Kasiano Muyenzi
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 13,858
- 22,729
- Thread starter
- #61
Kwa mujibu wa Biblia Yesu alipopaa alikwenda juu mbinguni (hapa humaanisha mbinguni ni juu na sio chini), hata Eliya alipoondoka duniani alipaa na kwenda juu akiwa na gari la kukokotwa na farasi.Sasa nimeuliza Mbinguni ni wapi, umesema Peponi. Labda uniambie ni kwenye Sayari nyingine, lakini hii tunayoshi Peponi haipo kwenye ramani, ndio maana nawaza kwa sauti, Je Peponi sehemu ya kufikirika? Unaweza kuniweka sawa na wengine wakapata faida vilevile.
Ukiwa ni msomaji mwelewa wa Biblia huwezi kushindwa kuelewa kuwa mbinguni ni wapi, ila ikiwa si msomaji mwelewa hata ukieleweshwa ni sawa na kulazimisha mbuzi acheze ngoma ya "mwaka wangu" kitu ambacho haiwezekani kabisa.
Nikushauri tu jifunze kuwa mwelewa utaelewa mengi yaliyomo ktk Biblia.