Korogwe: Bodaboda wadaiwa kuchoma basi la Saibaba baada ya mwenzao kugongwa

Korogwe: Bodaboda wadaiwa kuchoma basi la Saibaba baada ya mwenzao kugongwa

Nawakubali sana wanangu wa boda wana umoja na uthubutu kuliko wasomi wetu siku wa kiamka hawa ndio tutapata mapinduzi ya kweli.

Kuna siku mwanajeshi aligonga mwanafunzi halafu hakisimama wakamfukizia mpaka akasimamisha gari wakaenda nae kituo cha police wana mapungufu yao ila ni watu ambao poa sana wana umoja sana.
Siwaamini hawa watu,nimeshaona wanaua watu wasio na hatia kupitia umoja wao kipuuzi kwa mambo ya barabaran tu tena mara nyingi wao ndo wenye shida.
 
Kuna wanaomuita Lema ni nabii. Sasa tunaona kile alichokiita 'laana'!
Kwa sasa kunguni wanajificha jua limetoka wanaogopa kuonwa na binadamu, ila ingekuwa upande mwingine wasinge ogopa hata jua la saa saba!.
 
Nawalaani kwa nguvu zote waliohalalisha pikipiki kubeba abiria, nawalaani askari wa usalama barabarani kwa kutofuatilia na kuangalia mwenendo wa bodaboda hapa nchni, nawalaani wanasiasa wote hasa wa ccm kuwatumia bodaboda kisiasa. Majanga wanaosababisha bodaboda na hayaripotiwi Au kuupuuziwa na mamlaka ni makubwa mno
Laana hiyo inatokana na kwamba una Hela na uwezo wa kigari
 
Basi la Kampuni ya Sai Baba linalofanya Safari kutoka Dar es Salaam kuelekea Mkoani Arusha limeteketezwa kwa Moto mara baada ya kusababisha Ajali kwa kumgonga Dereva wa Bodaboda na kudaiwa kusababisha kifo kwa dereva huyo wa Bodaboda katika eneo la Msambiazi wilayani Korogwe mkoani Tanga leo Februari 27, 2024.

Waendesha Pikipiki (Bodaboda) katika eneo hilo wamejichukulia sheria mkononi mara baada ya kushuhudia ajali hiyo ikitokea kwa kulichoma basi hilo moto kwa kutumia mafuta ya Petroli.

View attachment 2918376View attachment 2918378View attachment 2918377
Wasambaa na wadigo wana roho ngumu na mbaya na isiyo na huruma kama akina nanii wanaochinja watu huku wakimuita mtu wanayesema ni "mungu"

Ukipata ajali hapo wanakuja kukumalizia na kukuibia.
Ukiharibikiwa gari wanatamani ufe wakuibie.
ajali ikitokea wanavua maiti nguo na hata nguo za ndani.
 
Imagine tungekuwa tunaishi bila sheria maisha yangekuwaje
Wewe muendesha gari je kungekuwa hakuna sheria zinazokubana mambo yangekuwaje
Hivi unaweza kuvumilia foleni na wakati unaweza kuchepuka ukatokea mbele na ukaendelea na safari bila shida yoyote?
Boda wako sahihi
Unajua kuwa foleni nyingi sababu ni kukosa ustaarabu kwa madereva?
Hivi unajua magari ya viongozi na serikali yako rafu barabarani kuliko hao boda
Aiseeee hawa madereva wa serikali na bodaboda hawana tofauti kabisaa!!! Upo Sahihi Kwa upande Fulani Ila hawa bodaboda lazima serikali ifanye Jambo Fulani la Sheria Kwa hawa jamaa
 
Nawakubali sana wanangu wa boda wana umoja na uthubutu kuliko wasomi wetu siku wa kiamka hawa ndio tutapata mapinduzi ya kweli.

Kuna siku mwanajeshi aligonga mwanafunzi halafu hakisimama wakamfukizia mpaka akasimamisha gari wakaenda nae kituo cha police wana mapungufu yao ila ni watu ambao poa sana wana umoja sana.
Tenaa mno.
 
