Kongamano la Wahariri limeacha maswali mengi. Nani yuko nyuma?

Kama haya mabwawa madogo hayajai Maji ya kuzalisha umeme mwaka mzima Hilo jidubwana mtalijaza na mate? Mimi nasema hata likikamilika halizazalisha kiasi hicho cha umeme kinachosemwa. Sababu kuu ni kwamba haitatokea likajaa katika kiwango kinqchotakiwa.


Hilo bwawa linapigiwa kelele Kama gesi ya mtwara tu. Tatizo la umeme ni neema kwa CCM na hawatopenda liishe Kama ulivyo ujinga wa wengi.
 
Jamani mafisadi yamerudi kwa kasi ya kutisha sasa yanateketeza hakuna kitakachobaki. Kwa sasa yanajipanga kuiba kura 2025 ili yaendelee kubaki madarakani
Hawatoweza, this time ugomvi ndani ya familia utawanufaisha waliomo na wasiokuwepo

Tusubiri.
 
Kuna Fununu kwamba Kongamano hilo limeandaliwa mahususi kuwahadaa watanzania kwamba Mradi wa Bwawa la JNHPP hautafanya kazi hata kama utakamalika kwa sababu maji ya mto Ruaha yamekaushwa na wakulima na wafugaji.
Nikiona watu wanamuamini habibu mchange ,nawashangaaa sanaaaa.
 
Tunapigwa pakubwa sanaaaaa.
 
mimi pia nilijiuliza maswali mengi sana, ila ukweli utajulikana ngoja waje wajuzi wa mambo wasaidie uchambuzi huu mujarab. ila mtoa post nakupa kongole kwa uchambuzi makini sana. KINA BALILE, MCHANGE, KITENGE waje na maelezo
Hakuna cha uchambuzi hala anaewindwa ni mr makamba,, huyu jamaa watu wanamuwinda sana kwasababu ana IQ kubwa sana ndani ya system,, wakimwa gusha huyu, kuelekea 2025 njia yao itakua imekua cake walk kuelekea magogoni, yupo huyo, mwigulu, kinana,,, na kadhalika,, hawa watawindwa sana manake hawa ndo strategists wakubwa waccm kuelekea 2025
 
Huyu Kitenge ana akili gani za kuweza kuwa mmoja wa watu wenye akili kubwa? Habib anajulikana kama ni Msoga team.
 
Naww unaamini kwamba pale utatoka umeme wakutosha kuendesha viwanda are you serious? achana na porojo za watawala wa cccm hakuna kitu pale
 
Nikiona watu wanamuamini habibu mchange ,nawashangaaa sanaaaa.
Sio mchange tu wote kwenye genge lao hakuna mwenye credibility yakusimama mbele za watu wasiotumia utumbo kufikiri wakasema jambo nakuaminika
 
Mwanzisha mada kauliza maswali ya msingi sana. Askofu Fulton Sheen aliwahi kusema " The devil may have his hour but God will have his Day!

Nia ovu hushinda kwa muda tu! Ipo hivyo always

..Mtoa mada ana tatizo ambalo nimeliona kwa Watanzania wengi.

..Mtoa mada hakutakiwa kuuliza maswali kwa watu [ wahariri ]ambao inaelekea hawaamini.

..Alitakiwa afanye utafiti wake na kuja na majibu ya masuala anayoyatilia mashaka.

..Mtoa mada aende bonde la mto Ruaha, afanye utafiti, na kutuletea taarifa ambazo anaamini ni sahihi kuhusu hali ya kimazingira ya eneo hilo.
 

..gharama za umeme wa Stieglers zitategemea aina ya MKOPO uliotumika kujenga mradi.

..kama tumechukua mkopo mbaya wenye masharti ya kibiashara basi tusitegemee gharama za umeme kuwa nafuu.
 
Wamelipiwa na serikali, kwani kuna tatizo hapo?
 
Mtoa mada ni mtetezi wa wale wahujumu 12.
 
Njoo na hoja nyingine kuhusu hoja ya kujaza maji kwenye bwawa. Kwa taarifa yako hata lile la Grand Ethiopian Renaissance Dame litajazwa kati ya miaka 4-7.

Soma hapa kwenye hiki chanzo

 
Spot on mkuu!
Kuna watu akili ni ndogo kubeba information, lazima waambiwe ili waweze kuelewa!
 
Tena tuna fail kipuuzi. Halafu haraka tunahadaiwa kuwa mabeberu ndo hawataki.... Unajiuliza wanafaidikaje na hali hii.... Hupati majibu. Toka miaka na miaka Wazungu ndo wamekuwa wabeba makosa yetu. Leo hii mtu hali vizuri anakosa nguvu za kiume au kuzalisha. Anasingizia wazungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…