Kombe la Shirikisho Barani Afrika 'CAF' Azam FC dhidi ya Triangle United, Wazimbabwe Lazima Wakae!

Kombe la Shirikisho Barani Afrika 'CAF' Azam FC dhidi ya Triangle United, Wazimbabwe Lazima Wakae!

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya Kombe la Shirikisho Soka Barani Afrika, Kuendelea kutimua vumbi leo Jumapili ya September 15, 2019 ambapo wawakilishi wa Tanzania Azam FC wakiwakaribisha Triangle United ya kutoka nchini Zimbabwe kwenye Uwanja wa nyumbani wa Azam Complex.

Azam FC walisonga mbele kufikia hatua hii baada ya kuitoa Fasil Kenema ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya mechi ya awali iliyopigwa nchini Ethiopia ambapo Fasil Kenema waliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 na kufuatia mechi iliyopigwa jijini Dar es salaam ambapo Azam FC walitakata kwa ushindi wa mabao 3-1.

Mchezo huu ni burudani ya pekee wiki hii kwenye Kombe la Shirikisho, burudani ambayo si ya kukosa ewe Mzalendo, Mshabiki, Mwanachama na Mdau wa Kandanda, kwani Azam FC ndo wawakilishi wetu Kimataifa hapa nchini Tanzania, hivyo basi twendene kwa wingi tukaujaze Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Mbagala na kuwashangili vilivyo wawakilishi wetu wa ukweli Azam FC.

Wazimbabwe Lazima Wakae.....!KwaHisaniYaNguvuMoja..!Usikose Ukaambiwa, kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10:00 jioni.
••••••••••=================•••••••

Kutoka Chamazi Mbagala jijini Dar es salaam..Mchezo wa kombe la Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF;

Azam FC, wakicheza kwenye dimba lao la Azam Complex, licha ya kucheza vizuri na kutawala mchezo lakini washambuliaji wao walishindwa kuwa watulivu kwenye lango la Triangel ili kuweza kufanya umaliziaji ambao ungeleta matokeo ya ushindi.

Hivyo kujikuta wakikubali kichapo kwa kufungwa bao moja bila na Triangle United, bao lililofungwa na Ralph Kawondera dakika ya 34 ya mchezo.

Kwa matokeo haya, Azam FC ili iweze kusonga hatua inayofuata watahitaji kuwafunga Triangle mabao 2-0 ugenini kwenye mchezo wa marudiano.
IMG_20190915_104601_093.jpeg
FB_IMG_1568534486409.jpeg
 
Kila la heri Azam FC, wawakilishi wetu Kimataifa nchini Tanzania

Wazimbabwe Lazima Wakae
 
Az
Patashika ya Kombe la Shirikisho Soka Barani Afrika, Kuendelea kutimua vumbi leo Jumapili ya September 15, 2019 ambapo wawakilishi wa Tanzania Azam FC wakiwakaribisha Triangle United ya kutoka nchini Zimbabwe kwenye Uwanja wa nyumbani wa Azam Complex.

Azam FC walisonga mbele kufikia hatua hii baada ya kuitoa Fasil Kenema ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya mechi ya awali iliyopigwa nchini Ethiopia ambapo Fasil Kenema waliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 na kufuatia mechi iliyopigwa jijini Dar es salaam ambapo Azam FC walitakata kwa ushindi wa mabao 3-1.

Mchezo huu ni burudani ya pekee wiki hii kwenye Kombe la Shirikisho, burudani ambayo si ya kukosa ewe Mzalendo, Mshabiki, Mwanachama na Mdau wa Kandanda, kwani Azam FC ndo wawakilishi wetu Kimataifa hapa nchini Tanzania, hivyo basi twendene kwa wingi tukaujaze Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Mbagala na kuwashangili vilivyo wawakilishi wetu wa ukweli Azam FC.

Wazimbabwe Lazima Wakae.....!KwaHisaniYaNguvuMoja..!Usikose Ukaambiwa, kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10:00 jioni.View attachment 1208104View attachment 1208106
Azam wapo na viungo wazuri sana kuliko simba na yanga Mudathir na Sure Boy
 
Azam FC timu bora kwa bidhaa bora kila la heri kwenye game ya leo

Kila atakayeingia uwanjani koo lake litalainishwa kwa Ukwaju..!
 
jana wababe wa Simba UD SONGO wamefungwa na wazimbabwe, kumbe hawa UD SONGO ni vibonde sema walikutana na timu mbovu Simba
 
jana wababe wa Simba UD SONGO wamefungwa na wazimbabwe, kumbe hawa UD SONGO ni vibonde sema walikutana na timu mbovu Simba
Simba sio mbaya walifungwa na hao kwa sababu ya kujiamini kuwa nyumbani hakuna timu inayo weza kutoka na pili yule msemaji wao kuwa benchmark
 
Wewe unawaza kula tu acha njaa hiyo
Huo ndo utaratibu wa Azam FC kwa sasa toka mechi iliyopita, ya Kimataifa, sasa wapi nimewaza kula?

Tafadhali sana wajinga msitupotezee muda wa kuwajibu..Kuna wenye IQ kubwa ambao hawapati nafasi ya kujibiwa kwa sababu yenu.

Kila la heri Azam FC
 
Huo ndo utaratibu wa Azam FC kwa sasa toka mechi iliyopita, ya Kimataifa, sasa wapi nimewaza kula?

Tafadhali sana wajinga msitupotezee muda wa kuwajibu..Kuna wenye IQ kubwa ambao hawapati nafasi kwa sababu yenu.

Kila la heri Azam FC
Best regards
 
Sasa kwa Yanga tutasemaje si zaidi ya mbovu ikiwa hawapati bao mpaka mipira ya kutengwa..!

Mmezoea Kujidhalilisha wenyewe![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
jana wababe wa Simba UD SONGO wamefungwa na wazimbabwe, kumbe hawa UD SONGO ni vibonde sema walikutana na timu mbovu Simba
 
Habari njema!
Mudathir amepona!
Mwantika amepona!
Ngoma kapona!

Habari mbaya!
Aggrey Morris
Bado anapigania uimara wa afya yake!
Screenshot_20190915_132630.jpeg
 
Ukwaju Ice Cream, na Ukwaju Juice ambao utazinduliwa rasmi hapo uwanjani..Radha zote zitapatikana mkuu..!

Kila la heri Azam FC
Ukwaju 2! Ule wa kunyonya na ule wa Juice!
 
Kikosi cha Azam FC kitakachoanza kwenye mtanange dhidi ya Triangle FC
FB_IMG_1568548358220.jpeg
 
Back
Top Bottom