Kongamano la Wahariri limeacha maswali mengi. Nani yuko nyuma?

🤣🤣🤣🤣🤣
Mkuu, ukweli ni kuwa kitu chochote kwa sasa kikihusisha tu wizara ya nishati ambako makamba yupo basi lazima uyasikie mengi sana mabaya.........watu watadadavua kinafiki, watamwaga hisia zao hasi, watu watapewa maneno ya wasiwasi a.k.a kuogofya hadi wakimbie. KATU HUTOSIKIA NENO LA MATUMAINI HATA MOJA. Hivyo ndivyo atendewavyo makamba; kuna dhamira ya wazi 'ya kumuua' ambayo hauhitaji hata kutumia darubini kuiona.

Tunazuiwa hata kusikiliza nini kizuri anasema; negative comments mwanzo mwisho......ukijifanya umesikia lolote zuri utatukaniwa hadi your great great grandparents. Siajabu, katika maswali yako haya, ukakutana na katusi huko mbele maana ni maswali yanayohitaji facts na sio longolongo.

Humu akitajwa tu makamba, unacholazimishwa kufanya ni kutaja wizi/madili (usiulize kaiba nini, lini, wapi na kivipi; utatukanwa); unalazimika kutaja biashara ya generators (ukiuliza kivipi utaambulia matusi au majibu yatakushangaza na kukuchekesha); utalazimika kumwita makamba mnafiki kwa hoja kuwa alilipinga bwawa akiwa waziri wa mazingira na sasa analisimamiaje? (Ukisema kuwa alikuwa anafanya kazi yake kwa kipindi hicho kutoa concerns za kimazingira km waziri wa mazingira.......na hii ni kama kweli aliwahi kulipinga. Na kiitifaki wazo lako linaposhindwa kufanya kazi basi hauna budi kuungana na kutekeleza wazo bora zaidi lililopita kitu am ambacho ndo anafanya; utaishia kutukanwa)
 
mimi pia nilijiuliza maswali mengi sana, ila ukweli utajulikana ngoja waje wajuzi wa mambo wasaidie uchambuzi huu mujarab. ila mtoa post nakupa kongole kwa uchambuzi makini sana. KINA BALILE, MCHANGE, KITENGE waje na maelezo
Kila ninaposikia "Mchange" nasikia kichefuchefu ... Nakumbuka jinsi alivyouza ubunge wake kwa Mzee Makamba sitakaa nisahau
 
huwa nikisoma mada za humu,nyingi ni lawama tu
 
We nawe neno iQ unalitumia vibaya sana . Yani utaje vilaza apa tena wanaongoza nchi iliyo jaa vilaza afu uwafanye kuwa na iyo IQ? Tafakar..!ila hoja unayo sema tumizi la Neno IQ ndio limeharibu
 
We kubali kwamba wenzio wanaanzia ulipoishia wewe kufikiri. Nothing more nothing less
 
Hivi na wewe unajiita mfikiriaji?!!!!!
Ulio wahofia kuja kumpinga uyo unaye mkingia kifua ndio wafikiriaji . Mimi ni kweli sio mfikiriaji ,kwani huwa hawampingi kwa hoja ?? Think big bro!
 
Ulio wahofia kuja kumpinga uyo unaye mkingia kifua ndio wafikiriaji . Mimi ni kweli sio mfikiriaji ,kwani huwa hawampingi kwa hoja ?? Think big bro!
Mimi niliwazungumzia ambao tayari walishampinga na mashaka yangu yalikuwa juu ya kukosekana kwa ushahidi wa wazi wa tuhuma kibao apewazo huyo jamaa.....wizi, uuzaji wa generators n.k sawa na maswali aliyouliza yule mdau niliyemquote. Au tukariri tu?!!! Mkisema mwizi basi tuitikie tu tawire. Jazia taarifa tuungane; tofauti na hapo itaonekana majungu tu.
 
Mkuu tatizo watu wanaongozwa na hisia sana, ukienda YouTube Ile video January anayotangaza Bwawa kujazwa Maji aisee hakuna pongezi ni lawama na matusi mpaka unashindwa kuelewa kwamba Bwawa likiisha shida, lisipoisha shida Sasa wanataka Nini?

Na ukiuliza aliiba Nini na wapi hakuna majibu, hivi kweli ulete mgao kuuza majenereta? Mgao kwa siku Moja tu unaleta hasara zaidi ya Billion 1 hayo majanereta utauza mangapi Hadi yakupe billion 1 Kila siku??

So weird.
 
🤣🤣 Mkuu tuvumiliane tuu
 
Wao wametumia akili ipi kuweza kupata hiyo advanced technology ambayo sisi inatushinda kuipata, au uwezo wetu wa kufikiri upo limited kiasi kwamba hatuwezi fanya innovation yoyote zaidi ya kutegemea innovation walizofanya wazungu ?
 
Ulio wahofia kuja kumpinga uyo unaye mkingia kifua ndio wafikiriaji . Mimi ni kweli sio mfikiriaji ,kwani huwa hawampingi kwa hoja ?? Think big bro!
Hakuna hoja ni speculations tu, walisema anahujumu Bwawa mbona Sasa analijaza Maji?

Walisema mgao kuuza majenereta mbona umepungua kama walivyoahidi before mwaka mpya sahivi upungufu ni chini ya 150 MW!!

Tukosoe watu kwa hoja sio speculations, mimi sipendi character assassinations bila facts. In fact umeme wa Tanzania unategemea GESI sio Maji so huwezi hujumu umeme bila kuhujumu Bomba la gesi au mitambo ya Kinyerezi pale.
 
Binafsi nimechagua kuwa mtazamaji wa hizi movie zinazoendelea ,Mkuu Bongo hii haijawahi ishiwa vihoja ..na mapicha picha 😂😂
 
Mleta hoja wewe ni mmoja wa wahujumu uchumi wetu kwa kuharibu mti Ruaha mkuu!
Kwani wewe umepata wapi uthubutu wa kuandika upuuzi huu ambao ni kero na kichefuchefu kwa mamilioni ya wa Tz?
 
mambo ni mengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…