Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Fedha zimekopwa na Zanzibar kwa jina la Tanzania ndiyo maana Saada Mkuya yupo na inakwenda kujenga Hospitali Zanzibar.Hii ni sawa, pesa imekopwa na muungano sio Tanganyika, na kwa vile TRA kuna Kodi inakusanya Zenj na kuziweka hazina BOT dar, hii ni sawa tu
Hakuna fedha kutoka TRA inayovuka bahari hata senti tano! kama ipo tuambie mwaka 2023/2024 kiasi gani kililetwa
Katika Takwimu za kila robo mwaka za BoT lini uliona mapato ya Zanzibar.
Hizi fedha zimekopwa ili kujenga Hospitali kwa ajili ya AFCON. Moja ya masharti ni kuwa na Hopsitali katika viwango vya Kimataifa. Ile ya V.I. Lenini au Mnazi mmoja ipo chini ya kiwango ndio maana inajengwa hii ya rufaa
Hakuna tatizo Zanzibar kukopa, kuna tatizo moja hakuna anayejua mkopo wa Zanzibar unalipwaje.
Ukisoma Bajeti ya SMZ hakuna sehemu ya malipo ya mikopo!
Kwa maneno mengine Tanganyika kwa jina la Tanzania ndiyo italipa katika mtindo ule ule wa madeni ya Umeme
Zanzibar wanataka kila formula ya kugawana nafasi za ajira, misaada , mikopo . Hutawasikia wakitoa formula ya kuchangia muungano au formula ya kulipa madeni!
Hili deni mtalipa Watanganyika kwa jina la Tanzania! ndio msemo wao siku hizi, kila Mzanzibar ni Mtanzania lakini si kila Mtanzania ni Mzanzibar!