Exim Bank ya Korea imeikopesha Serikali ya Tanzania zaidi ya Bilioni 400 Kwa Ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kisasa na Chuo Cha Mafunzo(Mfano wa Muhimbili-Mlonganzila) Zanzibar.
---
Serikali ya Tanzania imepokea mkopo wa Dola za Marekani 163.6 milioni (Sh427.8 bilioni) kutoka Benki ya Exim ya Korea, kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Binguni Zanzibar pamoja na kituo cha mafunzo ya utabibu.
Mkataba wa mkopo huo umesainiwa leo Juni 5, 2024 kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Natu Mwamba na Mkurugenzi Mtendaji Mwandamizi wa Benki ya Exim ya Korea, Hwang Kiyeon na kushuhudiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais wa Zanzibar, Fedha na Mipango, Dk Saada Mkuya.
Mkataba huo wa mkopo umetiwa saini wakati Rais Samia Suluhu Hassan akiendelea na ziara yake ya siku sita nchini Korea.
Chanzo: Mwananchi
My Take
Tunawashukuru watu wa Korea. Mcheza kwao hutunzwa, turudi nyumbani kumenoga.
Pia soma
RC Chalamila: Hospitali ya Muhimbili itabomolewa yote na kujengwa upya kwa msaada wa Korea Kusini alipokwenda Rais Samia
Pia someni hapa
Tanzania Kushirikiana na Korea Kusini Kujenga Bandari ya Uvuvi Bagamoyo. Itagharimu Bilioni 400