Omusolopogasi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2017
- 7,101
- 18,051
Tusikatishane tamaa. Suala la katiba mpya ni la kila mpenda haki nchi hii. Muda wa kudai katiba mpya ni sasa. Siyo kusubiri mpaka 2025.
Mtu mwenye akili timamu huwezi tena kumuamini Lipumba, ni takataka tu inayotafuta njia ya kuendelea kupiga pesa, Cuf haina tena ruzuku, huu ni ubunivu wa kutafuta pesa kwenye ile account yao ya NMB.
Ni wajinga wenzake tu ndio watakaokubali kutumika na Lipumba kwa maslahi yake binafsi.
Yani sasa hivi ndio nimeelewa kumbe ni bora ile rasimu ya Warioba licha ya kina Samwel Sitta na wajinga wenzake kuinajisi lakini ingepitishwa hivyohivyo leo hii tungekuwa tayari tuna tume huru ya uchaguzi zingesalia hoja chache tungeshinikiza zifanyiwe kazi kama serikali tatu.
Wakenya wenzetu wamepitisha kwanza katiba yao mpya na sasa wanadai BBM.