Kongo (DRC) imeipiku Ethiopia na kuwa nchi ya tano kwa uchumi mkubwa zaidi barani Afrika.

Kongo (DRC) imeipiku Ethiopia na kuwa nchi ya tano kwa uchumi mkubwa zaidi barani Afrika.

Wamempa Marekani madini, halaf Marekani na yeye akawapa Congo uchumi wa kwenye makaratasi (paper Tiger) ili kuwahadaa na kuendelea kuwanyonya vizuri.

Wenye maono, na ujuzi wa mambo hatushangazwi Na hili.
I see
 
Kongo imeipiku Ethiopia na kuwa nchi ya tano kwa uchumi mkubwa barani Afrika kusini mwa jangwa la Sahara ambapo Afrika Kusini bado ndio inayoongoza kwa kuwa na uchumi mkubwa zaidi barani Afrika.

Katika muktadha huu haijulikani Tanzania ni ya ngapi lakini ni ukweli ulio wazi kwamba inazidiwa kabisa na majirani zake kama Kenya na hiyo Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na hii ni kwa mujibu wa shirika la fedha duniani.

Paper economy?...

Raia wa Drc watulie Sasa waache vita ili wanufaike na huu uchumi mkubwa...

Yoda zitto junior
 
Mzee kiingereza hujui au!Hii Jf ndio maana kila siku nasema inakosa credibility,hiyo link yako ukiisomabtu kwa nje unagundua inaongelea future sio present au huelewi kiingereza? Ukifungua link yako inasema The Democratic Republic of Congo is poised to overtake Ethiopia to become.... sentensi hiyo kwa kiswahili inamaanisha Drc inategemewa (ndani ya muda mchache ujao) kuipita Ethiopia na kuwa namba tano kwa uchumi kusini mwa jangwa la sahara..

Tatizo lako la kutokujua kiingereza lisikufanye ukawa na ubishi wa kijinga na wakati wenzio hiyo ndio field tuliyopo na wiki ya jana IMF imerelease data mpya za GDP PPP za mwaka
Sawa kwa mujibu wa IMF imeshathibitika kwamba kwa mwaka huu (2026) hiyo ndio itakua nafasi ya Congo kiuchumi sasa nilichokosea ni nini hapo.

"If there is a word in the heading that makes the context to be inconsistent with the article below it then it's just an oversight which is not uncommon in writing."
 
Wamempa Marekani madini, halaf Marekani na yeye akawapa Congo uchumi wa kwenye makaratasi (paper Tiger) ili kuwahadaa na kuendelea kuwanyonya vizuri.

Wenye maono, na ujuzi wa mambo hatushangazwi Na hili.
Hiyo taarifa ni ya IMF na wala si ya Marekani kama mnavyo karirishwa mara kwa mara na kama unaipinga basi tupe ya kwako iliyo sahihi na iambatane na uthibitisho na sio maneno ya vijiweni.
 
Takwimu ni za uongo na sababu kubwa ni DRC kuwa na mikataba na USA ya ulinzi ya hivi karibuni.
Hiyo 30b USD iliyoongezeka imetoka wapi ghafla hivyo kuipiku Ethiopia ?
Fuatila kwenye mtandao wa IMF usipinge tu wakati hauna taarifa mbadala.
 
Sawa kwa mujibu wa IMF imeshathibitika kwamba kwa mwaka huu (2026) hiyo ndio itakua nafasi ya Congo kiuchumi sasa nilichokosea ni nini hapo.

"If there is a word in the heading that makes the context to be inconsistent with the article below it then it's just an oversight which is not uncommon in writing."
Zingatia neno "ITAKUA"
 
IMF, and the like of WB zote ziko chini ya US kiutendaji so unaposema ni taarifa za IMF bado haina uhalisia ndani yake
Sio kweli kabisa, uliza vizuri IMF haipo chini ya Marekani na hivi vyombo vya kifedha duniani vinaongozwa kwa sera na haviongozwi kisiasa kwa matakwa ya nchi fulani na ikiwa hivyo wakuu wake wanajiuzulu kwani sio kama taasisi za kitanzania.
 
Sio kweli kabisa, uliza vizuri IMF haipo chini ya Marekani na hivi vyombo vya kifedha duniani vinaongozwa kwa sera na haviongozwi kisiasa kwa matakwa ya nchi fulani na ikiwa hivyo wakuu wake wanajiuzulu kwani sio kama taasisi
 
On paper ni kwle viko independent,ila kwenye uhalisia haiko hivyo,...For instance UN walikemea vikali Russia kuivamia Ukraine miaka 5 iliyopita,lakn umeshawahi kuisikia ikipinga waziwazi uvamizi wa US na washirika wake Mashariki ya kati tangu enzi za Persian Gulf,Iraq,hata sasa Iran?
 
Paper economy?...

Raia wa Drc watulie Sasa waache vita ili wanufaike na huu uchumi mkubwa...

Yoda zitto junior
Hoi takwimu ilinishangaza, uchumi wa mabilionea wachache unakuwa extrapolated kwa wananchi wote?

Itabidi nikasome vizuri methodology waliyotumia isije ikawa zile takwimu za nadharia kama thamani ya madini ardhini n.k
 
Back
Top Bottom