Korea Kusini nchi yenye hifadhi kubwa ya silaha duniani wakataa kutoa silaha zaidi kwa Ukraine

Korea Kusini nchi yenye hifadhi kubwa ya silaha duniani wakataa kutoa silaha zaidi kwa Ukraine

Lakini taarifa za kijasusi zimedai kuwa Russia ambayo ni nchi rafiki wa Korea Kusini kupitia ushirikiano wa kijeshi na kiuchumi pamoja na Korea Kaskazini walifanya mazungumzo jna tangia hapo Korea Kusini hawajatuma tena silaha kwa Ukraine na hawatofanya hivyo
Utata huu .....una maana gani hapa ?
 
Nchi nyingi zilounda umoja wa nchi za kujihami wa NATO zimegundua kuwa zimeingizwa mkenge na Marekani kwa kuwepo katika misheni ambayo haijulikani mwisho wake. Kitendo cha nchi hizo ambazo nyingi ni zile zilojiunga juzijuzi na zilokuwa sehemu ya USSR zimejikuta katika wakari mgumu kwani zimeingia woga kuwa iko siku nazo zaweza kushambuliwa na Russia na hata Belarus.
Una uhakika na hili ? Yaani Poland, Baltic states zote zinaamini zimeingizwa mkenge na US na zinaogopa kuvamiwa na Urusi ?.......you are not serious

Kuundwa na BRICS na ukuaji wa wanachama wake ni tishio kubwa kwa ustawi wa bara la Ulaya na Marekani katika uimarishaji uchumi wake na mahusiano yake ya kimataifa kati yake na mabara mengine.
Maybe ?...
 
Katiba yao hairuhusu wao kupelekea silaha kwenye nchi zenye mgogoro, na ndiyo maana watapeleka artillery shells zaidi ya 500,000 kwa serikali ya Marekani, kisha Marekani atazipeleka Ukraine.
Wazungu hamuwajui.
 
Huna akili., Urusi anakuwaje mwamba?
Mwamba aliyeekwa kati ni kikundi kidogo cha Wagner ambacho alikitengeneza mwenyewe, wakachukua kituo cha jeshi Rostov bila kuua hata kuku? Putin akajificha chumba chini ya ardhi mpaka rais wa Belarus alipomuangukia Prigozhin putini akakubali masharti mbio mbio kwa usalama wake na udikteta wake., Madevdev alikimbia usiku ule ule na ndege akatokomea kusikojulikana

Unafkiri siku NATO wakiamua kutumia Jesho la nchi 32 duniani kuingia vitani na Putin inaweza chukua hata dakika 10 nchi iitwayo Russia haijapotea kwenye ramani ya dunia na kubaki vumbi tupu
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848] haya ni makopa[emoji175][emoji175]au mahaba??!!!!
 
Kuna baadhi ya Vijana ni wa hovyo aisee...!! Mungu lisaidie Taifa letu...hapo utakuta na akili hz uko ofisini fulani kama mtoa maamuzi na kuna watu wanakuita Boss!

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
Vijana wa hovyo zaidi katika taifa hili liliponga uvamizi wa Iddi Amini ni wanaoshangilia uvamizi wa nchi moja kwa nchi nyingine.
 
Kuna kitu flani nashindwa kuelewa, naomba nieleweshwe.
BRICS ni neno linalotokana na nchi tano wanachama, sasa hizi nchi zingine zinazoomba uanachama wakikubaliwa neno BRICS inavunjika na kuundwa neno lingine lenye maana na kuakisi jumuiya isiyotaja hizo nchi tano pekee?
 
Wanaweza kufanya hivyo au wakaweka BRICS & Alliances au wakabaki na neno hilo kama symbol tu ila yenye wanachama wengi zaidi au wakaja na jina ambalo litakuwa la kudumu hata mwanachama akiongezeka!Hilo tunabaki tunabashiri!
 
Na iwapo nchi za Ulaya pamoja na USA wakiomba kujiunga na BRICS wanaweza kukataliwa? Au kuna sehemu wamesema exactly nchi ambazo wanaruhusiwa kujiunga kwenye BRICS? Naomba kujua pia.
 
Na iwapo nchi za Ulaya pamoja na USA wakiomba kujiunga na BRICS wanaweza kukataliwa? Au kuna sehemu wamesema exactly nchi ambazo wanaruhusiwa kujiunga kwenye BRICS? Naomba kujua pia.
Mkuu kwenye hilo,hizo nchi zimeanzisha umoja huo kupunguza Dominance ya US hasa baada ya US kutumia dola kama silaha kuziadhibu nchi zilizo kinyume naye!Ukiangalia hata waanzilishi hao,unaona wazi kabisa hawana ndoa na US!
So kusema US au UK kujiunga BRICS ni suala lisilowezekana!Sijui kuhusu nchi nyingine za Ulaya!
 
