Kombe la Shirikisho Afrika: Yanga vs BDF XI [14 Feb 2014]

Mkuu kwenye biashara yoyote kutangangaza tenda kupo hata sisi wafugaji huwa tunatangaza kwamba jamani mimi nauza ng'ombe wangu yule Nzangamba mkubwa mkwendu mwenye hela anajitokeza ukiridhika nayo unachukua.

Wanaosema kwamba Yanga walikataa wana hoja, mimi kwa masikio yangu kupitia kituo kimoja cha redio nilimsikia Jerry Muro anasema wao kama Yanga hawako tayari mechi ionyeshwe kwa Dar es Salaam, walikuwa tayari mechi ionyeshwe mikoa mingine kwa makubaliano maalumu kama kuna TV ilijitokeza kwa maana ya kutorusha matangazo Dar es salaam hapo sijui ila alikataa hataki mechi kurushwa Dar es salaam na kwa sababu Dar es salaam ndo kuna watazamaji wengi hasa hawa wa ving'amuzi huenda wenye TV zao walishindwa masharti kwa nini walipe halafu wakatazwe kupeleka kule ambako wana wateja wengi.

Lakini twende mbele turudi nyuma ni kweli watu wanazipenda sana hizi timu (Simba na Yanga) lakini viongozi wa hizi timu wanakatisha tamaa sana huwezi kuzuia mamilioni ya watu wasione wakati wewe soko lako la viingilio limelenga watu chini elfu 60. Wangekuwa na liberated mind wangeshusha kwanza gharama za viingilio halafu haki za matangazo wangeuza kwa wenye TV na hapa mapato yangekuwa makubwa kuliko ya kutegemea mlangoni.
 
Mkuu usipaniki sana kuwa na amani, mwenyewe amekataa kunikaribisha na hata kama angenikaribisha naanzaje kwenda Southern Sun usiku usiku na kuacha familia yangu. Familia yangu ndo kitu cha mhimu hapa duniani kuliko kitu chochote.
 
Sikukaribishi kabisa, umevunja makubaliano. Tena bora ungebaki kwa mikia wako, umekuwa upande wa wapinzani tunaocheza nao mechi.
Heee ndio maana hata sijakutakia Happy Valentine's...
Bora hujanikaribisha wala kunitakia Valentine njema maana mmeo anavyowaka talaka ingekuhusu.
 
Viongoz wa hiz timu zetu za Kulwa na Doto wanakera sana, wao wameweka mbele maslahi yao binafsi.
Ndo tuliowachagua na bahati mbaya kwa Tanzania mtu mwenye hela ndo anayeonaekana anaweza kila kitu, yeye ndo mwenye akili, yeye ndo anayejua uongozi. Angalia hata upande wa pili Zakaria anavyoamua kuchukua majukumu karibia yote.
 
hongereni ndala kwa ushindi safi sana tz up..
 
Acha uongo,kwa hy unaniambia mechi zote za nyuma zilikuwa zinaoneshwa?!!!

wewe mbona unashadidia kutooneshwa unanufaikaje , hayo mambo hayana nafasi kwenye dunia ya leo. wapenzi wa yanga mikoani imetuudhi sana
 
Bora hujanikaribisha wala kunitakia Valentine njema maana mmeo anavyowaka talaka ingekuhusu.

Ha ha hahaaaaaa mkuu Masuke unamsikiliza kikaragosi changu Komeo Lachuma?
Huyo ni wakumzoea tu, leo ni siku ya upendo inatakiwa kukaribisha tu, ingekuwa si familia hope ungetu join.
Maana msukuma wangu ndugu yako tena, wala hanaga neno. Mpole sana msukuma huyu, nikutakie Valentine njema mkuu.
Ila umeniangusha kutoishangilia Yanga, hata kauzalendo kidogo jamani!!!
 
Last edited by a moderator:
Azam ndo wafadhili wa ligi ya Uganda so lazima waonyeshe mechi za ligi yao
 
Azam ndo wafadhili wa ligi ya Uganda so lazima waonyeshe mechi za ligi yao

Si suala la ufadhili tu bali ni mbinu ya kibiashara pia...
 
nashukuru Masuke kuonesha ustaarab. wanawake wa siku hizi tuwazoee ndugu yangu. mimi nimeshazoea kuitwa buzi,kikaragosi n.k wala sishangai. nasikitka tu kama mama mkwe wangu angejua naitwa hivi??? ni suala la makuzi si malezi. mi napokea matusi yote toa kwa bibie Bantu lady najua ni wapi sisi tunakutana na ktk mazingira gani. akina Makoye Matale sijui kama wanabariki haya maneno ya dhihaka ya dada yao kwangu.lakini hamna shida bado ntaonesha upendo kwake. nafurah kwa yanga kushinda leo na pia huko iendako baadaye ikashinde. sina ubaya na yanga na siku zote nafurahia mahusiano yetu. sipend kuona mtu mwingine akimmiliki huyu dada.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…