DOKEZO Kongole kwa Serikali kwa kuondoa muingiliano wa kazi za TFDA na TBS, ikiwapendeza sasa muitazame RITA na NIDA

DOKEZO Kongole kwa Serikali kwa kuondoa muingiliano wa kazi za TFDA na TBS, ikiwapendeza sasa muitazame RITA na NIDA

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

deonova

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2013
Posts
742
Reaction score
419
Awali natoa pongezi kwa serikali kwa kuwasilisha bungeni muswada wa sheria ya kuyaondoa majukumu ya udhibiti ubora wa chakula na vipodozi kutoka TFDA na kuyahamishia TBS. Ni hatua nzuri ktk kuondoa muingiliano wa majukumu ya taasisi mbili (TFDA na TBS) pamoja na kupunguza mzigo wa tozo za ukaguzi kwa mfanyabiashara.

Sasa Serikali mkimalizana na hilo, ikiwapendeza, angalieni pia muingiliano wa RITA na NIDA (ktk baadhi ya majukumu). Ningependekeza jukumu la Usajili (registration) wa vifo na uzazi liondolewe kutoka RITA, lihamishiwe NIDA; ili sasa RITA ibaki na majukumu makuu mawili tu ya Ufilisi (Insolvency) na Udhamini (Trusteeship)

Naomba kuwasilisha

SOMA Serikali yaunganisha RITA na NIDA na Kufuta Mashirika mengine 20 ya Umma
 
NIDA na RITA ingeunganishwa kuwa moja tu

Kwa mtazamo wangu nadhani kuna baadhi ya kazi kama za Ufilisi na Udhamini ukizipeleka NIDA kama haitaendana flani hivi chief, ndo maana nimehisi kama kipengele kimoja tu cha Usajili (vifo na uzazi) ndo vipelekwe NIDA, halafu hivyo viwili vibaki RITA (tuondoe hii "R" Registration)
 
Hili suala bwana Mpango alilileta kama pendekezo kwenye hotuba ya bajeti 2019/2020, je katika kuyajadili mapendekezo yake waliafikiana vipi?
 
Na pia system za nida na uhamiaji ziunganishwe, maana mtu anakua na kitambukisho cha taifa ila bado uhamiaji hawaamini kama kweli ni mtanzania wanakwambia leta cheti cha kuzaliwa cha baba yako.
 
Habari Njema, umenikumbusha kauli mbiu ya Mh. Bashe juu ya uunganishwaji wa taasisi za serikali zenye kufanya majukumu yanayo karibiana sana, nakumbuka alizungumzia taasisi kama TIRDO, Brela, etc

Natumai utandaji kazi utaboreka zaidi
 
Wakati wananchi tunalia baadhi ya taasisi ziungane kupunguza gharama na matumizi serikalin,wao serikal wanazidi tu kujigawa..leo hii sumatra imegawanywa nakuunda taasisi mbil (tasac& latra)
 
Bara

Na TFDA wangeiunganisha na Baraza la Famasi (Pharmacy Council).
Hapana. Zisiunganishwe ila majukumu yanayofanywa na hizi taasisi kwa pamoja ndio yawekwe kwenye taasisi moja(TFDA au Pharmacy Council).

Hii hoja ya kuweka majukumu yaliyokuwa yanafanywa na taasisi zaidi ya moja kwenye taasisi moja, naiunga mkono. Ila siungi mkono mambo kufanywa kisiasa bila kitaalamu.

Kwa muda mrefu sana, taasisi mbalimbali za kitaaluma zimeanzishwa kwa kukopi kutoka kwa wenzetu walioendelea mfano US wana FDA (Food and Drugs Authority).

Ukiangalia majukumu ya FDA ni kudhibiti Chakula na Dawa, japo kina majukumu mengine mengi inayafanya, lengo ni kuimarisha afya ya binadamu ndio maana Chakula na dawa vipo sambamba.

Hapa kwetu wanataka kutenganisha Chakula na Dawa(vitu ambayo kwa pamoja ni kuhusu afya ya binadamu), sikubaliani. Mambo yote yanayohusiana na Afya ya binadamu viwe sehemu moja(yafanywe na taasisi moja).

Hapa lengo ni kurahisisha utoaji huduma kwa jamii jambo ambalo ni zuri wasiweke majukumu yanayoendana katika taasis tofauti.

Kuna suala la kusajili majengo(Premisses registration) ambalo linaelekezwa TBS na kuna suala la kibali cha biashara ( business permit) ambalo lipo TFDA, haya mambo yanatakiwa yakae sehemu moja(TFDA). Anayesajili majengo ya biashara ndio atoe na kibali cha biashara.

Pharmacy Council isichanganywe na taasisi nyingine bali majukumu ambayo ilikuwa inayafanya halafu yanafanywa na taasisi nyingine yahamishiwe ama Pharmacy Council au taasisi hiyo. Pharmacy Council iendelee kudhibiti taaluma ya Pharmacy na mambo yote yanayohusiana na taaluma.

Mambo yasifanywe kisiasa, itakuwa kla siku tunabadilishana sheria pasipo na kusonga kimaendeleo.
 
Tumekuwa tukilipigia kelele hili suala la kuwa na mashirika mengi yanayofanya kazi moja
 
Awali natoa pongezi kwa serikali kwa kuwasilisha bungeni muswada wa sheria ya kuyaondoa majukumu ya udhibiti ubora wa chakula na vipodozi kutoka TFDA na kuyahamishia TBS. Ni hatua nzuri ktk kuondoa muingiliano wa majukumu ya taasisi mbili (TFDA na TBS) pamoja na kupunguza mzigo wa tozo za ukaguzi kwa mfanyabiashara.

Sasa Serikali mkimalizana na hilo, ikiwapendeza, angalieni pia muingiliano wa RITA na NIDA (ktk baadhi ya majukumu). Ningependekeza jukumu la Usajili (registration) wa vifo na uzazi liondolewe kutoka RITA, lihamishiwe NIDA; ili sasa RITA ibaki na majukumu makuu mawili tu ya Ufilisi (Insolvency) na Udhamini (Trusteeship)

Naomba kuwasilisha
👂
 
Sasa wale watumishi wa TFDA sijui nao watawahamishia TBS?!!!.
Kwani mifuko ya kijamii ilipounganishwa wafanyakazi wa taasisi hizo walipelekwa/walibaki/walitawanywa wapi?

Hebu ulizia (wataalamu njooni) kwa wajuvi humu jamvini ili uni tag na mimi nipate mwanga/uelewa.
 
Tume ya maadili ya viongozi wa umma iungane na PCCB na polisi iungane na TISS maana majukumu yao yapo the same hili Mh.mtukufu rais aliangalie ili kupunguza bajeti zisizo na tija
 
Tume ya maadili ya viongozi wa umma iungane na PCCB na polisi iungane na TISS maana majukumu yao yapo the same hili Mh.mtukufu rais aliangalie ili kupunguza bajeti zisizo na tija

Hahaahaaaa.....hilo la Police kuungana na TISS gumu sana
 
Back
Top Bottom