Korogwe: Bodaboda wadaiwa kuchoma basi la Saibaba baada ya mwenzao kugongwa

Korogwe: Bodaboda wadaiwa kuchoma basi la Saibaba baada ya mwenzao kugongwa

Nawakubali sana wanangu wa boda wana umoja na uthubutu kuliko wasomi wetu siku wa kiamka hawa ndio tutapata mapinduzi ya kweli.

Kuna siku mwanajeshi aligonga mwanafunzi halafu hakisimama wakamfukizia mpaka akasimamisha gari wakaenda nae kituo cha police wana mapungufu yao ila ni watu ambao poa sana wana umoja sana.
Asilimia 99 ni wapumbavu wasiojitambua
 
Yule aliyosema bodaboda ni LAANA naanza kumuelewa.
Kwa hapa DAR sijaona sehemu yenye shida kuendesha gari kama hii barabara ya kutoka mbagala - chamazi kama wewe ni dereva ebu njoo kwenye hii barabara hakika unaweza kupaki gari pembeni ili bodaboda wapite
Hawa dawa yao ukiona anakufata pembeni we mzibie tu njia atadondoka mwenyewe
 
Habari zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa kundi la waendesha bodaboda, leo Februari 27, 2024 wamelichoma moto na kuliteketeza basi linalodaiwa kuwa ni mali ya Kampuni ya Saibaba, lililokuwa linatoka jijini Dar es Salaam kuelekea Arusha, baada ya kudaiwa kumgonga bodaboda mmoja na kusababisha kifo chake.

Habari zilizotufikia hivi punde, zimeeleza kuwa tukio hilo limetokea katika eneo la Kona ya Semkiwa, Korogwe mkoani Tanga na kusababisha kukatika kwa mawasiliano kati ya pande mbili za barabara hiyo, jambo lililosababisha foleni iliyodumu kwa takribani saa mbili.

Kwa mujibu wa mashuhuda, baada ya ajali iliyosababisha kifo cha mwendesha bodaboda, wenzake walijikusanya na kulizingira basi hilo, wakawaamuru abiria wote kushuka na kushusha mizigo yao kabla ya kuliteketeza kwa moto.

Kwa hizi picha zilizoambatanishwa basi lipo kwenye sait yake kabisa hivyo makosa yake hayapo wazi ....japo yaweza kuwa Boda kachomekea basi na dereva wa basi hakupunguza kumsaidia apite???
 
Wengi ktk huu uzi wanamuhukumu bodaboda,ukweli jamaa wapo rough lakini sometimes huwa wanapelekewa chuma.

Jana nilimsikia shuhuda mmoja aliyejitambulisha kama mkata mkaa akihojiwa na radio za huku Kaskazini akasema bus ali-over take mwanzo wa kona (nikiangalia video kweli kule nyuma kuna corner inaonekana) wakati anamaliza akakutana na boda akampiga pikipiki ikaingia chini ya bas so hapo kuna mawili kosa ni la dereva na dereva alitaka kukimbia kilichomzuia ni pikipiki kuingia kwenye chassis.

Kwa mtu anayezijua kona za Msambiazi hakuna asiyejua tabia za madereva wa malori na mabasi wanapokuwa maeneo yale.
 
Duuuuhhhh
Ilikuwa one day mpemba/mwarabu alimgonga bodaboda wa hapo , boda wakapiga kiberiti li v8 lake.
Mpemba/mwarabu akapiga Albadri, sasa sijui alipiga yeye mwenyewe au alimtafuta fundi wa hiyo kazi.
Maana unaweza kuwa umesoma Quran lakini usiweze kuipiga hiyo kitu ikaleta matunda.
Basi kila aliyehusika kuchoma ile gari alipukutika
Kijiwe chote kikapukutika walisalimika ambao hawakuwepo kipindi cha tukio tu.
Albadri sio mchezo.
Mzee wangu anaweza kuipiga hata usingizini .
Kilwa ilipigwa hiyo kitu na sheikh mmoja hivi iliua aliyeangua nazi, aliyefua, aliyepikia, aliyekula bila kujali hakutenda kosa.
So far mpaka vyombo vilivyotumika kupikia viliungua mpaka jiti lililotumika kufua nazi liliungua
Shehe ilikuaje hapo manake ni nyumbani kabsa ndo maana kuna bodaboda wengne maarufu hawapo tena
 
