Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Uongozi, hufafanuliwa kama uwezo wa mtu binafsi, kikundi, au shirika wa kushawishi njia mbadala na si kufuata tu njia aliyoikuta hata kama njia hiyo inaelekea kuzimu.
Hatua ya Mbowe naye kutangaza kutetea nafasi yake, mimi naipongeza kwani itakiwezesha Chadema kuitafsiri falsafa yake ya kidemkrasia kwa tabia na vitendo.
Kujitosa kwa Mbowe katika kinyang'anyiro hicho kutatoa nafasi nzuri na adimu kwetu wapenda demokrasia kuupima ukomavu wa kisiasa ndani ya Chama hicho.
Pia tendo hili linafungua ukurasa mpya katika uendeshaji wa siasa nchini na kutoa funzo ambalo kwa hakika vyama vyote vya siasa nchini vinatakiwa kuiga mfano wake.
Nina hakika vipo, vyama vidogo na vikongwe, ambavyo Chadema wakifanikiwa kuendesha uchaguzi wake kwa ufanisi vinaweza kujikuta matatani na kuachwa kwenye mataa.
Demokrasia inatakiwa iheshimiwe, ilindwe na itetewe na wale wote wanaojipambanua kama wapenda demokrasia na chaguzi zozote zile ni lazima ziendeshwe kwa uhuru na haki.
Nawatakia wagombea wote wa nafasi ndani ya Chadema kila la heri na wawe tayari kukubali matokea na uchaguzi uitwe hivyo na si uchafuzi tunaoushuhudia wa walevi wa madaraka.