Patashika ya Kombe la Shirikisho Soka Barani Afrika, Kuendelea kutimua vumbi leo Jumapili ya September 15, 2019 ambapo wawakilishi wa Tanzania
Azam FC wakiwakaribisha
Triangle United ya kutoka nchini Zimbabwe kwenye Uwanja wa nyumbani wa
Azam Complex.
Azam FC walisonga mbele kufikia hatua hii baada ya kuitoa Fasil Kenema ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya mechi ya awali iliyopigwa nchini Ethiopia ambapo Fasil Kenema waliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 na kufuatia mechi iliyopigwa jijini Dar es salaam ambapo Azam FC walitakata kwa ushindi wa mabao 3-1.
Mchezo huu ni burudani ya pekee wiki hii kwenye Kombe la Shirikisho, burudani ambayo si ya kukosa ewe
Mzalendo, Mshabiki, Mwanachama na Mdau wa Kandanda, kwani Azam FC ndo wawakilishi wetu Kimataifa hapa nchini Tanzania, hivyo basi twendene kwa wingi tukaujaze Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Mbagala na kuwashangili vilivyo wawakilishi wetu wa ukweli Azam FC.
Wazimbabwe Lazima Wakae.....!KwaHisaniYaNguvuMoja..!Usikose Ukaambiwa, kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10:00 jioni.
View attachment 1208104View attachment 1208106