saidoo25
JF-Expert Member
- Jul 4, 2022
- 624
- 1,456
Kongamano la Wahariri naweza kusema limeacha maswali mengi sana kuliko mafanikio tuliyotarajia tuyaone kutokea hapo.
1. Nani aliyewalipa posho na malazi kwa siku zote walizokaa Iringa(Yeye mlipaji ananufaikaje kwa fedha zake alizotoa)
2. Wametajwa wabunge, majaji, mawaziri kuwa ndio wanalimiki Ranchi ya Usangu je ni Kweli Ranchi ya Usangu inamilikiwa na watu binafsi au Serikali? ukweli ukoje kwenye hili. (Kwanini hadi leo wameshindwa kutaja majina yao)
3. Wametajwa watu wanaotumia maji ya mto Ruaha kwa shughuli za Kilimo, je Sheria inasemaje kuhusu wanaotumia maji? ziko Water Use Permit zinazotolewa na Mamlaka za Kiserikali za Mabonde ya Mito chini ya Wizara ya Maji na zinalipiwa ada nadhani kila mwaka kama sikosei.
Kosa la hao wenye vibali vya kutumia maji liko wapi? kwanini watangazwe kwamba ni wahalifu ilihali wanatumia maji kisheria na kama mtu anatumia maji bila kibali sheria inasemaje?
4. Kuna Fununu kwamba Kongamano hilo limeandaliwa mahususi kuwahadaa watanzania kwamba Mradi wa Bwawa la JNHPP hautafanya kazi hata kama utakamalika kwa sababu maji ya mto Ruaha yamekaushwa na wakulima na wafugaji.
5. Point Namba 4 ndio inatajwa sana kufadhili kongamano na kundi hilo hilo hilo la wahariri ndio kila leo linakwenda kwenye Mradi wa JNHPP na kusifia kwamba hakuna kilichosimama.
Huku wakitambua mradi huo umecheleweshwa na mkandarasi kwa miaka 2na una mambo mengi yanahitaji majibu kuhusu shilingi Trilioni 1.5 ambazo mkandarasi alipaswa kuilipa Serikali kwa kuchelewesha mradi kwa mujibu wa mkataba.
Maswali ambayo Kina Balile na Kina Pascal Mayala licha ya kuwa Wanasheria wabobevu wameshindwa kuyauliza kwenye mamlaka husika hadi leo na hatujui kwanini wanafanya hivyo?
Kwa ufupi Wahariri wote wameandaa kongamano hilo ili kutengeneza hadaa na kuwaandaa kisaikolojia watanzania li kufanikisha lengo lao la kuonyesha tatizo la umeme halitakwisha leo wala kesho ili zile biashara zingine za Majenereta na Mikataba mingine iendelee ya kuiuzia umeme Tanesco. kwa kigezo cha kukosekana maji
Uthibitisho ya hayo siku chache Kabla ya Kongamano hilo, Mwenyekiti wa MERICA, Habib Mchange alifanya PRESS alitamka kwamba tutamlaumu Januari Makamba umeme wa mgao atafanya nini kama maji Ruaha hayapo?
MERICA imeshindwa kuuliza kwa nini umeme haukukatika katika kipindi chote cha miaka 6 iliyopita je hali ya ukame imekuja tu baada ya Januari kuwa Waziri? na je kuhusu madai ya baadhi ya watumishi wasio waadilifu wa TANESCO kufungulia maji ya Mabwawa ili yasijae kuzalisha umeme nalo kwa nini halizungumziwi.
Kwanini wazungumziwe kundi moja tu la wakulima na wafugaji ndio waliomaliza maji? na je miaka yote 6 ambayo umeme ulikuwa haukatiki wafugaji na wakulima waliacha shughuli za kilimo na ufugaji? kwanini maswali hayo hayapati nafasi? na kwanini kongamano hilo halikuwashirikisha wakulima na wafugaji kupitia vyama vyao kama MVIWATA na Chama cha Wafugaji Tanzania.
Tuendelee kutafakari kwa pamoja kuhusu kongamano hili na mambo yaliyojificha nyuma ya pazia ila uzuri duniani hakuna siri hasa jambo likishashirikisha watu zaidi ya mmoja na Makamu wa Rais ukweli aliofichwa ataufahamu.
Rejea nyingine muhimu juzi Waziri wa Nishati, Januari Makamba alinukuliwa akisema itahitajika misimu 2 ya mvua kujaza bwawa la nyerere.
Saidoo25.