadhani Nijimbere (Bur)
George Gatogato (Bur)

Get
=====================

UPDATES:

MMGL0060.jpg

Mchezaji wa timu ya Yanga,Mrisho Khalfan Ngassa akiwania mpira na Mchezaji wa timu ya BDF XI FC ya nchini Botswana wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jini Dar es salaam leo

MMGL0118.jpg

Mashabiki ya Yanga wakifuatilia mchezo kwa makini

Mpira umekwisha na matokeo ni Yanga SC 2 - 0 BDF XI

Magoli yote mawili yamefungwa na Hamis Tambwe dakika ya kwanza ya mchezo na dakika ya 55 ya mchezo.

hongereni ndala kwa ushindi safi sana tz up..
 
Acha uongo,kwa hy unaniambia mechi zote za nyuma zilikuwa zinaoneshwa?!!!

wewe mbona unashadidia kutooneshwa unanufaikaje , hayo mambo hayana nafasi kwenye dunia ya leo. wapenzi wa yanga mikoani imetuudhi sana
 
Bora hujanikaribisha wala kunitakia Valentine njema maana mmeo anavyowaka talaka ingekuhusu.

Ha ha hahaaaaaa mkuu Masuke unamsikiliza kikaragosi changu Komeo Lachuma?
Huyo ni wakumzoea tu, leo ni siku ya upendo inatakiwa kukaribisha tu, ingekuwa si familia hope ungetu join.
Maana msukuma wangu ndugu yako tena, wala hanaga neno. Mpole sana msukuma huyu, nikutakie Valentine njema mkuu.
Ila umeniangusha kutoishangilia Yanga, hata kauzalendo kidogo jamani!!!
 
Last edited by a moderator:
Azam ndo wafadhili wa ligi ya Uganda so lazima waonyeshe mechi za ligi yao
 
nashukuru Masuke kuonesha ustaarab. wanawake wa siku hizi tuwazoee ndugu yangu. mimi nimeshazoea kuitwa buzi,kikaragosi n.k wala sishangai. nasikitka tu kama mama mkwe wangu angejua naitwa hivi??? ni suala la makuzi si malezi. mi napokea matusi yote toa kwa bibie Bantu lady najua ni wapi sisi tunakutana na ktk mazingira gani. akina Makoye Matale sijui kama wanabariki haya maneno ya dhihaka ya dada yao kwangu.lakini hamna shida bado ntaonesha upendo kwake. nafurah kwa yanga kushinda leo na pia huko iendako baadaye ikashinde. sina ubaya na yanga na siku zote nafurahia mahusiano yetu. sipend kuona mtu mwingine akimmiliki huyu dada.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom