Kongamano la amani: Wanenaji ni Askofu Kakobe, Askofu Malasusa na Sheikh Abdallah

Tunataka kongamano la HAKI haya ya amani yametuchosha sasa.
 
Bado siku saba kufikia tarehe ya uchaguzi lakini bado darasa la TAL halijawaingia - hakuna amani inayokuja bila haki! Tulichokuwa nacho Tz ni utukive tu. Sijui viongozi hawa wa kiroho wamekula maharagwe ya wapi? Wamuulize Baba Askofu Dkt Sheikh Rashid Halima Josephat Gwajima.
 
Ni amani kati ya nani na nani? Hao wote ni pro jpm.Gamanywa mpaka anamwalika polepole wapo kukampeni. Sema ni kampeni za ccm kivingine
 
Waongelee haki na maendeleo. Amani bila haki ni ukondoo
 
Laiti dunia ingekuwa na usawa, kinachohitajika ni kongamano la HAKI na hapo Amani ingekuja yenyewe bila kuwatoa watu majasho namna hii!!
 

Wakati kunafanyika uhayani, ukatili na ushenzi wa wazi dhidi ya wapinzani kwenye chaguzi za marudio, hakukuwa na kongamano la amani. Uchaguzi wote wa serikali za mitaa umenajisiwa hao viongozi hawakuitisha kongamano la kupinga hiyo dhuluma, ila Sasa wameona watu hawako tayari tena kuporwa haki yao ndio wanaitisha kongamano la amani, ili watu watulie waporwe tena haki yao! Wamebug men.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…