Kwani mkuu, unafikiri US au UK wakituma maombi kujiunga na BRICS wanaweza kukataliwa kwasababu tu uanzilishi wa BRICS ilikuwa ni kuiondoa monopoly ya dola sokoni.
Ila sijui, kwani kukimbia tatizo ndo njia ya kutatua tatizo? Matumizi ya Dola nadhani ikikimbiwa na wengi na kuanzishwa kwa kitu kingine then tatizo lingine linaenda kuzaliwa tena...tena yawezekana ikawa kubwa zaidi kuliko kulikokimbiwa huku.
 
Kikubwa hapo kinachojaribu kutengenezwa ni balance of power!
Yaani unachosema ni sawa na Russia atume maombi kujiunga NATO!Huo utakuwa utani maana NATO iko zaidi kujikabili dhidi ya Russia!
 
Raisi wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol ameondoka nchini Ukraine kurudi Seul baada ya kufanya ziara ya kustukiza akitokea Vilnius nchini Lithuania.

Raisi huyo wa Korea Kusini alikuwa alihudhuria kikao cha NATO kilichokutana kujadili masuala mbaimbali likiwemo suala lla misaada zaidi kwa Ukraine ambayo iko vitani na Russia.

Akiwa mjini Kyiv raisi Yoon alikutana na raisi wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy na kumuahidi kumpatia msaada zaidi ingawa usio silaha kali (non-lethal weapons).

Korea Kusini imeahidi kuipatia Ukraine msaada kama mavazi ya kujilinda (Body Armour), vifaa vya kuondoa mabomu (Demining Devices) na kofia ngumu (Helmets) lakini si silaha na vifaa vingine vizito kama munitions na silaha zingine ndogondogo.

Korea Kusini ni nchi yenye hifadhi kubwa ya silaha duniani zingine tayari ikiwa ilikwishatoa huko nyuma kwa ombi la Marekani. Korea Kusini pia ni nchi ya tisa duniani kwa biashara ya silaha na mshirika wa karibu wa Marekani.

Itakumbukwa kuelekea mwishoni mwa mwaka jana raisi Joe Biden alifanya ziara nchini Korea Kusini na baada ya hapo nchi hiyo ikatuma shehena kadhaa ambazo kwa njia ya nyuma (Indirectly) zikaenda kwa Marekani ambapo nchi hiyo nayo ikapeleka mzigo huo nchini Poland ili Ukraine iweze kupewa mzigo huo.

Lakini taarifa za kijasusi zimedai kuwa Russia ambayo ni nchi rafiki wa Korea Kusini kupitia ushirikiano wa kijeshi na kiuchumi pamoja na Korea Kaskazini walifanya mazungumzo jna tangia hapo Korea Kusini hawajatuma tena silaha kwa Ukraine na hawatofanya hivyo. Hiyo ni kutokana na sheria na katiba ya nchi hiyo ambayo yakataza kutoa silaha katika sehemu zenye migogoro kama vita ya Ukraine.

Hata hivyo Korea Kusini imekuwa ikishiriki katika kampeni ya kuisaidia Ukraine ukiwemo msaada wa fedha zaidi ya Euro milioni 100 ambazo nchi hiyo iliipatia Ukraine na mapema mwaka huu ikatoa tena msaada wa Euro Milioni 150.

Pamoja na msaada huo wa fedha Korea Kusini imeshiriki kutengeneza vikwazo vya kiuchumi kwa Russia, kutoa kauli za kuilaumu Russia (rhetoric statements) na pia kusaidia teknolojia vita vya taarifa (technological information wars).

Taarifa hizo za kijasusi zimedai kuwa Korea Kusini safari hii wamekataa kutoa msaada wa kijeshi (vifaa vya kijeshi) kwa Ukraine kwa kuogopa kuharibu ushirikiano na Kremlin ambayo ni wa kihistoria na pia kuogopa kusababisha Kremlin kuipa nguvu zaidi Korea Kaskazini ambayo ni nchi yenye uhasama wa kihistoria na Korea Kusini.

Nchi nyingi zilounda umoja wa nchi za kujihami wa NATO zimegundua kuwa zimeingizwa mkenge na Marekani kwa kuwepo katika misheni ambayo haijulikani mwisho wake. Kitendo cha nchi hizo ambazo nyingi ni zile zilojiunga juzijuzi na zilokuwa sehemu ya USSR zimejikuta katika wakari mgumu kwani zimeingia woga kuwa iko siku nazo zaweza kushambuliwa na Russia na hata Belarus.

NATO haiwezi kuona ukweli kwamba katika karne hii ya 21 kuwa kwa kuifuata Marekani na sera zake za mambo ya nje ni kujitengenezea mazingira ya kuja kupqta shida siku za usoni.

