Korea yaikopesha Tanzania Shilingi Bilioni 400 za kujenga Hospitali ya Rufaa Zanzibar

Korea yaikopesha Tanzania Shilingi Bilioni 400 za kujenga Hospitali ya Rufaa Zanzibar

Kwani huduma za afya ni mambo ya Kimuungano?
Hapana.
Afya siyo suala la muungano ndiyo sababu Znz wana wizara yao ya Afya.

Yaani tunakopa Tanzania Bara halafu Hospitali inaenda kujengwa Zanzibar?

Deni tunakuja kulipa Tanzania Bara 🙆

It's unfair aisee 🙌
Duh,
Ajabu sana.
Awamu hii Tanganyika itakamuliwa hadi damu
 
Wao hawajali kwa kuwa huo Mkopo unalipwa na utalipwa na Watanganyika ....!!

Imagine Afya si swala la Muungano ... sijui inakuwaje serikali ya Muungano inakopa kwenda kujenga Hospital Zanzibar. Kweli Wajinga ndiyo waliwao.
Kwa sasa wao Znz wameshika mpini, maana wanamiliki serikali zote mbili
 
Ni mpaka pale Tanganyika itakapoacha kujivika koti la Tanzania na kuchukua koti lake la utanganyika.Vinginevyo cha Tanzania ni cha wote Tangnyika na Zanzibar .Tatizo ni watanganyika wenyewe kuikataa Tanganyika yao.
Fact bigup
 
Na Korea inawajengea AICC au JNICC yao....mikutano yote mikubwa ya kimataifa itakuwa inafanyika Zanzibar...
Na Wakorea wanajenga bandari kubwa ya mafuta, gesi, uvuvi na makontena.... Zanzibar itakuwa kituo kikubwa cha utalii na usafirishaji wa baharini.
Ila wanafanya ujenzi wote huo kwa mikopo itakayolipwa na Tanganyika pekee
 
Vyanzo vya mapato vya sm ni vipi, maana mambo ya nje ni muungano so mikopo ni mambo ya nje...

Huu muungano umekaa vibaya
Hiyo ndiyo point. Muungano umekaa vibaya. Pia inayokopa siyo Wizara ya nje na wala mkopo haupitii hiyo Wizara. Sijui ni kwa nini Mzee wa TRAT and TRA aliachwa kwenye hili deal. Inawezekana ikawa ndiyo mwanzo wa mwisho wake Serikalini. Nguvu ya January ni kubwa mno.
 
Kwani bajeti ya Zanzibar kwa mwaka ni kiasi gani?
Bajeti yao ni around Trilion 2 na nukta.

Ilhali bado iko supplemented na mapato toka bara..

A lot of exemptions wanapewa.

Deni la umeme walisamehewa na mengineyo mengi.

Mkopo unalipwa na watu wa bara ila wazanzibar it's just a walk in the park.
 
Tanganyika inaonewa sana na viongozi wake ni kama hawasikii wala kuyaona.
 
Back
Top Bottom