Kwa hizi picha zilizoambatanishwa basi lipo kwenye sait yake kabisa hivyo makosa yake hayapo wazi ....japo yaweza kuwa Boda kachomekea basi na dereva wa basi hakupunguza kumsaidia apite???
Shuhuda aliyeshuhudia alisema jamaa wa bus alimgongea boda nyuma kule kwenye corner inayoonekana baada ya ku-overtake akakutana nae akamzoa.

Hapo bus alitaka kukimbia tukisema ajali ilitokea hapo kwenye tambalale tutakuwa tunajidanganya kwamba pikipiki Haujue ilitaka kucheza chicken sport na Scania tena Marcopolo kitu ambacho hakiwezekani.
 
Hawajui Bima wanalipa ila roho ya aliyekufa hairudi?

Inatakiwa ioneshwe mfano kwa kurekodiwa kisha wapigwe miaka 30 kutokana na arson
Hapo hamna case,

Wananchi wenye hasira Kali hawajawahi kushtakiwa na kupatikana na HATIA kokote duniani.

Muhimu ni mabasi waheshimu uhai, na voda wafuate SHERIA.
 
Wanajua bei ya Scania hao nguruwe kwa Kisambaa?
Kwanini mafukara mna chuki sana na matajiri?
Yaani uhai wa boda uliopotea Bure Hauna thamani kama scania?

Hili ni funzo Kwa madreva wa maroli na mabasi kuthamini uhai, pia boda waongeze Umaskini na kuacha Rafu barabarani.
 
Huo ni unyasaji wa kijinsia hata km umegongwa Sawa lakini haikufaa kufanya Jambo km hilo wanakuaje km vichaa namna hio unachomaje Gari unajua gharama yake wewe?

Hio clip ionyeshe pia waliofanya tukio hilo alafu Jeshi la Polisi lidili nao hao vichaa waliojificha kwenye kichaka cha ubodaboda
Ndugu mropokaji unajua thamani ya uhai wa mtu kulinganisha na hilo lichuma. Naamini huna hata baskeli zaidi ya masufuria ndani kwako ,lasivo ungewajua dereva wa mabasi walivyo mbwa .
 
Safi sana. Juzi nikiwa stendi ndani , alikuja dereva n'a basi lake alitaka kuniua. Imagine gari kilo ndani ya stendi Tena ametoka kuosha gari anarudi kupaki stendi lakini jamaa anakimbiza gari utadhani anaenda mkoani. Ilibasi sentimika chache anikanyage bila sababu, bahati nzuri niliruka sana. Raia walimzinguka akidhani labda amepata kichaa. Next time wale na dereva .
 
Na hivi hai boda hawana ekimu yoyote juu ya sheria za usalama barabarani ni tatizo kubwa. Je walujua nani mwenye kosa?
 
Ndugu mropokaji unajua thamani ya uhai wa mtu kulinganisha na hilo lichuma. Naamini huna hata baskeli zaidi ya masufuria ndani kwako ,lasivo ungewajua dereva wa mabasi walivyo mbwa .
Washadakwa wote waliohusika na wanafikishwa mahakamani nyuma ya nondo panawahusu hasira za kisengerema zinaenda kuwafanya wakale maharage ya Jela, wapo 13 na wote wapo rupanga mda huu
 
Safi sana. Juzi nikiwa stendi ndani , alikuja dereva n'a basi lake alitaka kuniua. Imagine gari kilo ndani ya stendi Tena ametoka kuosha gari anarudi kupaki stendi lakini jamaa anakimbiza gari utadhani anaenda mkoani. Ilibasi sentimika chache anikanyage bila sababu, bahati nzuri niliruka sana. Raia walimzinguka akidhani labda amepata kichaa. Next time wale na dereva .
Sheria Kali zingetungwa kwa bodaboda maana nao wanagonga wanaua wanasababisha ulemavu wa watu

