beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
China iliahidi kuipatia Kenya vifaa mbalimbali vya Ofisini kama sehemu ya kuboresha urafiki wao. Ubalozi wa China nchini Kenya ulipewa taarifa kuwa vifaa hivyo vimetumwa kwa meli na vitawasili Julai 2019
Lakini katika hali isiyo ya kawaida Ubalozi wa China umeonesha kushangazwa baada ya kutaarifiwa na Bunge kuwa kontena lilipofika Bungeni Julai 30, 2019 na kufunguliwa lilikuwa halina kitu chochote ndani(tupu)
Ubalozi huo umebainisha kuwa hii na mara ya kwanza kwa kitendo kama hicho kutokea kwani kwa miaka kadhaa wamekuwa wakiwasaidia Wakenya vitu mbalimbali na vyote vimekuwa vikifika salama
Kutoka na suala hilo, Bunge limeitaarifu Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai na China inaamini kuwa litashughulikiwa na vifaa hivyo kupatikana bila wasi wasi huku wakisisitiza kuwa wataendelea kuisaidia Kenya