Mkuu kwenye biashara yoyote kutangangaza tenda kupo hata sisi wafugaji huwa tunatangaza kwamba jamani mimi nauza ng'ombe wangu yule Nzangamba mkubwa mkwendu mwenye hela anajitokeza ukiridhika nayo unachukua.J
At lest umeongea point,lakini hiyo ya kutangaza tenda ya kuonesha mechi..mmmmh,kwani wenye tv wanasubiri tenda ya kuonesha mechik kwani umekuwa ujenzi wa barabara..?..ratiba wanaijua mapema na wanajua mechi itachezwa lini..na wanaosema yanga imegoma kuoneshwa mechi yao,yanga ilitangaza lini mgomo?
Wanaosema kwamba Yanga walikataa wana hoja, mimi kwa masikio yangu kupitia kituo kimoja cha redio nilimsikia Jerry Muro anasema wao kama Yanga hawako tayari mechi ionyeshwe kwa Dar es Salaam, walikuwa tayari mechi ionyeshwe mikoa mingine kwa makubaliano maalumu kama kuna TV ilijitokeza kwa maana ya kutorusha matangazo Dar es salaam hapo sijui ila alikataa hataki mechi kurushwa Dar es salaam na kwa sababu Dar es salaam ndo kuna watazamaji wengi hasa hawa wa ving'amuzi huenda wenye TV zao walishindwa masharti kwa nini walipe halafu wakatazwe kupeleka kule ambako wana wateja wengi.
Lakini twende mbele turudi nyuma ni kweli watu wanazipenda sana hizi timu (Simba na Yanga) lakini viongozi wa hizi timu wanakatisha tamaa sana huwezi kuzuia mamilioni ya watu wasione wakati wewe soko lako la viingilio limelenga watu chini elfu 60. Wangekuwa na liberated mind wangeshusha kwanza gharama za viingilio halafu haki za matangazo wangeuza kwa wenye TV na hapa mapato yangekuwa makubwa kuliko ya kutegemea mlangoni.