Korea yaikopesha Tanzania Shilingi Bilioni 400 za kujenga Hospitali ya Rufaa Zanzibar

Haya kuna thread yenu kule kujenga tawi la chuo kikuu cha dar es salaam chato watu kelelee nyingiii huku napo kelele za nini?

Mi nishasema sisi hatujui hadi sasa nini tunahitaji na itakuwa ndiyo hivi hivi hadi mwisho.
 
Na Korea inawajengea AICC au JNICC yao....mikutano yote mikubwa ya kimataifa itakuwa inafanyika Zanzibar...
Na Wakorea wanajenga bandari kubwa ya mafuta, gesi, uvuvi na makontena.... Zanzibar itakuwa kituo kikubwa cha utalii na usafirishaji wa baharini.
 
Exim Bank ya Korea imeikopesha Serikali ya Tanzania zaidi ya Bilioni 400 Kwa Ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kisasa na Chuo Cha Mafunzo(Mfano wa Muhimbili-Mlonganzila) Zanzibar.

---
Serikali ya Tanzania imepokea mkopo wa Dola za Marekani 163.6 milioni (Sh427.8 bilioni) kutoka Benki ya Exim ya Korea, kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Binguni Zanzibar pamoja na kituo cha mafunzo ya utabibu.

Mkataba wa mkopo huo umesainiwa leo Juni 5, 2024 kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Natu Mwamba na Mkurugenzi Mtendaji Mwandamizi wa Benki ya Exim ya Korea, Hwang Kiyeon na kushuhudiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais wa Zanzibar, Fedha na Mipango, Dk Saada Mkuya.

Mkataba huo wa mkopo umetiwa saini wakati Rais Samia Suluhu Hassan akiendelea na ziara yake ya siku sita nchini Korea.

Chanzo: Mwananchi

My Take
Tunawashukuru watu wa Korea. Mcheza kwao hutunzwa, turudi nyumbani kumenoga.

Pia soma RC Chalamila: Hospitali ya Muhimbili itabomolewa yote na kujengwa upya kwa msaada wa Korea Kusini alipokwenda Rais Samia

Pia someni hapa Tanzania Kushirikiana na Korea Kusini Kujenga Bandari ya Uvuvi Bagamoyo. Itagharimu Bilioni 400
Naomba kueleweshwa kwa anaeelewa.

Hivi mambo ya afya ni jambo la muungano au sio.
 
Huyu Abdul anaikopea Zanzibar ili Tanganyika tulipe deni lao
 
Back
Top Bottom