Komesha Ushabiki maandazi na uchawa: Ukweli Kuhusu China, Marekani, na Ndoto za Kujitegemea

Komesha Ushabiki maandazi na uchawa: Ukweli Kuhusu China, Marekani, na Ndoto za Kujitegemea

CardoVerli

Member
Joined
May 15, 2026
Posts
17
Reaction score
21
Watu wengi mtandaoni wamekuwa wakipiga kelele wakiamini kuwa China au Marekani zinaweza kusimama peke yake bila kusaidiwa na mtu, au kwamba nchi hizi zinaweza kutengana kirahisi tu. Huu ni upofu wa kifikra unaoletwa na kukosa data na kutazama dunia kupitia vioo vya simu.

1. Kwa nini Marekani ilienda China?
Makampuni ya Marekani hayakuenda China kutafuta skilled labor bali yalikimbilia nguvukazi ya bei rahisi (cheap labor), kodi nafuu, na ruzuku kubwa za serikali zilizowasaidia kupunguza gharama za uzalishaji bidhaa duniani.

2. Je Marekani itakosa sehemu ya kwenda ikifukuzwa China?
Hapana, haitakosa kabisa. Tayari mfumo wa uzalishaji umeshaanza kuhama (Supply Chain Diversification), ambapo viwanda vinahamia nchi kama Vietnam, Thailand, India, na Mexico kwa ajili ya soko la karibu. Dunia imejaa nchi nyingi zenye nguvukazi ya bei rahisi.

3. Je, China ingekuwa China ya leo bila Magharibi?
Kamwe isingekuwa hapa ilipo. Katika miaka ya 1980 na 1990, China ilikuwa masikini sana. Ilikuwa ni uwekezaji, teknolojia, na masoko ya nchi za Magharibi yaliyomwaga mitaji nchini humo ndiyo yaliyoijenga China kuwa kitovu cha viwanda tunachokiona leo.

4. Nchi zinazojitegemea duniani:
Hakuna nchi hata moja duniani inayoweza kusimama peke yake kwa asilimia mia moja. Hata mataifa makubwa yamefungamanishwa kwenye mfumo mmoja wa kimataifa (Globalization) ambapo rasilimali, nishati, na masoko husafirishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

5. Kwa nini kutengana kwao ni ndoto ya mafala?
Watu wanaodhani China na Marekani zinaweza kukata mahusiano leo na kila mtu akasimama kivyake ni wajinga wa uchumi wa dunia. Uchumi wa nchi hizi mbili umeunganishwa kwa mishipa ya damu; Marekani inategemea bidhaa za China kuweka bei za chini kwa wananchi wake, na China inategemea soko la Marekani ili kuendesha viwanda vyake na kuajiri mamilioni ya watu.

Sooooo. kila siku humu kuna discussion ambazo bhna ni uchawa usio na maana
Acha kupumbazwa na stori za vijiweni na ushabiki wa kijinga wa mitandaoni wakati wakubwa wenyewe wanafanya biashara na kujua fika kuwa wote wako kwenye mashua moja ya kufa na kupona

We umekalisha makalio huko na kibando chako cha jero ukikoment online eti china ni better
or Marekani ni better than
 
Ni kweli kwa hali ya dunia ilivyo sasa mataifa yote yanategemeana na hakuna taifa lolote linaloweza kusimama peke yake na likasitawi.

Kwa mantiki hiyo basi taifa kama Iran ilipofikia maelewano na Marekani lazima tu itaumia hali itakayopelekea utawala huo kuanguka ifikapo mwaka ujao.
 
Ni kweli kwa hali ya dunia ilivyo sasa mataifa yote yanategemeana na hakuna taifa lolote linaloweza kusimama peke yake na likasitawi.

Kwa mantiki hiyo basi taifa kama Iran ilipofikia maelewano na Marekani lazima tu itaumia hali itakayopelekea utawala huo kuanguka ifikapo mwaka ujao.
😃😃😃 mwaka ujao mwezi wa ngapi itakua ishaanguka
Ili tupate kutunza kumbu kumbu vyema !!!
 
Back
Top Bottom