Tatizo mapenzi yenu juu ya Ukraine yanafanya mnaanza kupotoka haya baadhi ya ushahidi wa hizo topic huo hapo nyingine unaweza kusearch chukua heading kama ilivyo ingiza google utapelekwa moja kwa moja kwenye site husika
Zimeandikwa lini na nani wameandika na kila kitu angalia hapo utaona au unataka ushahidi gani mwingine?
Hakuna propaganda inasambazwa basi pingana na The Guardian hapo kwamba wanasambaza propaganda
View attachment 2276631View attachment 2276634View attachment 2276635
Asante sana, nashukuru. Ila: Kwa nini hujataja vyanzo tangu mwanzo? Sasa tumeona 3 kati ya sentensi 8 tulizopewa kama nukuu. Basi hata kama umeleta nukuu zote (mimi naona ni kosa kuleta sentensi kama nukuu bila kuonyesha chanzo, kama ni pro- au contra ya kitu chochote) sahihi,
mpangilio wako unadai eti kabla ya uvamizi wa Putin media za magharibi waliona kasoro tu huko Ukraine na baada ya uvamizi wanasifu tu. Hii si kweli .
Media zinazofaa kuheshimiwa zinatoa taarifa kila upande: sifa na kasoro, uzuri na ubaya.
Hata baada ya Putin kuanzsha vita yake, nimeona taarifa zilizoeleza matatizo ya ufisadi nchini Ukraine; commentaries zilizoeleza jinsi gani kiasi cha ufisadi inaweza kuwa kizuizi cha kupokea nchi katika Umoja wa Ulaya na kadhalika.
Jinsi unavyoleta vichwa vya habari unapiga propaganda. Mfano makala ya Josh Cohen kupitia Reuters - je umeisoma???
Ndani yake kuna ukosoaji mwingi kwa makundi wa kulia - pamoja na sentensi
"To be clear, the Kremlin’s claims that Ukraine is a hornets’ nest of fascists are false: far-right parties performed poorly in Ukraine’s last parliamentary elections, and Ukrainians reacted with alarm to the National Militia’s demonstration in Kiev."
Jinsi unavyoleta mambo hapa unaonekana kushikamana na hao wanaosambaa uwongo eti Ukraine inatawaliwa na WaNAzi, au zaidi (jinsi wanavyosema watu kadhaa nchini Urusi): Ukraine wote wana roho ya Unazi wanahitaji "kukombolewa" kama wanataka au la.
Ambayo yote ni uwongo mtupu bila msingi.
Nakubali kabisa kuhesabu na kujadili Wanazi wa Ukraine, lakini pamoja na Wanazi wa Urusi na changamoto ya kichaa katika nchi za Ulaya MAshariki ambako kote kuna makundi madogo ya Wanazi wanaotembea na ishara za watu hao waliojaribu kuangamiza mababu yao.