Ana premium insuarance, naona basi jipya linaenda kununuliwa
Screenshot_20240228-102218_Chrome.jpg
 
Basi la Kampuni ya Sai Baba linalofanya Safari kutoka Dar es Salaam kuelekea Mkoani Arusha limeteketezwa kwa Moto mara baada ya kusababisha Ajali kwa kumgonga Dereva wa Bodaboda na kudaiwa kusababisha kifo kwa dereva huyo wa Bodaboda katika eneo la Msambiazi wilayani Korogwe mkoani Tanga leo Februari 27, 2024.

Waendesha Pikipiki (Bodaboda) katika eneo hilo wamejichukulia sheria mkononi mara baada ya kushuhudia ajali hiyo ikitokea kwa kulichoma basi hilo moto kwa kutumia mafuta ya Petroli.

View attachment 2918376View attachment 2918378View attachment 2918377
Bodaboda alikuwa analipita lori bila kuangalia mbele akajiingiza kwanye basi, picha inaonesha magurudumu ya kushoto yako sehemu yake sahihi karibu na msitari wa rangi ya chungwa.
 
Habari zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa kundi la waendesha bodaboda, leo Februari 27, 2024 wamelichoma moto na kuliteketeza basi linalodaiwa kuwa ni mali ya Kampuni ya Saibaba, lililokuwa linatoka jijini Dar es Salaam kuelekea Arusha, baada ya kudaiwa kumgonga bodaboda mmoja na kusababisha kifo chake.

Habari zilizotufikia hivi punde, zimeeleza kuwa tukio hilo limetokea katika eneo la Kona ya Semkiwa, Korogwe mkoani Tanga na kusababisha kukatika kwa mawasiliano kati ya pande mbili za barabara hiyo, jambo lililosababisha foleni iliyodumu kwa takribani saa mbili.

Kwa mujibu wa mashuhuda, baada ya ajali iliyosababisha kifo cha mwendesha bodaboda, wenzake walijikusanya na kulizingira basi hilo, wakawaamuru abiria wote kushuka na kushusha mizigo yao kabla ya kuliteketeza kwa moto.

Mbona picha inaonesha basi liko upande wake sahihi, angalia magurudumu ya kushoto yapo kwenye msitari wa orenji wa kushoto, ni dhahiri bodaboda alijiingiza kwenye basi.
 
Ila saibaba ruti nyiingi mara mbeya,kampala,masasi,tanga,sumbawanga...gari zenyewe sasa vichekesho.
 
Navyofahamu mimi waendesha pikipiki huwa na adabu sana kwa mabus ila madereva wa haya mabus hujiona wao ndio wenye haki ya barabara. Pia huwa na viburi sana barabarani.

Imeshawahi kunitokea, nilikuwa natoka kisesa Mwanza naelekea mjini na kipikipiki changu. Mbele yangu kulikuwa na Lori linatokea mjini na nyuma yake ilikwepo bus ya Zakaria. Ghafla bus likaovertake likajaa upande wangu na sikua na nafasi ya kupita. Ilibidi niingize pikipiki mtaroni ili kuepuka kusababishiwa ajali.

Mara nyingi hakuna haki yoyote anapata bodaboda akigongwa na bus, hii imesababisha hasira kwa hawa watu, wanaona nibora mmalizane upate hasara kuliko kwenda kuzungushwa kisha aambulie patupu.
Tusitetee bodaboda. Hawa jamaa ni wapuuzi mno hawana akili kabisa. Mbona hujasikia baiskeli hapo kagongwa au hata gari ndogo kila mara ni wao mwendo kasi Dar e salaam unakuta wao. Sasa niambie mwenye basi kawakosea nini kumtia hasara? abiria kosa lao lipi kuwatia hasara? haya uharibifu wa barabara hapo bado huoni hawa wajinga ni wapumbavu sana. Hujakutana nao ndiyo maana unawatetea jamaa wanatuharibia magari mno bumper wanazipitia na side mirror kiufupi ni wapuuzi.
 
Back
Top Bottom