Kongole Chadema! Kiongozi ni yule anayejua njia, anaonyesha njia, kutengeneza njia pale hakuna njia!

Wanalia sana, kwanza wenyewe wanashangaa, tunawauliza zile kura 200 zilitokaka wapi, sitahudhiriia kwenye misiba hata furaha zao, ujinga wa mchengerwa umetuumiza wengi
 
Chama kikuu cha upinzani kufanya haya miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu ni kufeli, uwajibikaji lazima uwepo.
 
Kujitosa kwa Mbowe katika kinyang'anyiro hicho kutatoa nafasi nzuri na adimu kwetu wapenda demokrasia kuupima ukomavu wa kisiasa ndani ya Chama hicho.
Kwa bahati mbaya sana, tegemeo la aina hii ambalo sote tunge lifurahia sana, linaweza lisiwezekane kwa sababu mpangilio wa uvurugaji tayari umekwisha wekwa mahali pake.

Uchaguzi wa Mwenye kiti wa chama haufanywi na wanachama wote ndani ya chama. Hao wajumbe watakao kuwa na jukumu la kufanya kazi hiyo tayari wamekwisha wekwa kwenye mipango maalum kwa Mwenyekiti anaye maliza muda wake kupanga na kuandaa safu ya kuaminika kwake kwenye kanda zote ambako uchaguzi tayari umekamilika.

Tundu Lissu anaweza akawa na wana chama wengi; ambao hawata husika katika kumchagua Mwenyekiti wa chama. Hili linaweza kuwa tatizo tayari kwake.
Labda tuamini kwamba, maadam sasa kumekuwepo na hali mpya (Tundu Lissu kuwania) itegemewe kuwa hao wajumbe watakao husika kwenye uchaguzi huo wengi watabadili mwelekeo ulio kuwepo, kwa sababu ya haya mapya yaliyo ingia kwa uhusika wa Tundu Lissu kwenye kinyang'anyiro.
 
Nakusoma sana mkuu 'Erythro', na kuelewa kila unacho andika humu kwenye hizi siku za karibuni.
Kwa hilo neno moja Erythrocyte, ameonesha ukomavu kuliko ilivyotegemewa. Huo ukomavu wake umenizidishia imani kuwa Chadema ni zaidi ya wengi wanavyoifikiria.

Lissu hakukurupuka na nina imani Mbowe naye hatakurupuka kwani wote wanatambua Chadema ndio tumaini pekee lililobaki na litakalotuokoa mikononi mwa majangili tulio nao.

Kongole Chadema, kongole Mbowe na kongole Lissu, wananchi wako pamoja nanyi. Hivi sasa wako watu hawalali wakihangaika jinsi ya kujiokoa katika mikono yenu simba wawili wakali.

Tik tak, tik tak, tik tak...
 
Sasa hivi habari ni CDM
 
Sasa hivi habari ni CDM
Naam, habari ni Chadema. Hivi sasa Tanzania yaihitaji Chadema kuliko wakati wowote uliopita. Miaka zaidi ya nusu karne ni CCM, CCM...santuri hii imechacha na sasa inachosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…