Kombe la Shirikisho Barani Afrika 'CAF' Azam FC dhidi ya Triangle United, Wazimbabwe Lazima Wakae!

Kombe la Shirikisho Barani Afrika 'CAF' Azam FC dhidi ya Triangle United, Wazimbabwe Lazima Wakae!

Haya majinga yamefungwa goli la kizembe sana
Patashika ya Kombe la Shirikisho Soka Barani Afrika, Kuendelea kutimua vumbi leo Jumapili ya September 15, 2019 ambapo wawakilishi wa Tanzania Azam FC wakiwakaribisha Triangle United ya kutoka nchini Zimbabwe kwenye Uwanja wa nyumbani wa Azam Complex.

Azam FC walisonga mbele kufikia hatua hii baada ya kuitoa Fasil Kenema ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya mechi ya awali iliyopigwa nchini Ethiopia ambapo Fasil Kenema waliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 na kufuatia mechi iliyopigwa jijini Dar es salaam ambapo Azam FC walitakata kwa ushindi wa mabao 3-1.

Mchezo huu ni burudani ya pekee wiki hii kwenye Kombe la Shirikisho, burudani ambayo si ya kukosa ewe Mzalendo, Mshabiki, Mwanachama na Mdau wa Kandanda, kwani Azam FC ndo wawakilishi wetu Kimataifa hapa nchini Tanzania, hivyo basi twendene kwa wingi tukaujaze Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Mbagala na kuwashangili vilivyo wawakilishi wetu wa ukweli Azam FC.

Wazimbabwe Lazima Wakae.....!KwaHisaniYaNguvuMoja..!Usikose Ukaambiwa, kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10:00 jioni.
••••••••••=================•••••••
Mchezo wa kombe la Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF

Azam FC, wakicheza kwenye dimba lao la Azam Complex, licha ya kucheza vizuri na kutawala mchezo lakini wamejikuta wakikubali kichapo kwa kufungwa bao moja bila na Triangle United lililofungwa na Ralph Kawondera dakika ya 34 ya mchezo.

View attachment 1208104View attachment 1208106
 
Kwa hiyo Simba ikifeli hizi timu zingne huko kimataifa zinarukaruka tu
 
Ndairagije afukuzwe stars..TFF tafuteni kocha mzungu kutoka hata Romania
 
Back
Top Bottom