Korogwe: Bodaboda wadaiwa kuchoma basi la Saibaba baada ya mwenzao kugongwa

Korogwe: Bodaboda wadaiwa kuchoma basi la Saibaba baada ya mwenzao kugongwa

Yule aliyosema bodaboda ni LAANA naanza kumuelewa.
Kwa hapa DAR sijaona sehemu yenye shida kuendesha gari kama hii barabara ya kutoka mbagala - chamazi kama wewe ni dereva ebu njoo kwenye hii barabara hakika unaweza kupaki gari pembeni ili bodaboda wapite
 
Zamani dereva alikuwa anaambiwa heshimu mtu yoyote anaetembea barabarani.Siku hizi madereva hawaheshimu matokeo yake ndo haya.Ajali nyingi za bodaboda huwa zinatokea iweje leo inawezekana kuna kitu.Madereva wa mabasi makubwa pamoja na haraka zenu muwapo barabarani jitahidi kujali watembea kwa miguu na hata pikpik maana huwa nao ni binadamu wengine wanategemewa pia.
Wewe kama sio dereva hauwezi kuona kero za bodaboda hawa jamaa ni hatari sana na hakuna wanachojua zaidi ya breki na kukanyaga mafuta Tu...ukiona Hadi bungeni nako wameanza kuwa na mashaka dhidi ya bodaboda ujue hapo kuna shida
 
Mkuu usiombee hivyo hayo majamaa mapuuzi sana sijui yanavutaga bangi? Yanaweza kukudhibiti yakakuchoma pamoja na gari! Kuna jirani yetu mtaa wa tatu yalimpiga mawe mpaka kupelekea kifo chake! Kosa alilolifanya ni kutoa bastola na kupiga hewani baada ya dereva kuchoropoka!
Mi nikitembea na cha moto sipigi hewani, nawalamba tu. Ukiwachekea wanakuua. Kama jirani yako ni kisa kilichotokea Dodoma mwaka jana, namjua huyo jamaa alikuwa mwanajeshi.
 
Innaa lillaahi wainnaa ilaihi raaji'un, poleni sanaa wanafamilia wa boda boda, pia pole sana tajiri wa bus hilo.

Ila boda boda mmezidi sana, sasa mnalichoma bus kwa kumkomoa nani! Dereva sio bus lake, anaeumia ni tajiri. Sasa mtaenda kujieleza mahakamani kwa uhalifu huo.
 
Kwahiyo hapa abiria wakashuka wakala pembeni wakishudia Maafisa Ubashiri wakifanya Yao, mpaka wanashusha mizigo hakuna hata alieonyesha juhudi ya kuita polisi maana pale Msambiazi ni hatua chache toka Korogwe stand wangeweka road block Kwa boda zote zinazotoka Msambiazi labda kama waamue kwenda Mombo nako wangekamatwa
aisee abiria walishushwa kwa vioo kupigwa mawe na baadhi ya vitu vya abiria vilibebwa na hao boda boda
 
Basi la Kampuni ya Sai Baba linalofanya Safari kutoka Dar es Salaam kuelekea Mkoani Arusha limeteketezwa kwa Moto mara baada ya kusababisha Ajali kwa kumgonga Dereva wa Bodaboda na kudaiwa kusababisha kifo kwa dereva huyo wa Bodaboda katika eneo la Msambiazi wilayani Korogwe mkoani Tanga leo Februari 27, 2024.

Waendesha Pikipiki (Bodaboda) katika eneo hilo wamejichukulia sheria mkononi mara baada ya kushuhudia ajali hiyo ikitokea kwa kulichoma basi hilo moto kwa kutumia mafuta ya Petroli.





View attachment 2918376View attachment 2918378View attachment 2918377
Lema aliwahi kusema bodaboda ni laana, mkampinga, ona sasa bangi, pombe kali ndiyo zinawadrive.
 
Duu kampuni yenyewe ishajichokea inatembea jina tuu,
Hilo basi lililochomwa ndio First Class yake.

Polisi nao walikua wapi? Si wapo karibu tuu hapo.
kuna polisi alifika mwanzo hakuwa na silaha yoyote nae alizidiwa nguvu jamaa walikuwa na dumu lenye petrol
 
Wewe kama sio dereva hauwezi kuona kero za bodaboda hawa jamaa ni hatari sana na hakuna wanachojua zaidi ya breki na kukanyaga mafuta Tu...ukiona Hadi bungeni nako wameanza kuwa na mashaka dhidi ya bodaboda ujue hapo kuna shida
Imagine tungekuwa tunaishi bila sheria maisha yangekuwaje
Wewe muendesha gari je kungekuwa hakuna sheria zinazokubana mambo yangekuwaje
Hivi unaweza kuvumilia foleni na wakati unaweza kuchepuka ukatokea mbele na ukaendelea na safari bila shida yoyote?
Boda wako sahihi
Unajua kuwa foleni nyingi sababu ni kukosa ustaarabu kwa madereva?
Hivi unajua magari ya viongozi na serikali yako rafu barabarani kuliko hao boda
 
Back
Top Bottom