🤣🤣🤣🤣🤣Mkuu naomba niulize jambo maana hii issue ya kwamba mgao inatengenezwa Ili majenereta ama mikataba ya IPTL/DOWANS irudi inarudiwa rudiwa Sana.
Tanzania kwenye mpango wa taifa imeeleza kufocus kwenye energy mix yaani umeme sio tu kupitia Maji ila gesi, joto ardhi, upepo, solar n.k Sasa wote tunafahamu focus ipo kwenye gesi in fact Kinyerezi 3 Iko mbioni kujengwa Ili gesi izidi kuongeza mchango wake kwenye umeme.
Sasa wote tunafahamu zaidi ya 60% za umeme wa Tz unategemea gesi sio Maji na pia umeme wa gesi ni gharama sana kufua kuliko wa Maji.
1. Je kwanini wapiga Dili wasihujumu gesi maana ndio tegemeo kwenye umeme Tz?
2. Maintenance ya Bomba/mitambo ya gesi ni gharama kuliko umeme wa Maji kwanini wasihujumu gesi wavune mabilion?
3. Pia majenereta Yana faida kiasi gani Hadi yarudishe cost za mgao? Sababu hata hao mafisadi Wana viwanda/mashamba/mahoteli n.k?
Ntashukuru kwa majibu yenu
Mkuu, ukweli ni kuwa kitu chochote kwa sasa kikihusisha tu wizara ya nishati ambako makamba yupo basi lazima uyasikie mengi sana mabaya.........watu watadadavua kinafiki, watamwaga hisia zao hasi, watu watapewa maneno ya wasiwasi a.k.a kuogofya hadi wakimbie. KATU HUTOSIKIA NENO LA MATUMAINI HATA MOJA. Hivyo ndivyo atendewavyo makamba; kuna dhamira ya wazi 'ya kumuua' ambayo hauhitaji hata kutumia darubini kuiona.
Tunazuiwa hata kusikiliza nini kizuri anasema; negative comments mwanzo mwisho......ukijifanya umesikia lolote zuri utatukaniwa hadi your great great grandparents. Siajabu, katika maswali yako haya, ukakutana na katusi huko mbele maana ni maswali yanayohitaji facts na sio longolongo.
Humu akitajwa tu makamba, unacholazimishwa kufanya ni kutaja wizi/madili (usiulize kaiba nini, lini, wapi na kivipi; utatukanwa); unalazimika kutaja biashara ya generators (ukiuliza kivipi utaambulia matusi au majibu yatakushangaza na kukuchekesha); utalazimika kumwita makamba mnafiki kwa hoja kuwa alilipinga bwawa akiwa waziri wa mazingira na sasa analisimamiaje? (Ukisema kuwa alikuwa anafanya kazi yake kwa kipindi hicho kutoa concerns za kimazingira km waziri wa mazingira.......na hii ni kama kweli aliwahi kulipinga. Na kiitifaki wazo lako linaposhindwa kufanya kazi basi hauna budi kuungana na kutekeleza wazo bora zaidi lililopita kitu am ambacho ndo anafanya; utaishia kutukanwa)