Korea Kaskazini imesema itatuma wanajeshi wake nchini Ukraine kuisaidia Urusi

Wanaenda kuliwa vichwa tu hao putini ashaulisha watu wengi sana kwa mtindo kama huu, Wagner leo wako wapi? vijana aliowaaajiri, wafungwa na sasa north korea na hata wanajeshi wa russia superpower anatapa tapa
 
Yaan mnyama hajaingia kwenye uwanja wa vita miaka yote 3 putini anaajiri vikosi kutoka North Korea..! nakubali sana Ukraine mziki mnene
 
Yaani Urusi isaidiwe? Hapana. Urusi ipo vizuri sana kijeshi. Haihitaji msaada.
Kila mtu na washirika wake,
USA alikua na Yuko na NATO.
USSR alikua na Warsaw Pact.
Sasa hivi Russia nae ana washirika wake.
Maisha ndivyo yalivyo.
Sio kwamba amezidiwa la ha Sha Bali ni washirika,kwa sababu Ukraine nae anasaidiwa na NATO
 
Kwanini Putin asi withdrawal na kurudi Moscow. Akubali tu kuishi vizuri na jirani yake mwenye uhuru kamili.
Kwa Nini Ukraine asikubali kuachana na mpango wake wa kutaka kujiunga na NATO?
Ambayo ni adui mkubwa wa Urusi ili aishi vizuri na jirani yake Urusi kwa amani na uhuru?
 
Urusi ndo wa kuomba jeshi kusaidiwa kupigana na ka nchi ka Ukraine?
Kwani kwa mujibu wa ranki zenu kati ya Urusi na Marekani ni nchi Gani Ina jeshi kubwa ,bajeti ya ulinzi silaha Bora na sifa nyingine nyingi?
Lakini mbona USA ana ombaga msaada wa nchi nyingine kwenda hata kupigana na watalaban TU?
Sasa kama USA ana omba msaada kwa NATO na washirika wengine kwa Nini Urusi nae asiombe msaada kwa marafiki zake kupigana na NATO ?
 
Hawa mashabiki wa USA na NATO bana,ni watu wa ajabu sana.
Wako kama USA yenyewe yaani ni unafiki TU kwa kwenda mbele.

Hebu fikiria.

Marekani kwenda kupigana na Iraq,Watalaban, Yugoslavia na Sasa kuisaidia Ukraine alikokota na amekokota nchi Dunia nzima pamoja na NATO yake ili zimsaidie.
Je huyu si hua tunaambiwa kua ndio jeshi namba moja duniani na Wana bajeti kubwa hata ziungane nchi zote duniani haziwezi kuifikia bajeti ya USA ?
Je kwa Nini asiende vitani peke yake?

Urusi tunaambiwa na haohao pro NATO kua ni nchi masikini na Ina jeshi dhaifu,je kama ni nchi masikini mbona akisaidiwa na marafiki zake TU mnaanza kupiga kelele?

Au mmesahau kua wakati wa USSR kulikua Kuna NATO na Warsaw Pact?

Sasa Kuna ubaya Gani Kila mtu kua na washirika wake?
Hofu ya Nini?
Au ndo manapenda vita nyepesi?
Kama NATO wameamua kuisaidia Ukraine basi Urusi nayo Ina haki ya kusaidiwa na marafiki zake.
 
Kwani nani kasema kuna ubaya kila mtu kuwa na washirika wake?

Au ni wewe ndio umefikiria halafu ukaota kwamba Pro NATO ndio wamesema?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…