Korea yaikopesha Tanzania Shilingi Bilioni 400 za kujenga Hospitali ya Rufaa Zanzibar

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2022
Posts
9,436
Reaction score
10,944
Exim Bank ya Korea imeikopesha Serikali ya Tanzania zaidi ya Bilioni 400 Kwa Ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kisasa na Chuo Cha Mafunzo(Mfano wa Muhimbili-Mlonganzila) Zanzibar.

---
Serikali ya Tanzania imepokea mkopo wa Dola za Marekani 163.6 milioni (Sh427.8 bilioni) kutoka Benki ya Exim ya Korea, kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Binguni Zanzibar pamoja na kituo cha mafunzo ya utabibu.

Mkataba wa mkopo huo umesainiwa leo Juni 5, 2024 kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Natu Mwamba na Mkurugenzi Mtendaji Mwandamizi wa Benki ya Exim ya Korea, Hwang Kiyeon na kushuhudiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais wa Zanzibar, Fedha na Mipango, Dk Saada Mkuya.

Mkataba huo wa mkopo umetiwa saini wakati Rais Samia Suluhu Hassan akiendelea na ziara yake ya siku sita nchini Korea.

Chanzo: Mwananchi

My Take
Tunawashukuru watu wa Korea. Mcheza kwao hutunzwa, turudi nyumbani kumenoga.

Pia soma RC Chalamila: Hospitali ya Muhimbili itabomolewa yote na kujengwa upya kwa msaada wa Korea Kusini alipokwenda Rais Samia

Pia someni hapa Tanzania Kushirikiana na Korea Kusini Kujenga Bandari ya Uvuvi Bagamoyo. Itagharimu Bilioni 400

Pia, Soma=> Ufaransa yaipa Tanzania mkopo wa Tsh. Bilioni 361.7 kuzalisha umeme wa jua
 
Kwani huduma za afya ni mambo ya Kimuungano?

Yaani tunakopa Tanzania Bara halafu Hospitali inaenda kujengwa Zanzibar?

Deni tunakuja kulipa Tanzania Bara 🙆

It's unfair aisee 🙌
 
Yaani Zanzibar wanashindwa kujenga hospital ya bilioni 400 mpaka wapate mkopo ?

Na mpo hapa kusifia bila aibu!

Wao hawajali kwa kuwa huo Mkopo unalipwa na utalipwa na Watanganyika ....!!

Imagine Afya si swala la Muungano ... sijui inakuwaje serikali ya Muungano inakopa kwenda kujenga Hospital Zanzibar. Kweli Wajinga ndiyo waliwao.
 
Mama akichukua mkopo kwenye kikoba, baba ndiye hupata mateso ya kulipa deni. Mbaya zaidi mama akope alafu tusile ata nyama kumbe amekopa kwa ajili ya kuhudumia mchepuko aliye chini ya kivuli cha shemeji! Bado sijaona sijaona🎵🎶🎵🎶
 
Ni mpaka pale Tanganyika itakapoacha kujivika koti la Tanzania na kuchukua koti lake la utanganyika.Vinginevyo cha Tanzania ni cha wote Tangnyika na Zanzibar .Tatizo ni watanganyika wenyewe kuikataa Tanganyika yao.
 
Exim Bank ya Korea imeikopesha Serikali ya Tanzania zaidi ya Bilioni 400 Kwa Ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kisasa na Chuo Cha Mafunzo(Mfano wa Muhimbili-Mlonganzila) Zanzibar.
Korea inapaswa kuikopesha Zanzibar na sio Tanzania, hawa waswahili wa Zanzibar bwana, inapokuja ishu ya kugawana fedha wanataka tugawane nusu kwa nusu, linapokuja suala la mikopo wanataka mkopo mkubwa kwa vitu vidogo, linopokuja suala la kulipa wanataka Tanzania ilipe 100% na bado hawaendelei!!!
 
Exim Bank ya Korea imeikopesha Serikali ya Tanzania zaidi ya Bilioni 400 Kwa Ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kisasa na Chuo Cha Mafunzo(Mfano wa Muhimbili-Mlonganzila) Zanzibar.

---
Serikali ya Tanzania imepokea mkopo wa Dola za Marekani 163.6 milioni (Sh427.8 bilioni) kutoka Benki ya Exim ya Korea, kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Binguni Zanzibar pamoja na kituo cha mafunzo ya utabibu.

Mkataba wa mkopo huo umesainiwa leo Juni 5, 2024 kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Natu Mwamba na Mkurugenzi Mtendaji Mwandamizi wa Benki ya Exim ya Korea, Hwang Kiyeon na kushuhudiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais wa Zanzibar, Fedha na Mipango, Dk Saada Mkuya.

Mkataba huo wa mkopo umetiwa saini wakati Rais Samia Suluhu Hassan akiendelea na ziara yake ya siku sita nchini Korea.

Chanzo: Mwananchi

My Take
Tunawashukuru watu wa Korea. Mcheza kwao hutunzwa, turudi nyumbani kumenoga.

Pia soma RC Chalamila: Hospitali ya Muhimbili itabomolewa yote na kujengwa upya kwa msaada wa Korea Kusini alipokwenda Rais Samia
UCHAGUZI UNAKARIBIA
 
Korea inapaswa kuikopesha Zanzibar na sio Tanzania, hawa waswahili wa Zanzibar bwana, inapokuja ishu ya kugawana fedha wanataka tugawane nusu kwa nusu, linapokuja suala la mikopo wanataka mkopo mkubwa kwa vitu vidogo, linopokuja suala la kulipa wanataka Tanzania ilipe 100% na bado hawaendelei!!!
Zanzibar hairuhusiwi kukopa labda Kwa kibali Cha Tanzania
 
Back
Top Bottom