Sheria Kali zingetungwa kwa wenye kuendesha Bajaj maana nao wanagonga wanaua wanasababisha ulemavu

Sheria Kali zingetungwa kwa madereva wa mabus na madereva wa malori ya mizigo wanaua tena hawa ndio vinara wanajeruhi na kusababisha ulemavu wa kudumu

Sheria hio sio nyingine ikibanika bodaboda, Bajaj au dereva wa Lori la Mizigo au bus la abiria akibainika ameua kwa uzembe Sheria iwe na yeye anyongwe mpaka kufa au afungwe Maisha Jela,

Kwa Sheria hio nadhani hawa madereva wote wataacha kuua abiria na wataheshimiana wao kwa wao maana wanajua nikiua naenda kuishi Maisha yangu yote Jela

Maana hii Sheria ya sasa wanaidharau maana akiua hata watu 100 Sheria inasema apokonywe leseni kisha itafungiwa kwa Muda fulani alafu akishafikishwa mahakamani na ikibainika kweli amesababisha ajali hio na kuua watu aidha atafungwa miezi 6/12 pamoja na faini au ataambiwa alipe faini kisha ataachiwa kwenda kusubiri kifungo cha leseni yàke kiishe kisha ataenda kuchukua leseni na kuendelea kuingia barabarani na kuua tena watu wengine

Sheria hio inabidi ibadirishwe dereva akiua basi moja kwa moja Jela akanyongwe au akafungwe Maisha,
 
Shuhuda aliyeshuhudia alisema jamaa wa bus alimgongea boda nyuma kule kwenye corner inayoonekana baada ya ku-overtake akakutana nae akamzoa.

Hapo bus alitaka kukimbia tukisema ajali ilitokea hapo kwenye tambalale tutakuwa tunajidanganya kwamba pikipiki Haujue ilitaka kucheza chicken sport na Scania tena Marcopolo kitu ambacho hakiwezekani.
Hio njia napita sana bodaboda na Bajaj wa Msambiazi huwa wanaendesha pembeni,nje kabisa kwa pedestrian, hata ukiovateki wanakuwa nje. Ni wazi bus lilitoka nje kwenye kona ndio akamgonga na kuamsha hasira za wenzie.
Siafiki kuchoma bus,ila wenye buses ni wauaji kama wewe ni muendeshaji highway na una gari ndogo utanielewa.
 
Sheria Kali zingetungwa kwa bodaboda maana nao wanagonga wanaua wanasababisha ulemavu wa watu

Sheria Kali zingetungwa kwa wenye kuendesha Bajaj maana nao wanagonga wanaua wanasababisha ulemavu

Sheria Kali zingetungwa kwa madereva wa mabus na madereva wa malori ya mizigo wanaua tena hawa ndio vinara wanajeruhi na kusababisha ulemavu wa kudumu

Sheria hio sio nyingine ikibanika bodaboda, Bajaj au dereva wa Lori la Mizigo au bus la abiria akibainika ameua kwa uzembe Sheria iwe na yeye anyongwe mpaka kufa au afungwe Maisha Jela,

Kwa Sheria hio nadhani hawa madereva wote wataacha kuua abiria na wataheshimiana wao kwa wao maana wanajua nikiua naenda kuishi Maisha yangu yote Jela

Maana hii Sheria ya sasa wanaidharau maana akiua hata watu 100 Sheria inasema apokonywe leseni kisha itafungiwa kwa Muda fulani alafu akishafikishwa mahakamani na ikibainika kweli amesababisha ajali hio na kuua watu aidha atafungwa miezi 6/12 pamoja na faini au ataambiwa alipe faini kisha ataachiwa kwenda kusubiri kifungo cha leseni yàke kiishe kisha ataenda kuchukua leseni na kuendelea kuingia barabarani na kuua tena watu wengine

Sheria hio inabidi ibadirishwe dereva akiua basi moja kwa moja Jela akanyongwe au akafungwe Maisha,
Mkuu em tuambie kiwango chako cha elimu kwanza na tuambie nini unachojua kuhusu traffic accidents
 
Back
Top Bottom