Nchi kadhaa sasa hivi zaunda umoja wa BRICS, ambao ni muunganiko wa nchi za Brazil Russia India na China na ambao sasa hivi umoja huu wazidi kupata maombi ya uanachama kutoka katika nchi kadhaa kama Argentina, Iran, Saudi Arabia, South Africa, Egypt, United Arab Emitrates, Nigeria, Mexico na Algeria. Nchi zaidi zimeonyesha dhamira ya kujiunga na BRICS.

Mapema mwaka huu BRICS imetangaza kuwa nchi zipatazo 19 zimeomba kujiunga na BRICS zikiwemo Venezuela, Senegal, Uganda, ZImbabwe, Cuba, Angola, Gabon, Guinea Bissau, Honduras, Pakistan, Afghanistan, Belarus, Comoros, Syria, Sudan na Kazakhstan.

Pamoja na maazimio mengi yaliyomo katika uundwaji wa BRICS matumizi ya njia mpya za ubadilishanaji fedha ambazo zitatumika badala ya mfumo wa SWIFT. Mifumo hiyo ni ule wa CIPS (Cross-Border Inter-Bank Payment System wa China, SPFS(system for Transfers for Finanscial Systems) wa Russia, SFMS(Structured, FInancial Management System) wa India na mfumo wa Pix unotumiwa na benki kuu ya Brazil.

Kuundwa na BRICS na ukuaji wa wanachama wake ni tishio kubwa kwa ustawi wa bara la Ulaya na Marekani katika uimarishaji uchumi wake na mahusiano yake ya kimataifa kati yake na mabara mengine.

Vyanzo:

Reuters, NBC, Financial Times na kijarida cha Spytalk.
Umeandika vizuri lakini kuna Makosa muhimu (technical errors) kwenye bandiko lako. Habari yako inatakiwa asome mtu ambaye ni mjuvi wa mambo otherwise can swallow wrong information. Kijana wa leo atajua Russia na Korea Kusini ni marafiki , Korea Kusini ni Member wa NATO.
ALL IN ALL umeandika kitu muhimu sana hasa kwa zama hizi ambazo nchi za Ulaya zikipitia magumu kwa mgongo wa msaada kumbe ni misheni ya USA kupanua soko la siraha zinazotoka kwenye viwanda vyake.
 
Russia hana lolote huyo ni joka la kibisa tu, leo hii akipewa hata Poland tu anammaliza kama Ukraine tu mwaka wa pili amemshinda na hajui vita vitaisha lini yaani yuko gizani kabisa.
Hongera kwa kuchangia
 
Jipe moyo...anakuita.
Walimwambia kipofu Bathelomayo.
Maneno ya kwenye khanga kama haya huwa Urusi anayafumu kwa artillery vidogo dogo na akitokea muingreza au USA Mrusi hutumia Kynzal hypersonic missile na zile Strategic bombers like TUPOLEV 160 hazijaguswa bado huyo ndiye Mrusi taarabu peleka US
 
Utata huu .....una maana gani hapa ?
Mkuu, samahani ni typing error hii.

Russia ni rafiki wa chanda na pete wa Korea Kaskazini.

Hawa wakorea watuchanganya sana na mambo yao.
 
Una uhakika na hili ? Yaani Poland, Baltic states zote zinaamini zimeingizwa mkenge na US na zinaogopa kuvamiwa na Urusi ?.......you are not serious

Maybe ?...
Mkuu Russia ikishinda hii vita, usalama wa NATO countries utakuwa mashakani.
 
Umeandika vizuri lakini kuna Makosa muhimu (technical errors) kwenye bandiko lako. Habari yako inatakiwa asome mtu ambaye ni mjuvi wa mambo otherwise can swallow wrong information. Kijana wa leo atajua Russia na Korea Kusini ni marafiki , Korea Kusini ni Member wa NATO.
ALL IN ALL umeandika kitu muhimu sana hasa kwa zama hizi ambazo nchi za Ulaya zikipitia magumu kwa mgongo wa msaada kumbe ni misheni ya USA kupanua soko la siraha zinazotoka kwenye viwanda vyake.
Ahsante mkuu, "please accept my sincere apologies" hiyo ni typing error najitahidi kuwa na editor nzuri. Kwa urafiki ni Russia na Korea Kaskazini;.

Kuhusu Korea Kusini kuwa member ni kwamba hawa ni (Invited members).

Wanachama wa kukaribishwa wa NATO katika vikao vyao muhimu ni pamoja na Korea Kusini, Japan, Israel na nchi zingine zonijificha.

Hawa ndo wanoongoza kwa kusaidia NATO kuweka vikwazo vya kiuchumi kwa Russia na kusaidia mambo mengine muhimu.
 
Back
Top Bottom