Korea Kaskazini imesema itatuma wanajeshi wake nchini Ukraine kuisaidia Urusi

Yaani Urusi isaidiwe? Hapana. Urusi ipo vizuri sana kijeshi. Haihitaji msaada.
Ndiyo hivyo tena.

Mwenzako Putin alijiona mwamba sana akaanzisha special military operation ya wiki moja kudenazify na kudemilitarize Ukraine. Leo hii vita iko mwaka wa tatu akiwa keshapoteza zaidi ya vifaru zaidi ya 8,000, ndege za kivita zaidi ya 350, askari zaidi ya 500,000, meli za kivita zaidi 25. Siyo special military operation tena.

Sasa amaeamua kuomba msaada wa kijeshi kwa vikle amegundua hana ubavu wa kuanzisha vita ya wiki moja. Ana bahati sana republicans walizuia misaada ya silaha kwa Ukraine kwa zaidi ya miezi sita

 
Urusi kaanza kuchemka
 
Wazungu wa magharibi wanataka kuharibu mtiririko wa uchumi duniani baada ya kuona graph ya uchumi haipo upande wao kwahiyo wapo tayari dunia ianze upya
 
Sina Hakika na hizi taarifa...Maana zilianzishwa na South Korea ambao ni vibaraka wa US so inawezekana wanatumika kuropoka tu..Urusi ina watu mil 145 jeshi lao lina vifaa na zana nzito nzito wanazounda wenyewe haiwezi kuomna msaada huko Korea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…